Yaani nashangaa mno watu wanavyojidanganya kuwa lisu ana nguvu sana ya kuitisha CCM!!!, Yule wanajua namna ya kumuendesha kama tiara,CCM ni lidubwashwa kubwa achana na safu ya uongozi unayoiona ya sijui mwenyekiti, makamu, katibu mkuu (na safu nzima ya uongozi).
Hiko chama kina walinzi wake wa kudumu ambao wamebobea kweli-kweli kwenye siasa na washashika nafasi za juu kwenye uongozi za kuendesha taasisi zingine za serikali.
Baada ya pilika za uchaguzi wanaingia kati kuhakikisha watu wanarudi kwenye mstari, kazi yao ni kuilinda CCM.
CDM aina luxury ya kuvurumana wenyewe, shughuli ya kuwaunganisha watu baada ya mgawanyiko wa chaguzi sio ndogo.
CCM wenyewe hawana hizo skills, ni walinzi wao chama ambao ni watu nyeti awali serikalini.
Watu ambao mnadhani siasa za Lissu ni sahihi amuielewi CCM, unadhani ni ya mzaha-mzaha.
Sasa kama CCM chama kikongwe kinategemea walinzi wake waliobobea kwenye siasa na walikuwa na nafasi nyeti serikalini huko nyuma kuwaweka sawa.
Jiulize CDM ambayo aina hao watu, hao NCCR Mageuzi na CUF havikudhoofika bure bure.
Political tip (CCM awabahatishi umoja wao).
Kushabikia siasa za Lissu ni utoto tu wa kutoelewa siasa za Tanzania.
Wanamtafutia mtu mmoja tuu serikalini, kazi yake ni kumlisha fake informations!!! Ndani ya mwezi tuu anadharaulika