Tujadili Mfumo wa Elimu utakaotufaa Tanzania. Maoni yataunganishwa na kufikishwa Bungeni na Serikalini

Tujadili Mfumo wa Elimu utakaotufaa Tanzania. Maoni yataunganishwa na kufikishwa Bungeni na Serikalini

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
3,880
Reaction score
11,134
Members, Huu uzi ni kwa ajili ya kutoa ushauri, Maoni na Marekebisho kuhusu mfumo wetu wa elimu Tanzania.

Hoja zitakazotolewa hapa zitaunganishwa na kuwafikishia wahusika Bungeni na kwenye mamlaka ya Serikali.

Tujadili ni aina gani ya masomo tunayohitaji yafundishwe kwa watoto wetu, Watoto wetu wasome kwa miaka mingapi?

Tujadili mtoto amalizapo kila ngazi ya elimu awe na ujuzi na uwezo wa kufanya jambo gani?

Tujadili aina za shule tunazozihitaji kwa watoto wetu na aina ya walimu tunaowahitaji kwa ajili ya watoto wetu.

Mfumo wetu wa elimu umeundwa kwa mtoto kuanza chekechea akiwa na miaka mitatu mpaka mitano, Anaanza elimu ya msingi akiwa na miaka sita mpaka nane, Anaishi na elimu ya msingi kwa miaka saba, Baadae elimu ya upili ya Sekondari anaishi kwa miaka minne, Anajiunga na elimu ya juu ya Sekondari kwa mwaka moja na nusu mpaka miaka miwili, Baadae chuo Kikuu kwa shahada ya awali miaka mitatu mpaka mitano.

Kimahesabu mtoto anayesoma kufikia shahada ya awali ukiondoa udaktari na uinjinia anatumia miaka kumi na sita shule, 7+4+2+3=16

Je, ni sahihi mtoto kukaa miaka kumi na sita shule anaondoka bila ujuzi wowote ule.

Mtoto unampokea nyumbani tangu alipoanza kuwa bize akiwa na umri wa miaka minne, Anarudi mikononi mwako tena baada ya miaka kumi na sita bila ujuzi wowote.

Tunahitaji maoni yenu na ushauri hapa Jamiiforum, Uzoefu wa kila mmoja wetu unahitajika ili tutengeneze mfumo imara wa elimu kwa vizazi vijavyo.

Nina hakika huu uzi utatoa dira na maono kwa miaka mingi ijayo hapa JamiiForums.

Soma pia:

1) Mfumo wa elimu wa Nchi ya Ufini unavyolifanya Taifa hilo kuwa bora katika elimu Duniani; Tanzania inajifunza nini?

2) Muundo wa Elimu ya Tanzania

3) Kitila Mkumbo: Je, Tanzania tuna mtaala wa elimu?

4) Matatizo matatu katika Mfumo wetu wa Elimu
 
Wabunge wenyewe ni darasa la saba kweli watathamini elimu? Hamna wa bunge wa hovyo kama wa Bunge wasasa hivi, elimu ya Tznia ilitoleea kafara na chama cha CCM, ilikiendelee kutawala tu.
Ni kweli, Lakini tufanyie kazi maoni tutakayotoa hapa

Mkuu toa mawazo yako hata kama hawa wabunge hawafai
 
Lugha ya kufundishia toka chekechea iwe kiingereza, kisha elimu ya nadharia inayolenga kufaulu ipungue, tuwe na elimu ya ujuzi zaidi.

Kwa maneno marahisi sekondari za kukaririsha ili kufaulu zipungue, sekondari nyingi ziwe ni za ujuzi na maarifa.

75% ziwe sekondari za ufundi, na 25% ndio za watu wa maofisini wa utawala.
 
Tubadili mitaala ili iendane Na mazingira yetu.mf tumejaliwa misitu watoto wetu waandaliwe tangu elimu ya awali kujifunza namna kutunza misitu ni lahisi kupata wabobezi wa Mali asili.

Jambo lingine ni kungelikuwa na utaratibu wakulazimisha viongozi wa selikari wa maenoe usika watoto wao kusoma katika shule Za Kata maana wangelikuwa wasimamizi wa elimu yetu lakini hali ilivyo Kwa Sasa wao wamewatenga watoto wao Na elimu inayotolewa Na selikari.
 
