Wewe ni muongo. Kinacho kusukuma kwenye thread hii ni ushabiki wa party politics kuliko ukweli. Kwanza, siyo kweli kwamba hakuna nchi duniani yenye lugha tofauti za kufundishia. SIYO KWELI. Nitakuwa mifano michache.
Canada ni taifa kubwa duniani. Kwenye baadhi ya majimbo wanatumia kifaransa na mengine kingereza. Switzerland wana lugha 3 za taifa: Kitaliano, Kifaransa na Kijerumani. Mwanafunzi anaweza kuwa amejifunzia kifaransa primary school kwenye jimbo la kifaransa na baadae akaenda kusoma degree kwa kiingereza kwenye jimbo la kiingereza na bado akafanya vizuri.
Pili, kuna watanzania wengi kama mimi walio maliza form 6 kwa kiingereza na baadae kwenda kwenye masomo nchi za nje zinazotumia totally lugha tofauti kama Urusi, Bulgaria, Poland, China, Hungary, France, n.k. lakini still wakafanya vizuri kwenye masomo yao kuliko wazawa kwa kujifunza kwa muda mfupi lugha husika. Muhimu hapa ni ubora wa elimu na ubora wa ufundishaji, ambalo ni tatizo kubwa.
Tatu, pamoja na kwamba wewe unaelekea kuwa mpenda "lugha za kugeni" iwe lugha ya kufundushia Lisu anasema wazi kiswahili iwe ndo lugha hiyo ALL THE WAY. Nina hakika kwa msimamo huo wa Lisu hata ndani ya Chadema ni wachache watakao kubaliana na mlengo huo. Narudia tena, issue ni ubora wa elimu inayotolewa - walimu, mitaala, vifaa, mifumo, n.k. including udhaifu wa kutojua lugha husika.