Tujadili Mfumo wa Elimu utakaotufaa Tanzania. Maoni yataunganishwa na kufikishwa Bungeni na Serikalini

Darasa I-III
Uraia, Kiswahili na Hisabati

IV-VII
Hisabati, Kiswahili, Historia na Ufundi stadi (LEVEL 1)

Form I-IV (LEVEL 2-3)

Hisabati, Kiswahili, Historia na Ufundi stadi
Form V-VI

Hisabati, Kiswahili, Historia na Ufundi stadi (LEVEL 4-6)
Naona umeamua kumtengeneza mswahili

Yaani somo la kiingereza umetupilia
Mbali
 
Serikali iwawezeshe ma professor na research funds nchi haiwezi endelea kama hamna research za maana zinazofanyika
 
Elimu ya chuo wafanye malekebisho sana maana apana kitu pale asa wanao somea uwalimi na shelia wengi upoteza muda
 
Wakafanye case study ya elimu inayo tolewa china,singapore,malaysia na n.k

Halafu waunganishe study na kuja na elimu tendaji ZAIDI kuliko upuuzi Huu uliopo!!!

Mitihani ya Necta ifutwe ibaki mitihani ya faculty husika ndio isimamie na Sio lazima mitihani ifanane bali mazingira yaangaliwe na uzalishaji eneo husika!!!
 
1. Elimu ya msingi ingebakia kwa maboresho ya kuwepo na namna mtoto atajifunza elimu ya msingi vzur na kuifahamu vyema nchi yake kuanzia jiografia, uchumi, siasa

2. Elimu inayofuata iwe ni ya vitendo zaidi(ujuzi + maarifa) ili imuandae mtoto na mazingira halisia ya nchi yake

3. Tuangalie nchi inahitaji sana wataalamu katika sekta hizo na zipewe kipaumbele na siyo kila mwaka vyuoni courses ni zile zile Na admissions zinafanyika kwa wingi tuu.

Nb: Ujerumani tu diploma yake kwa huku kwetu nahs ndo kama mtu mwenye PhD
 
Kula tisa
 
Upper second ya kukariri??
Wewe unayo upper ipi ya kuelewa mkuu. Nimechomekea na elimu ya wabunge ama viongozi wetu jamani mbali na elimu darasa ya watt wetu.

Vipi wewe mwenye kuelewa wa upper highest second umelifanyia Nini Taifa lako.

Ambao hata wamekariri wanatibu watu wanajenga nyumba unazotumia kila siku. Ni wahasibu na ma hr wapo wanafanya kazi mbalimbali nje na ndani ya nchi.
 
Advance (form 5 na 6) zifutwe, ni mambo ya kale
Binafsi nikijiassses najilaumu kwanini nilienda advance, sio kwamba ngumu ni nyepesi sana, ila nikiwaza nilivyokuwa nakomaa na ma organic chemistry, unaambiwa sijui uprove existance ya OH , sijui benzene. Tunaishia kukariri TU kwasababu hauwezi hakuna practical ya hayo mambo. Bora ningeenda diploma Sasa hivi ningekuwa hata mtaalamu mzuri wa magari. Kama upo chuo na una lengo la kujiajiri kwa unachikisomea unaweza ukaelewa
 
Mambo makubwa 2 naona yafanyike.
1. Shule zote kuanzia msingi mpaka sekondari form six pamoja na masomo ya kawaida pia wasome masomo ya lazima kama somo la biashara, kilimo(agribusiness), machenics, uchumi na sanaa mfano uchoraji, upishi, ususi n.k

2. Masomo yote 75% yawe practical na hiyo 25% theory. Mtoto ajengewe self competency ya fani sio taka taka za hivi sasa.


Japo vichwa vya viongozi wetu vimejaa michongo ya posho na trip allowance tuombe Mungu itokee mabadiriko ya mfumo wa elimu maana ni aibu tupu.
 
Nakuunga mkono hasa point ya 1 &2, just imagine tupo chuo first year bachelor, mwanafunzi wa engineering nafundishwa communication skills, halaf content yenyewe nakumbuka nilifundishwa darasa la 7 sijui la 6 Ile!. Kama issue ni kingereza lugha ya kimataifa au ya biashara, kwanini tusisome English course kabisa huku masomo mengine tunasoma Kwa lugha yetu( kiswahil)
 
Yes mda wa kufanya field week 10 hazitoshi, waweke mwaka kabisa au hata nusu mwaka
 
toa na kimbizaaa CCM madarakani, mambo mengine yatakaa sawaa tuu
 
China na Singapore wao utaratibu wao upo vipi?

Unaweza toa maoni yako hapa kidogo
 
China na Singapore wao utaratibu wao upo vipi?

Unaweza toa maoni yako hapa kidogo
Practical based education in relevance to natural environment and by improving production of raw materials for industries to manufacture goods for consumption!!ETI leo tuna upungufu wa mafuta ya kula hadi bei inapanda tu wakati tuna alizeti,michikichi,karanga,pamba nazi na n.k halafu watoto wanakariri atomic mass hadi chuo kikuu badala ya kuzalisha na kukuza uchumi!!!Pumba TUPU Mkuu!!!Tunaua viwanda VYA ndani kea kufundisha ujinga watoto wetu!!bado nyama na maziwa ku process Ili tuuze hadi nje!hata viwanda VYA nyama hatuna humu NCHINI!!!?TURUDI KWENYE MISINGI YA UZALISHAJI MKUU!!!cha kushangaza hatuna scheme za kutosha za umwagiliaji hapa NCHINI ETI tuna kilimo cha msimu mmoja tu !!hatuwezi production KWA style hiyo!!
 
Mkuu kuliondoa SoMo la Historia nisawa na kuruhusi Giza Nene kwenye fikra za watanzania asiyejua atokako hawezi kujua aendako.
 
Kwa mtazamo huu labda walimu watoke nje ya nchi kama ilivyo ktk soka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…