Uchaguzi 2020 Tuikomboe Tanzania kupitia Lissu, hakuna nchi Duniani ina mifumo miwili ya lugha za kufundishia

Uchaguzi 2020 Tuikomboe Tanzania kupitia Lissu, hakuna nchi Duniani ina mifumo miwili ya lugha za kufundishia

Una point ila kuhusu Lugha za kufundishia hiyo mbona ipo kwa Nchi nyiingi zilizoendelea (Nchi nyingi tu za Ulaya ambazo Kiingereza sio Lugha ya kwanza wana mtaala wa Lugha yao ya Asili na Mtaala mwingine wa Kiingereza na Hata Vyuo hadi Vyuo Vikuu; Mtu akitaka kuomba kutokea Nje mfano Africa, anatakiwa kuwa makini kuomba chenye mtaala wa Kiingereza
Uliza China, Ujerumani, Holand nk
Acha uongo :ulisikia wapi Marekani au UK private schools na government schools wanafundishwa kwa lugha mbili tofauti kama Tanzania😂😂au bado haujajua shule za msingi Tanzania mfumo wake haupo sawa kwa iyo unaona fresh tu watoto wengine wapewe elimu kwa English na wengine kwa Kiswahili😂😂 tulia tafakari vizuri utaona kasoro , ila lugha ya kufundishia kuanzia secondary hadi chuo ipo fresh tatizo hapo kwenye primary schools,*&nursery
 
Una point ila kuhusu Lugha za kufundishia hiyo mbona ipo kwa Nchi nyiingi zilizoendelea (Nchi nyingi tu za Ulaya ambazo Kiingereza sio Lugha ya kwanza wana mtaala wa Lugha yao ya Asili na Mtaala mwingine wa Kiingereza na Hata Vyuo hadi Vyuo Vikuu; Mtu akitaka kuomba kutokea Nje mfano Africa, anatakiwa kuwa makini kuomba chenye mtaala wa Kiingereza. Uliza China, Ujerumani, Holand nk
Kwa elimuya juu hakuna shida kwa vile watu walishajengewa msingi mzuri huko chini. naweza kuwa sina tarifa za kila nchi. lakini tukubali lugha ni tatizo kubwa kwa elimu yetu. Naona huu ni wakati muafaka tuchue hatua nchi yetu inaelekea baya.
 
Uongo
Una point ila kuhusu Lugha za kufundishia hiyo mbona ipo kwa Nchi nyiingi zilizoendelea (Nchi nyingi tu za Ulaya ambazo Kiingereza sio Lugha ya kwanza wana mtaala wa Lugha yao ya Asili na Mtaala mwingine wa Kiingereza na Hata Vyuo hadi Vyuo Vikuu; Mtu akitaka kuomba kutokea Nje mfano Africa, anatakiwa kuwa makini kuomba chenye mtaala wa Kiingereza
Uliza China, Ujerumani, Holand nk
 
Shida tupu yani
Tatizo la lugha Tanzania limekua kubwa, hata kiswahili chenyewe kinatushinda. Ukisoma machapisho ya watu humu JF utagundua hata kiswahili hatujui kuandika vizuri. Najiuliza kama Taifa tunaelekea wapi? Hatupo kwenye English wala Kiswahili. majirani zetu ambao tunapenda kujlinganisha nao Wakenya. Siku hizi wanafusnwa kiswahili vizuri kuliko sisi. wao wanamafaa kuliko sisi kwa vile wanajua Kingereza vizuri na Kiawahili wanakijua vyema.
 
Nilishangaa kumuona Profesa Ndalichako hajui kimombo.

Sasa kama Profesa hajui kimombo sisi kajamba nani itakuwaje? Tuna-fake tu ila lugha haipandi.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Ila kitumike kiswahili.

Au kuwe na shule aina 3.

Za english medium na kiswahili medium.

Pia Na kama zilizopo sasa.

Alafu tupime ufanisi wa kila medium.
Lugha iwe moja tu ambayo ni universal language kuanzia primary hadi chuo , waondoe ubaguzi wa lugha za kufundishia , shule za serikali na private zote wafundishe kwa English-language na sio watoto wa mama mmoja ndani ya nyumba moja kila mmoja akienda shule anafundishwa kwa lugha tofauti si vichekesho ivi😂😂 mfano mmezaliwa wawili nyumbani halafu kila mmoja anaongeleshwa lugha tofauti na anayoongeleshwa mwingine ivyo si vichekesho na uliskia wapi mfumo kama huu wa lugha za kufundishia Nursery &primary unatumika Tanzania kwa Private &Government schools?
 
Lugha iwe moja tu ambayo ni universal language kuanzia primary hadi chuo , waondoe ubaguzi wa lugha za kufundishia , shule za serikali na private zote wafundishe kwa English-language na sio watoto wa mama mmoja ndani ya nyumba moja kila mmoja akienda shule anafundishwa kwa lugha tofauti si vichekesho ivi[emoji23][emoji23] mfano mmezaliwa wawili nyumbani halafu kila mmoja anaongeleshwa lugha tofauti na anayoongeleshwa mwingine ivyo si vichekesho na uliskia wapi mfumo kama huu wa lugha za kufundishia Nursery &primary unatumika Tanzania kwa Private &Government schools?
Hapo yanakuwa ni majaribio ili kujua ufanisi wa kila kila lugha. [emoji846]

Ili tusije kurupuka tu eti kiwe kiingereza from nursery.

