residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 8,146
- 11,434
Wewe jamaa ni mgumu kuelewa,unasadifu id yako.Wewe mwanasaccos hapo Afrika ya Kusini tu wameamua Kiswahili kuingizwa kwenye mtaala wao wakufundishia kwenye shule zao!! Wewe unadharau kiswahili!!
Ndio maana nikasema ukiweka juhudi, unaweza kujifunza lugha yoyote unayotaka duniani. Darasa linakupa mwongozo tu, lakini ukitaka kujua kitu kiundani ni juhudi zako.Kama umekaa Ulaya kizazi kipya wote wanajifunza kiingereza..cc Christiano Ronaldo
Tena yule waziri wa Elimu,Ndalichako ni muhanga wa lugha kuliko hata Jiwe!
Sasa si ungenielewesha ndugu.ndo ulichoelewa?
Sisi na nani weweee?Kwa sisi werevu hatuwezi kumpa kura yetu Lissu piga ua. Ila kwa wale wadukuwaji ndo mtakaompa kura lissu. Kila la heri kutuuza watanzania.
Lissu utajiangusha sana akishikilia Bango la lugha. Nimesikia mara nyingi akieleza jinsi mtu/kiongozi fulani eti anakiingerereza kibaya kweli kweli. Ajikite kwenye utendaji zaidi.Sasa si ungenielewesha ndugu.
Kiin
Navyojuwa mimi dunia imebadilika sana, watu wa jamii mbili tofauti wanauwezo wa kubadilishana mawazo au hata kufanya biashara kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Kujuwa kingereza sio jambo baya lakini kisiwe kipimo cha maarifa ya mtu kama vile Tundu Lissu anavyotuaminisha kwamba, baadhi ya majaji hawajui kingereza hivyo hawana uwezo wa kutoa hukumu mahakamani.
Marekani na Uingereza lugha ni Kingereza. Je, Urusi, China, Ujerumani lugha ni Kiingereza?Acha uongo :ulisikia wapi Marekani au UK private schools na government schools wanafundishwa kwa lugha mbili tofauti kama Tanzania😂😂au bado haujajua shule za msingi Tanzania mfumo wake haupo sawa kwa iyo unaona fresh tu watoto wengine wapewe elimu kwa English na wengine kwa Kiswahili😂😂 tulia tafakari vizuri utaona kasoro , ila lugha ya kufundishia kuanzia secondary hadi chuo ipo fresh tatizo hapo kwenye primary schools,*&nursery
Tuache upotoshaji. Lissu hakuchagua Kiingereza, bali alisema tuna muda mfupi wa kukielewa shuleni, kwa hiyo tuwe na mjadala ni lugha ipi tufundishie kwa muda wote. Na wewe hapa hutofautishi kati ya lugha ya kufundishia na lugha iliyo katika mtaala. Kiswahili si lugha ya kufundishia Afrika Kusini. Mimi sikubaliani na uchambuzi wa Lissu. Mfumo wa lugha za kufundishia Tz ni wa tangu ukoloni.Wewe mwanasaccos hapo Afrika ya Kusini tu wameamua Kiswahili kuingizwa kwenye mtaala wao wakufundishia kwenye shule zao!! Wewe unadharau Kiswahili!
Nimefurahi umeileta Urusi humu. Urusi, Norway na mahali pengi wanafundisha kwa lugha zao, lakini wanajifunza Kiingereza kuanzia Year 3 kama Tz. Tofauti ni kuwa wanaendelea na lugha yao kwa kufundishia, lakini wanaweka mkazo mkubwa kujua Kiingereza, na mwalimu kutoka nje akifundisha Chuo Kikuu cha kwao ana hiari ya kutumia Kiingereza. Vitabu vipo katika lugha hizo mbili Chuo Kikuu.Marekqni na uingereza lugha ni kingereza..je urusi china ujerumani lugha ni kiingereza?
Mbona umehamia kwa Kiingereza peke yako? Tunachotaka ni lugha moja ya kufundishia ama Kiswahili au Kiingereza, jikite hapoKwa dunia ya leo lugha sio kigezo cha kumkwamisha mwekezaji kuwekeza na kupata matokeo chanya. Lissu mwenye amekaa Ubelgiji miaka 3, je alikuwa anaongea kifaransa, ki datchi au kijerumani? Kama unataka kuongea kiingereza au lugha yoyote ile ni juhudi zako mwenye zitakusaidia na utaongea tu.
Huko sahihi kabsa, kwa sasa kijana kamaliza chuo kikuu hata msg za kawaida unaona anaandika vitu vya ajabu.Tatizo la lugha Tanzania limekua kubwa, hata Kiswahili chenyewe kinatushinda. Ukisoma machapisho ya watu humu JF utagundua hata kiswahili hatujui kuandika vizuri. Najiuliza kama Taifa tunaelekea wapi? Hatupo kwenye English wala Kiswahili. majirani zetu ambao tunapenda kujlinganisha nao Wakenya. Siku hizi wanafusnwa kiswahili vizuri kuliko sisi. Wao wanamafaa kuliko sisi kwa vile wanajua Kingereza vizuri na Kiawahili wanakijua vyema.
Nchi yetu ina lugha mbili zinazokubalika katika shughuli za kila siku, iwe kibiashara au kijamii nazo ni kingereza na kiswahili. Mh. Lissu analamika kusema tuna tapa tapa kwenye hizo lugha mbili na kuna baadhi ya watu hawazijuwi kwa ufasaha maana hawajui wa Hague ipi. Mimi nasema lugha sio kigezo kusema fulani ana akili au hana. Elimu inaweza kutolewa kwa lugha zaidi ya moja na watu wakaelimika.Mbona umehamia kwa kiingereza peke yako? tunachotaka ni lugha moja ya kufundishia ama kiswahili au kiingereza, jikite hapo
Wewe ni lazima uunge mkono[emoji23][emoji23]Naunga mkono hoja asilimia 100
Kukosa kwako kazi kwenye Mashirika ya Kimataifa kunachangiwa na mambo mengi, siyo ligha, ni swala la Network yako Mkuu haisomi vizuri!English ni lugha inayotumika duniani kibiashara, kweye vyuo vikuu ndio maana watz wengi wanakosa kazi kwenye mashirika ya kimataifa sababu hawawezi kujieleza kiufasaha.