Tujadili: Kuuliza bei kila muda

Tujadili: Kuuliza bei kila muda

Mzee Saliboko

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2018
Posts
1,311
Reaction score
1,018
Habari zenu,

Kuna hili suala nataka tujadili. Kuna hii hali ya wateja wanaokuja kwako mara kwa mara kununua bidhaa lakini kila wakija lazima waulizie bei.

Je, hii ni sahihi?
 
Ni sahihi sana, Demand is the function of Price.

Halafu wafanya biashara wa Tanzania sio waaminifu. Kitu kinauzwa 1800 lakini akija mtu akakupa 2000 basi haurudishi chenji unasema bei ni 2000. Yaani ilimradi tu uibe hiyo 200.

Na mimi huwa nauliza bei, maana kichwani tayar nina bei elekezi ukiongeza hata mia sinunui
 
Hii ndo akili ya wafanyabiashara wengi wa Kitanzania; hataki kuulizwa bei, kiburi kwa wateja, lugha mbaya na ya mkato, kuangalia mtu anayeingia dukani ndo waamue kumjibu bei au la, akianza kupata vipesa kidogo atauliza kama ni sahihi kumjibu mteja bei za bidhaa zake. So arrogant and naive.

Usiwajibu bei mkuu ni usumbufu; endelea kuchati na simu wateja wakija ofsini kwako.
 
Mdanganye mwenzako Sasa ajichanganye kama atapata wateja
 
Habari zenu,

Kuna hili suala nataka tujadili. Kuna hii hali ya wateja wanaokuja kwako mara kwa mara kununua bidhaa lakini kila wakija lazima waulizie bei.

Je, hii ni sahihi?
Bei hubadilika. Vituo vya mafuta wana mabango yanayoonyesha bei, na vile vile kuna controllers wa bei.
Wewe kama hutaki kuulizwa bei kila wakati, FANYA KAMA SUPER MARKET, BANDIKA BEI KWENYE KILA BIDHAA UNAYOIUZA
 
Ni sahihi sababu Bei ubadilika badilika,pili wengi ununua kwa kulinganisha Bei na maduka mengine
 
Kuuliza Bei sio kununua tena mtu ambae ajanunua yafaa umpokee vizur sana ili kesho aje.
Watu ni wa aina mbili mmoja wa Leo mwingine ni wa kesho
 
Habari zenu,

Kuna hili suala nataka tujadili. Kuna hii hali ya wateja wanaokuja kwako mara kwa mara kununua bidhaa lakini kila wakija lazima waulizie bei.

Je, hii ni sahihi?
Mteja anauliza bei hata kwenye bidhaa yenye price tag, na unatakiwa umjibu. Hata kama mtoto, sasa leta dharau utafurahi
 
Thus anaweza akaulizia Bei akaaga atazunguka wee akikuta huko kubwa akirudi Mara ya pili kaja na Hela Sasa kama ulimjibu vibaya na Hela yake utaikosa.
 
Kuuliza Bei sio kununua tena mtu ambae ajanunua yafaa umpokee vizur sana ili kesho aje.
Watu ni wa aina mbili mmoja wa Leo mwingine ni wa kesho
Kuna mtu anakuja anaulizia bei na hanunui ukwel ulivyosema kuwa huyo ambaye hanunui ndo WA kuwa nae kalibu sababu ya kutengeneza mnyororo mwingne WA watej,, wafanya biashala weng wamekalili wateja wao ila kutengeneza namna nyingne ya kupata watej Kwa wingi wanashindwa
 
Thus anaweza akaulizia Bei akaaga atazunguka wee akikuta huko kubwa akirudi Mara ya pili kaja na Hela Sasa kama ulimjibu vibaya na Hela yake utaikosa.
Kama ulimjibu mwanz ndo umemkosa hvyo Tena,, ko kama jamaa alivyosema hapo Kuna wateja WA Leo na Kuna wateja WA kesho,
 
Back
Top Bottom