Lugha ya kufundishia toka chekechea iwe kiingereza, kisha elimu ya nadharia inayolenga kufaulu ipingue, tuwe na elimu ya ujuzi zaidi. Kwa maneno marahisi sekondari za kukaririsha ili kufaulu zipungue, sekondari nyingi ziwe ni za ujuzi na maarifa. 75% ziwe sekondari za ufundi, na 25% ndio za watu wa maofisini wa utawala.
Je walimu wanaouwezo wa kufundisha masomo kwa kiingereza?

Waanze kwanza huko kwenye vyuo vya ualimu
 
Mimi sio mtaalamu wa haya masuala, lakini naamini Kama taifa tunao wataalam wengi wanaoweza kufanyia kazi hili jambo.

Ushauri wangu tupate katiba mpya itakayowezesha tupate viongozi wanaowajibika, na inayowapa wananchi uwezo mkubwa wa kuwawajibisha viongozi na watumishi wa umma wasiowajibika ktk nafasi zao.

Halafu tuache kuingiza siasa ktk mambo ya kitaalam.

Watumishi na wataalam waachwe watekeleze wajibu wao bila kuingiliwa na wanasiasa
 
Kufanyike mabdiliko katika sehemu 3 muhimu
1) Lugha ya kufundishia
2) Mitaala ya kufundishia
3) Muda wa kuwa shuleni

1. Lugha ya kufundishia
Kiuhalisia watanzania walio wengi wako huru sana kujifunza kwa lugha ya kiswahili na hili mimi mwenyewe ni shuhuda maana kipindi nasoma ngazi ya elimu ya upili na ya juu mwalimu alikua na kazi 2 kuu akiwa darasani: ya kwanza ni kutafsiri dhana (concept) iliyo kwenye mada husika kwa lugha ya kiswahili na pili ni kuifanya dhana ieleweke kwa wanafunzi.

Hii inafanya walimu kutumia nguvu nyingi sana kutoa elimu kwa kutumia Kiswanglish na kwa upande wa lugha haifanyi mwanafunzi kuwa na uwezo (competent) kwenye matumizi ya lugha yeyote iwe kiingereza au kiswahili.

Kwa kutumia kiswahili itawafanya wanafunzi kuwa huru (confortable) zaidi wakati wa jujifunza pia kuwa na uwezo mzuri katika matumizi sahihi ya lugha ya kiswahili.

Pia baada ya maisha ya shule kiuhalisia huku makazini watanzania tulio wengi tunafikiri sana kwa kiswahili vichwani mwetu lakini utendaji mara nyingi tunautafsiri uwe kwa kiingereza ili tuendane na mifumo iliyopo.

Hii inapunguza ufanisi kwa kiwango kikubwa sana. Kwa hiyo kupata ufanisi matumizi ya lugha mama katika kufikiri na kutenda ni muhimu sana.

Najua pia kunaweza kuwa na mashaka kidogo kwenye utimilifu wa lugha ya kiswahili kama lugha ya kufundishia na pia ugumu unaoonekana katika misamiati mbalimbali iliyo katika lugha ya kiswahili; ila ukweli ni kwamba hakuna lugha iliyo timilifu katika elimu na ndio maana hata kiingereza kimeazima misamiati mingi katika kada mbalimbali kama baolojia, fizikia na sheria kutoka lugha ya kilatini, kigiriki nk.

Pia ugumu wa lugha ya kiswahili tunauona kwa sababu sio lugha inayotumika kutufunza tangu tungali wadogo kielimu mpaka tunapokomaa; ni kama tu mtoto wa kisukuma/kichaga ambaye anachanganyiwa lugha katika makuzi yake, akija kukutana na msukuma/mchaga anayeongea lugha ya ndani kabisa (mfano babu zeru wasiojua kabisa kiswahili) basi lazima atasema kisukuma/kichaga cha ndani ni kigumu sana.

2. Mitaala ya kufundishia
Kwa kiwango kikubwa sana mitaala ya elimu yetu imepitwa na wakati na haijumuishi mambo mengi ya sasa. Hili lipo kuanzia ngazi ya shule za msingi mpaka vyuo vikuu. Kuna ulazima sasa wa kuhuisha mitaala yetu iendane na wakati.

Pia sioni ulazima wa mwanafunzi kupata elimu jumuishi (kwa kusoma masomo mengi yasiyowiana) kwa kipindi kirefu na kusoma masomo maalumu (ya michepuo) kwa kipindi kifupi kwani yanadumaza ubunifu/uwezo wa uvumbuzi wa mwanafunzi husika.

Kwa mfano hakuna ulazima wowote wa kusoma masomo tisa au zaidi kwa miaka saba shule ya msingi halafu usome tena masomo tisa yakufanana nayo kwa miaka minne shule ya upili. Nadhani wanafunzi waanze kusomea michepuo mbalimbali baada ya muda usiozidi miaka saba tangu kuanza elimu ya msingi.

