Maro bartazaro
Member
- Nov 14, 2021
- 10
- 8
kwani waalimu wanaofundisha english medium watoka vyuo gan?Je walimu wanaouwezo wa kufundisha masomo kwa kiingereza? Waanze kwanza huko kwenye vyuo vya ualimu
Walimu wengi wa shule za serikali hawajui kiingereza sijui wanawatoaga wapikwani waalimu wanaofundisha english medium watoka vyuo gan? ni vyuo hvyo hvyo wanasoma waalim wa shule za serikal
Mfumo haujadiliki isipokuwa vitu vinavouundaMembers, Huu uzi ni kwa ajili ya kutoa ushauri, Maoni na Marekebisho kuhusu mfumo wetu wa elimu Tanzania.
Hoja zitakazotolewa hapa zitaunganishwa na kuwafikishia wahusika Bungeni na kwenye mamlaka ya Serikali.
Tujadili ni aina gani ya masomo tunayohitaji yafundishwe kwa watoto wetu, Watoto wetu wasome kwa miaka mingapi?
Tujadili mtoto amalizapo kila ngazi ya elimu awe na ujuzi na uwezo wa kufanya jambo gani?
Tujadili aina za shule tunazozihitaji kwa watoto wetu na aina ya walimu tunaowahitaji kwa ajili ya watoto wetu.
Mfumo wetu wa elimu umeundwa kwa mtoto kuanza chekechea akiwa na miaka mitatu mpaka mitano, Anaanza elimu ya msingi akiwa na miaka sita mpaka nane, Anaishi na elimu ya msingi kwa miaka saba, Baadae elimu ya upili ya Sekondari anaishi kwa miaka minne, Anajiunga na elimu ya juu ya Sekondari kwa mwaka moja na nusu mpaka miaka miwili, Baadae chuo Kikuu kwa shahada ya awali miaka mitatu mpaka mitano.
Kimahesabu mtoto anayesoma kufikia shahada ya awali ukiondoa udaktari na uinjinia anatumia miaka kumi na sita shule, 7+4+2+3=16
Je, ni sahihi mtoto kukaa miaka kumi na sita shule anaondoka bila ujuzi wowote ule.
Mtoto unampokea nyumbani tangu alipoanza kuwa bize akiwa na umri wa miaka minne, Anarudi mikononi mwako tena baada ya miaka kumi na sita bila ujuzi wowote.
Tunahitaji maoni yenu na ushauri hapa Jamiiforum, Uzoefu wa kila mmoja wetu unahitajika ili tutengeneze mfumo imara wa elimu kwa vizazi vijavyo.
Nina hakika huu uzi utatoa dira na maono kwa miaka mingi ijayo hapa JamiiForums.
Kuna mambo very sensitive tungeweza kushauri lakini ukikumbuka unaokwenda kuwapa mapendekezo walioishia darasa la pili unaishiwa nguvuMkuu tuanze kwanza na mabadiliko ya uendeshaji wa bunge ndiyo tujadili mfumo wa elimu.
Kingereza sio issue mzee Bahresa aliishia darasa la pili hajui kingereza kabisa lakini ni Bilionea anatambuliwa dunia nzimaWalimu wengi wa shule za serikali hawajui kiingereza sijui wanawatoaga wapi
Elimu ya biashara , tena ile practical iingizwe kwenye mtaala toka shule ya msingi hadi chuo kikuu.Kingereza sio issue mzee Bahresa aliishia darasa la pili hajui kingereza kabisa lakini ni Bilionea anatambuliwa dunia nzima
Japan hawatumii kiingereza ,wachina hawatumii kingereza,Wajerumani, warusi wote hawasomeshi English medium lakini wako juu mno kila eneo
Lugha ya kufundishia ikiwa kingereza, taratibu kiswahili kitaanza kufa.Lugha ya kufundishia toka chekechea iwe kiingereza, kisha elimu ya nadharia inayolenga kufaulu ipungue, tuwe na elimu ya ujuzi zaidi. Kwa maneno marahisi sekondari za kukaririsha ili kufaulu zipungue, sekondari nyingi ziwe ni za ujuzi na maarifa. 75% ziwe sekondari za ufundi, na 25% ndio za watu wa maofisini wa utawala.
Tena waalikwe hadi akina mama ntilie wale wa chini kabisa wafundishe kupika vitumbua maandazi nkElimu ya biashara , tena ile practical iingizwe kwenye mtaala toka shule ya msingi hadi chuo kikuu.
Watoto wetu wafundishwe kwa lugha tunayozungumza sisi wazazi, yaan kiswahili kwa ngazi zote za elimu