Uchaguzi 2020 Tuikomboe Tanzania kupitia Lissu, hakuna nchi Duniani ina mifumo miwili ya lugha za kufundishia

Uchaguzi 2020 Tuikomboe Tanzania kupitia Lissu, hakuna nchi Duniani ina mifumo miwili ya lugha za kufundishia

Wewe mwanasaccos hapo Afrika ya Kusini tu wameamua Kiswahili kuingizwa kwenye mtaala wao wakufundishia kwenye shule zao!! Wewe unadharau kiswahili!!
Wewe jamaa ni mgumu kuelewa,unasadifu id yako.

Kuna umuhimu wa kuwa na lugha mbili za kufundishia ambazo zote mbili huzielewi vyema!?

Kwa nini tusiwe na mjadala wa kitaifa kuwa ama tufundishe kwa kiingereza au kwa kiswahili tangu chekechea mpaka chuo kikuu.

Lugha inasababisha mkose maarifa yanayotakiwa muwe nayo kulingana na kiwango cha elimu mlichofikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama umekaa Ulaya kizazi kipya wote wanajifunza kiingereza..cc Christiano Ronaldo
Ndio maana nikasema ukiweka juhudi, unaweza kujifunza lugha yoyote unayotaka duniani. Darasa linakupa mwongozo tu, lakini ukitaka kujua kitu kiundani ni juhudi zako.
 
ndo ulichoelewa?
Sasa si ungenielewesha ndugu.

Navyojuwa mimi dunia imebadilika sana, watu wa jamii mbili tofauti wanauwezo wa kubadilishana mawazo au hata kufanya biashara kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Kujuwa kingereza sio jambo baya lakini kisiwe kipimo cha maarifa ya mtu kama vile Tundu Lissu anavyotuaminisha kwamba, baadhi ya majaji hawajui kingereza hivyo hawana uwezo wa kutoa hukumu mahakamani.
 
Kwa sisi werevu hatuwezi kumpa kura yetu Lissu piga ua. Ila kwa wale wadukuwaji ndo mtakaompa kura lissu. Kila la heri kutuuza watanzania.
Sisi na nani weweee?
 
Si kweli, kauli yako juu ya lugha ya kufundishi ni potovu na haijafanya utafiti wa kutosha. Kuna mifano mingi lakini anza na India
 
Sasa si ungenielewesha ndugu.
Kiin
Navyojuwa mimi dunia imebadilika sana, watu wa jamii mbili tofauti wanauwezo wa kubadilishana mawazo au hata kufanya biashara kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Kujuwa kingereza sio jambo baya lakini kisiwe kipimo cha maarifa ya mtu kama vile Tundu Lissu anavyotuaminisha kwamba, baadhi ya majaji hawajui kingereza hivyo hawana uwezo wa kutoa hukumu mahakamani.
Lissu utajiangusha sana akishikilia Bango la lugha. Nimesikia mara nyingi akieleza jinsi mtu/kiongozi fulani eti anakiingerereza kibaya kweli kweli. Ajikite kwenye utendaji zaidi.
 
Akili kubwa Tundu Lissu anaeleweka sana. Kura za kutosha kwa Rais wetu kipenzi
 
Acha uongo :ulisikia wapi Marekani au UK private schools na government schools wanafundishwa kwa lugha mbili tofauti kama Tanzania😂😂au bado haujajua shule za msingi Tanzania mfumo wake haupo sawa kwa iyo unaona fresh tu watoto wengine wapewe elimu kwa English na wengine kwa Kiswahili😂😂 tulia tafakari vizuri utaona kasoro , ila lugha ya kufundishia kuanzia secondary hadi chuo ipo fresh tatizo hapo kwenye primary schools,*&nursery
Marekani na Uingereza lugha ni Kingereza. Je, Urusi, China, Ujerumani lugha ni Kiingereza?
 
Wewe mwanasaccos hapo Afrika ya Kusini tu wameamua Kiswahili kuingizwa kwenye mtaala wao wakufundishia kwenye shule zao!! Wewe unadharau Kiswahili!
Tuache upotoshaji. Lissu hakuchagua Kiingereza, bali alisema tuna muda mfupi wa kukielewa shuleni, kwa hiyo tuwe na mjadala ni lugha ipi tufundishie kwa muda wote. Na wewe hapa hutofautishi kati ya lugha ya kufundishia na lugha iliyo katika mtaala. Kiswahili si lugha ya kufundishia Afrika Kusini. Mimi sikubaliani na uchambuzi wa Lissu. Mfumo wa lugha za kufundishia Tz ni wa tangu ukoloni.

Kiingereza kinaanza darasa la tatu. Hadi Kidato cha nne ni miaka 9 ya Kiingereza. Inatosha kukijua. Ilikuwa inatosha kwa walioishia darasa la 8 zamani, tena wa kijijini. Tatizo si muda bali kukosa weledi kwa walimu tangu wakati wa UPE, na kutojali kwa wanafunzi wa sasa. Kiswahili nacho hawakiandiki kwa ufasaha.

Hata hivyo, huko huko kijijini, ndani ya shule za kata, unapata walimu wenye weledi na wanafunzi makini wanaomudu kiingereza. Ni mmoja mmoja, lakini wapo. Tukomae na lugha zote mbili kama zilivyo, maana Kiingereza ndicho Kiswahili cha Dunia.
 
