Tujadili tamko hili la Waziri wa Mifugo kuhusu usajili wa wafuga kuku

Tujadili tamko hili la Waziri wa Mifugo kuhusu usajili wa wafuga kuku

Ifike mahali viongozi wawe wabunifu na kuja na namna ya kufanya kitu kwa kushirikisha na kuelimisha wananchi na sio kuja na tamko la vitisho ili uonekane upo. Huo sio utendaji bora wa kazi. Tunahitaji kiongozi mbunifu na mwenye kuelimisha na sio kukurupuka na kutishia watu wakati hata huo utaratibu wa kusajili wafugaji haujulikani. Amekaa na sera zake huko za mwaka 47 ambazo hata hazijawa communicated kwa wananchi anaanza kutishia...
Yafaa hata waone aibu kilimo na ufugaji kwao muda wote havijawahi kuwa na maana, hata wameshindwa kuajiri hao maafisa ugani watoe japo ushauri kwa hao wanaofuga kwa mazoea ili wafanye hivyo kwa tija, baada ya kuona mkwamo wanakuja kwa vitisho, hebu wajitafakari na wafanye lililo sahihi. Ila hapa yote ya yote ni chanzo kipya cha kodi kinaangaziwa ila kwa utaratibu wenye mapungufu mengi.
 
Duuuh ila tutafika ila kuku wanyama kila baada ya miezi miwili au mitatu wanatakiwa kuuzwa kwa hiyo kila nikinunua wapya najisajili tena au inakuwaje?
 
Duuuh ila tutafika ila kuku wanyama kila baada ya miezi miwili au mitatu wanatakiwa kuuzwa kwa hiyo kila nikinunua wapya najisajili tena au inakuwaje?
Ushari wangu ,kabla hatujaenda mbali mamlaka husika ,watupatie takwimu ya mchango wao,hapa wanapofikiria kuvuna. Je waliwekeza kwa kiwango gani au ni mpango wa kutaka kuvuna wasicho panda?
 
Kwenye hili la kuku wafikirie mara mbili.
Mimi sio mfuga kuku lakini hili sio sawa.

Wengi wanaofanya biashara ya kuku ni watu wa viwango vya chini yaani masikini sasa ukiwawekea kodi lazima biashara zife.

Hiyo itapelekea umasikini kuongezeka mara dufu unategemea wataishije?

Hiyo ni taarifa mbaya kwa masikini hivi serikali inafikiria jinsi watu wanavyoishi huko mitaani Tanzania?
Au huko bungeni kwenye airC wanadhani wananchi wote wanaishi kama wao hivyo mnaweka sheria tu bila kufikiria negative impact kwa wananchi wa viwango vya chini?

This isn't fair at all.

Serikali ipo kwa ajili ya wananchi na sio wananchi wapo kwa ajili ya serikali.
Hivyo ni wajibu wake serikali kusikiliza wananchi.
 
Sijajua kwanini ni kuku tuu Aaaargggh hivi umenielewa kaka ? Wewe unavyoona wanaanzia wangapi ?

Hivi Unaweza fuga broiler 5 ukasema unafanya biashara ya kuku wa nyama ?
Wale obviously wanakuwaga wengi
Wingi ukumbuke unaanzia 2, sasa ili mtu asajiliwe hao wengi wanaanzia wangapi kama unafahamu
 
Mimi Nadhani kikubwa hapo kinachotafutwa sio database wala taarifa za kuku nchini

Ni Serikali inaangalia ni kwa Namna gani itapata chochote kitu. Unajua VAT inakatwa kwa Registered companies yoyote inayo zalisha bidhaa Au kutoa huduma frani Mf bidhaa za Bakhresa Au huduma za Vodacom

Hivyo basi kuwasajiri wafanyabiashara wa kuku wa nyama na mayai ni kuifanya Serikali kupata mapato (VAT 18%) kwenye kila kuku Au Yai moja

Mfano Sasa hivi kuku wa broiler ni 6000 mpaka 6500, endapo hili zoezi lao la usajiri litaenda sawa hawa kuku tutegemee kuuzwa 7500 na zaidi, the same kwnye mayai

Binafsi sioni shida katika hilo kabisa
Yani Serikali ipate KODI za kutosha Mimi nichukie Wallah ntakua mwenda wa zimu

Japo hili swala wamelileta kishkaji, Haliko wazi sana than it should be Au pengine no tatizo la muandishi wa hio habari gazetini [emoji2363]
Nakubaliana na issue ya kuongeza wigo wa kodi lakini Ujinga uliopo katika hili nikuwa kodi zinakwenda kuongezwa kwenye watu wale wale kama hilo ongezeko litakwenda kwa mlaji. Kupanua huo wigo ilikuwa kuwapata wale wasiolipa kodi wa lipe nakodi iwe kwa muuza kuku sio mlaji. Sasa kila kodi mpya mzigo ni kwa mlaji wa mwisho. Hiyo ya kuku itakwenda kuongeza bei ya kuku moja kwa moja.
 
Je, utaratibu ukoje?

Je, wafugaji wa wanyama wengine vipi?

Kusajili ni vizuri ila uwekwe utaratibu kwa mifugo yote wafugaji wasajiliwe kuwe na database na sio wafuga kuku wa nyama na mayai. Kuna mifugo mingi nchiniView attachment 1663632
Content na caption si sawa, kwenye content Waziri haonekani
 
Sijui tunaelekea wapi...
Watu wameshindwa kubuni vyanzo vya mapato
 
Nikaamua nianze kufuga kuku ili kuji kwamua kimaisha sasa mwee na huko nako wamebana.
 
Je, utaratibu ukoje?

Je, wafugaji wa wanyama wengine vipi?

Kusajili ni vizuri ila uwekwe utaratibu kwa mifugo yote wafugaji wasajiliwe kuwe na database na sio wafuga kuku wa nyama na mayai. Kuna mifugo mingi nchiniView attachment 1663632
Hili nalo litapita kama lile tamko la Hakuna kuolewa au Kuoa bila kuwa na cheti cha Form Four
 
Na kwa nini kuku tu na sio mifugo mingine? Vipi ng'ombe, bata, mbuzi, kitimoto, inabidi ifanyike kwa mifugo yote na pia kwa kuwa ni suala linalogusa jamii yote basi watoe elimu na utaratibu
Wanaenda hatua kwa hatua
Sasa hivi wanaanza na wafuga kuku badae inafuata wafugaji wa njiwa, bata, kanga, njiwa poli, ndege aina mbalimbali, paka na mbwa.
 
Nawaza kuku wangu wakiangua huyoo speed kwenda kusajili.. Hiv hawa viongozi wetu wanaishi Tanzania!!
 
Back
Top Bottom