3. Muda wa kuwa shuleni
Kwa sasa maisha ya kielimu ya kijana wa Kitanzania yanatumia muda mwingi sana shuleni kujifunza mambo mengi ambayo hayatakuja kumsaidia baadae.

Napendekeza mwanafunzi asitumie zaidi ya miaka kumi na moja (11) shuleni kabla ya kufika elimu ya chuo kikuu kama ilivyo sasa ambapo ni miaka saba ya elimu ya msingi, miaka minne ya elimu ya upili na miaka miwili ya elimu ya juu (jumla ya miaka 13).

Kiuhalisia ni wakati sasa wa kuupunguza muda wa elimu ya msingi na elimu ya upili na kuongeza muda wa elimu ya juu; miaka minne inatosha kabisa kwa elimu ya msingi na miaka mitatu kwa elimu ya upili lakini elimu ya juu yapaswa iwe na walau miaka mitatu hadi minne ambapo mwanafunzi atasoma masomo ya michepuo na baada ya hapo ndipo aende chuo kikuu kusomea fani itakayowiana na kipaji na uwezo wake.

Kwa maana hiyo tunatazamia kijana wa miaka 20 mpaka 22 atakuwa ameshapata elimu na ujuzi wa kutosha kuanza kulijenga taifa letu.

Nawasilisha.
 
Bila mabadiliko ya katiba mtasubiri sana.

Pigeni kelele tupate katiba bora.

Ikishindikana kwa amani twendeni barabarani. Katiba ni haki ya wananchi siyo hisani ya viongozi
 
Mimi kwa mawazo yangu,
Kwanza masomo yapunguzwe. Tukianza na elimu ya msingi, wasome masomo matano tu. kwa mchanganuo ufuatao:-

1. LUGHA [Kiswahili na kiingereza]

2.MAARIFA YA JAMII [Urai, Historia, na elimu ya mazingira na kujitambua]

3.STADI ZA KAZI [Kilimo, uvuvi, ufugaji na ufundi]

4.Sayansi [Jiografia,baiolojia,kemia na fizikia + kompyuta kozi(introduction)]

5. HESABU/HISABATI na BIASHARA
Kwa sekondari nako masomo yapunguzwe.

Wakimaliza shule ya msingi, wanapopangiwa kwenda sekondari basi wa speshelaizi na kombinesheni zao kabisa, yaani ukitoka shule ya msingi unapangiwa kwenda arts, science au business.

Masomo yawe kwa mchanganuo ufuatao:-

1.ARTS [LANGUAGE( kiswahili na kiingereza/kifaransa/kiarabu), + CIVICS and HISTORY + BASIC MATHEMATICS]

2. SCIENCE[PCM,PCB,PGM, CBG n.k + PURE MATHEMATICS]

3. BUSINESS[ECONOMIC, COMMERCE and ACCOUNTANCE + BASIC MATHEMATICS]

4. COMPUTER COURSE iwe kwa wote arts, science na business
-Kingine miaka ya kusoma nayo pia upunguzwe.

Kwa shule za msingi wanafunzi waanze shule wakiwa na miaka 7 baada ya kumaliza elimu ya awali ambayo kwasasa nayo pia iwe ya lazima.

-Shule ya msingi wasome miaka mitano ya darasani na mwaka mmoja wa stadi za kazi wakisubiri kuingia sekondari.

-Kwa sekondari wa wasome miaka minne ya darasani na mwaka mmoja wa stadi za kazi wakisubiri kuingia chuo.

-Baada ya hapo, chuo wasome miaka miwili/mitatu darasani mwaka mmoja kazi kwa vitendo.
Hayo ndo mawazo yangu.
 
Ni kweli yawezekan mh rais anania ya dhati kubadilisha mfumo wa elimu lkn chini ya mfumo wa utawala huu ambao muda wote unajipanga kutawala na si kuongoza atuwezi kupata mfumo bora.

Ubovu wa mfumo wetu wa elimu ni mtaji wa watawala kma tu huu mfumo na ubovu wake wanapata shida watakubali kuweka mfumo mzuri ili watoke madarakan ....

Maoni yngu kwnza tubadilishe mfumo wa kiutawala yan tupate katiba ambayo itaimalisha mifumo ya kitaasisi automatical mfumo wenyew tu utajiseti na utakuwa rafiki kwa taifa letu
 
Back
Top Bottom