Marekqni na uingereza lugha ni kingereza..je urusi china ujerumani lugha ni kiingereza?
Nimefurahi umeileta Urusi humu. Urusi, Norway na mahali pengi wanafundisha kwa lugha zao, lakini wanajifunza Kiingereza kuanzia Year 3 kama Tz. Tofauti ni kuwa wanaendelea na lugha yao kwa kufundishia, lakini wanaweka mkazo mkubwa kujua Kiingereza, na mwalimu kutoka nje akifundisha Chuo Kikuu cha kwao ana hiari ya kutumia Kiingereza. Vitabu vipo katika lugha hizo mbili Chuo Kikuu.
 
Kwa dunia ya leo lugha sio kigezo cha kumkwamisha mwekezaji kuwekeza na kupata matokeo chanya. Lissu mwenye amekaa Ubelgiji miaka 3, je alikuwa anaongea kifaransa, ki datchi au kijerumani? Kama unataka kuongea kiingereza au lugha yoyote ile ni juhudi zako mwenye zitakusaidia na utaongea tu.
Mbona umehamia kwa Kiingereza peke yako? Tunachotaka ni lugha moja ya kufundishia ama Kiswahili au Kiingereza, jikite hapo
 
Tatizo la lugha Tanzania limekua kubwa, hata Kiswahili chenyewe kinatushinda. Ukisoma machapisho ya watu humu JF utagundua hata kiswahili hatujui kuandika vizuri. Najiuliza kama Taifa tunaelekea wapi? Hatupo kwenye English wala Kiswahili. majirani zetu ambao tunapenda kujlinganisha nao Wakenya. Siku hizi wanafusnwa kiswahili vizuri kuliko sisi. Wao wanamafaa kuliko sisi kwa vile wanajua Kingereza vizuri na Kiawahili wanakijua vyema.
Huko sahihi kabsa, kwa sasa kijana kamaliza chuo kikuu hata msg za kawaida unaona anaandika vitu vya ajabu.
 
Wewe ni muongo. Kinacho kusukuma kwenye thread hii ni ushabiki wa party politics kuliko ukweli. Kwanza, siyo kweli kwamba hakuna nchi duniani yenye lugha tofauti za kufundishia. SIYO KWELI. Nitakuwa mifano michache.

Canada ni taifa kubwa duniani. Kwenye baadhi ya majimbo wanatumia kifaransa na mengine kingereza. Switzerland wana lugha 3 za taifa: Kitaliano, Kifaransa na Kijerumani. Mwanafunzi anaweza kuwa amejifunzia kifaransa primary school kwenye jimbo la kifaransa na baadae akaenda kusoma degree kwa kiingereza kwenye jimbo la kiingereza na bado akafanya vizuri.

Pili, kuna watanzania wengi kama mimi walio maliza form 6 kwa kiingereza na baadae kwenda kwenye masomo nchi za nje zinazotumia totally lugha tofauti kama Urusi, Bulgaria, Poland, China, Hungary, France, n.k. lakini still wakafanya vizuri kwenye masomo yao kuliko wazawa kwa kujifunza kwa muda mfupi lugha husika. Muhimu hapa ni ubora wa elimu na ubora wa ufundishaji, ambalo ni tatizo kubwa.

Tatu, pamoja na kwamba wewe unaelekea kuwa mpenda "lugha za kugeni" iwe lugha ya kufundushia Lisu anasema wazi kiswahili iwe ndo lugha hiyo ALL THE WAY. Nina hakika kwa msimamo huo wa Lisu hata ndani ya Chadema ni wachache watakao kubaliana na mlengo huo. Narudia tena, issue ni ubora wa elimu inayotolewa - walimu, mitaala, vifaa, mifumo, n.k. including udhaifu wa kutojua lugha husika.
 
Mbona umehamia kwa kiingereza peke yako? tunachotaka ni lugha moja ya kufundishia ama kiswahili au kiingereza, jikite hapo
Nchi yetu ina lugha mbili zinazokubalika katika shughuli za kila siku, iwe kibiashara au kijamii nazo ni kingereza na kiswahili. Mh. Lissu analamika kusema tuna tapa tapa kwenye hizo lugha mbili na kuna baadhi ya watu hawazijuwi kwa ufasaha maana hawajui wa Hague ipi. Mimi nasema lugha sio kigezo kusema fulani ana akili au hana. Elimu inaweza kutolewa kwa lugha zaidi ya moja na watu wakaelimika.

Wenzetu Afrika kusini wanalugha 11 zinazotambulika kitaifa na mbili kati ya hizi zinatumika kwenye elimu, kijamii na kibiashara. Ubelgiji wana lugha tatu, Canada wana mbili na maisha yanaendelea.
 
English ni lugha inayotumika duniani kibiashara, kweye vyuo vikuu ndio maana watz wengi wanakosa kazi kwenye mashirika ya kimataifa sababu hawawezi kujieleza kiufasaha.
Kukosa kwako kazi kwenye Mashirika ya Kimataifa kunachangiwa na mambo mengi, siyo ligha, ni swala la Network yako Mkuu haisomi vizuri!
 
Back
Top Bottom