Hata walimu wenyewe ambao wapo hawawezi kumudu.

Itabidi wazalishwe walimu. Kwa ajili ya mfumo wa kiingereza.
 
Jamani taaluma kwa maana ya elimu ni bidhaa pia. Bidhaa sio Tanzanite, Korosho au Dhahabu tu, wenzetu wanauza wataalamu wao nje na wanaleta pesa nyumbani. Kiswahili chetu ni bidhaa lakini huwezi enda SA kufundisha kiswahili kama hujui English. hivyo tuboreshe hizi lugha.Nilishangaa wakati wa kubadilisha passport nikasikia Watanzania wenye passport kubwa ni kama millioni 1, nikashangaa nchi ya watu 60m. Au lugha inatuangusha ndio maana hatuendi nje?
 
Wewe mwanasaccos hapo Afrika ya Kusini tu wameamua Kiswahili kuingizwa kwenye mtaala wao wakufundishia kwenye shule zao!! Wewe unadharau kiswahili!!
Acha uwongo. Afrika Kusini haijakifanya Kiswahili kuwa ni lugha ya kufundishia masomo bali imekuwa ni kati ya lugha zinazofundishwa shuleni, sawa kama ambavyo Tanzania, baadhi ya shule zinavyofundisha Kifaransa.

Baadhi ya watu, huenda ni kwa sababu ya uelewa mdogo, hata hawaelewi hoja ya Tundu Lisu, ambayo kimsingi ina mantiki kubwa.

Kiswahili ni lugha yetu, kingeweza kutundishwa kama somo la lugha la lazima kwenye ngazi zote. Kiingereza kingefundishwa kama somo la lugha na lugha ya kufundishia masomo ya maarifa.

Ni mjinga pekee anayeweza kuhoji kwa nini Kiingereza kitumike kama lugha ya kufundishia maarifa. Ukweli ni kuwa vyanzo vingi vya maarifa vipo katika lugha ya Kiingereza. Na sisi ni watumiaji wa teknolojia za watu wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo yanakuwa ni majaribio ili kujua ufanisi wa kila kila lugha. [emoji846]

Ili tusije kurupuka tu eti kiwe kiingereza from nursery.

Hata walimu wenyewe ambao wapo hawawezi kumudu.

Itabidi wazalishwe walimu. Kwa ajili ya mfumo wa kiingereza.
Ndio ila majaribio si tayari wameshafanya karibia miaka 50 wamejionea matokeo
 
Ndio ila majaribio si tayari wameshafanya karibia miaka 50 wamejionea matokeo
Lakini hizo shule za nursery na primary za english medium.
Hazijawahi kuwa operated by government.

Ila sawa. Waje wafanye jinsi watakavyoona inafaa.
 
Kama English ndo lugha ya kimataifa mkuu unabisha mifumo ya elimu kwako unaona ipo sawa? Hauoni Tanzania ina mifumo mibovu ya elimu , kwa mfano hauoni elimu ya msingi inaubaguzi kuna wanaofundishwa kwa kiswahili masomo, na kuna wa private wanafundishwa kwa english , kwa nini serikali isiamue elimu itolewe kwa lugha moja kama kiingereza iwe kwa wote private na government school vivyo ivyo chuo ndo itakuwa fresh ,
Nakubaliana na wewe Mfumo wetu wa elimu ni waha hovyo,inabidi ubadilishwe uendane na hali ya sasa
 
Lakini hizo shule za nursery na primary za english medium.
Hazijawahi kuwa operated by government.

Ila sawa. Waje wafanye jinsi watakavyoona
Mkuu waamue moja tu kila mtoto waki Tanzania hapate elimu kwa lugha ya kiingereza kuanzia nursery hadi chuo na sio elimu yao ya sa hivi ya kibaguzi , private &Government shools but different teaching languages
 
Mkuu waamue moja tu kila mtoto waki Tanzania hapate elimu kwa lugha ya kiingereza kuanzia nursery hadi chuo na sio elimu yao ya sa hivi ya kibaguzi , private &Government shools but different teaching languages
Sawa. Ila watoto wengi watakuwa wanaishia primary.
 
Hapo utapaswa kubadili mfumo kuanzia walimu.

Walimu wengi hawamudu kiingereza na watafundisha vipi kwa lugha ya Kiingereza.

Hata vyuo vikuu unakutana na wahadhiri ambao Kiingereza kinawapiga chenga kabisa.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Sawa. Ila watoto wengi watakuwa wanaishia primary.
Kwa nini? Hakuna kitu kama icho we hauoni watoto wanaosoma government schools kwa kiswahili upata shida wanapoingia secondary kuanza kusoma kwa kiingereza, huku wale wa private schools aka English schools wakiyafurahia maisha kwa sababu iyo lugha wamekuwa wakiitumia, au haujui Tanzania waliovizuri kwenye English language wengi ni zao la private schools aka English schools, nenda hata chuo vivyo ivyo
 
Back
Top Bottom