Kuna sehemu kwenye katiba inasema 'makamu aliyepigiwa kura'?
Katiba inasema, naomba kunukuu;
"Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano..."
Ukisoma hiyo ibara ya 37 kifungu cha 5, haitanabaishi kuwa awe makamu aliyepigiwa kura.
Awe aliyekuwa mgombea mwenza ama aliyepatikana kwa njia za kikatiba baada ya aliyekuepo kutangulia, kujiuzulu, au kuondoka kwa namna yeyote ile.