Tujadili: Wapi wana amani ama wanafurahia maisha kati ya wanandoa na walio nje ya ndoa?

Tujadili: Wapi wana amani ama wanafurahia maisha kati ya wanandoa na walio nje ya ndoa?

Ndikwega

R I P
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,979
Reaction score
5,529
Habarini WanaJukwaa Pendwa la MMU!

Katika Pita pita yangu nimekutana na Msuguano Mkali wa Juu ya Raha ya Kuwa na Ndoa ama Kutokuwa kwenye Ndoa.
Kuna Wengine Wamesema Ndoa ina Raha saana maana Ndiyo Utimilifu wa Maisha wenyewe. Wamedai kuwa Ukiwa Nje ya Ndoa maanake kunakuwa kama Kiungo Kimekosekana.

Aidha kwa Upande Mwingine hawa Wanaokataa Mambo ya Ndoa wanaona Kuwa ni Shida maana Mwanandoa Unakosa Uhuru, Unaishi Kwa Sheria unakosa maamzi yatakayo iburudisha Nafsi yako. Yaani Kiufupi unakuwa kwenye Kifungo, Kuwa umefungwa na Upande wa Pili wa mwenza wako.

Bila kuegemea Mambo ya Dini ama Imani, Naomba tupate hata wewe Mjango wako. Karibu kwenye Uwanja wa mawazo huru.

Ahsanteni!
 
Simple, walio nje ndio wana furaha zaidi. Mahusiano yanamchango mkubwa sana wa kuondoa furaha kuliko ambavyo yana mchango katika kuileta.

Sema tu kuna wakati mwingine tunaingia katika ndoa na mahusiano kwa ujumla si tu kwa sababu ya furaha pekee, kuna mambo kama hadhi, watoto, kusaidizana majukumu n.k
 
Mkuu kwa upande wangu naona ndoa ni furaha sana. Mke wangu nimempa uhuru sana na mimi amenipa uhuru sana kwakua tumepeana neno uaminifu japo uwezi jua kilichopo moyoni.

Pesa tunasaka wote mmoja akikosa mwengine anamgawia ; mmoja akikosa muda mwingine anamsaidia..mmoja akichoka kukaa ndani mwengine anasindikiza out; mmoja akiumwa mwengine anamuuguza; mmoja akikadirishwa kazini mwengine anampa faraja ;mmoja akiwa na amu mwengine anamtolea amu. na Mengine mengi
Furaha ninayopata ndani ya ndoa kubwa sana sikuyapata nikiwa bachelor.
 
Kwa mtazamo wangu kuwa kwenye ndoa ni bora zaidi kuliko kuwa nje ya ndoa, kwasabau ndoa humfanya mtu kujituma na kuboresha maisha yake na yawale wamtegemeao (mke,mume,watoto,wazazi,ndugu). Na pia ndoa huwatengeneza watu kuwa na tabia njema na kufanya mambo kiutuuzima na kibusara zaidi pamoja na kumfanya mtu ajitengenezee heshima na kuheshimika.
Ndio maana utaweza kuona mtu huonekana mhuni pale anapokuwa na watoto pasi na kuwa kwenye ndoa.
 
Usiishi kwa kuangalia watu..jiangalie mwenyewe. Dunia ina watu zaidi ya bil 10. Diversity ya kutosha...kila watu wana tabia zao wenyewe na style zao za maisha. Kuna wanaume ni walevi...sasa ukienda kuomba ushauri kwa mke wa mwanaume mlevi kupindukia ambaye hajali familia atakupa yake kutokana na nexperience yake.
 
Katika kipindi ambacho nmeweza kuwa huru...mwenye amani na furaha ni kipindi hiki nilicho single

Kuna mengi nmeweza kuyatimiza mwaka huu 2019 just naamin kwakuwa niko single

Japo kiukweli kuna mda hua najihic upweke...!!kuna mda hua nataman kuwa na mtu...lkn kwa wnawake niwaonao wa sasa hua naamua kupotezea..!!

Naamini ipo cku...wakat ukifika atapatikana nmtakaye...!!

Ila just uciingie kwenye ndoa kwakuwa uko mpweke...maisha ya ndoa ni bonge la NECTA...!!jipamge kimaisha kabla hujaingia...jipange kiakili kabla hujampa mtu maisha yako

Coz nna anko zangu kam wa3 ambao kwakweli walijijenga vema mno kipindi wapo single....ila waliporomoka ndan ya wiki 1 walipoingia kwenye mahusiano
 
Usiishi kwa kuangalia watu..jiangalie mwenyewe. Dunia ina watu zaidi ya bil 10. Diversity ya kutosha...kila watu wana tabia zao wenyewe na style zao za maisha. Kuna wanaume ni walevi...sasa ukienda kuomba ushauri kwa mke wa mwanaume mlevi kupindukia ambaye hajali familia atakupa yake kutokana na nexperience yake.
Bado sijakuelewa Umelenga nini haswa kwa kuoanisha na hii Mada Mkuu.
Hata hivyo Ahsante kwa Kushiriki.
 
Ndikwega, We huna akili hkn maisha bila ya dini acha ukafir wako! Kwahy unataka uwaambie watu kuzin ni bora kuliko kuoa!
 
Mkuu@BradFord93,
Mkuu unamaanisha ulizaoa alafu ukaachana ? au sijakuelewa. Umeelezea kama umeshapitia nyanja zote. Lakini kuna kuoa na kuishi na Mwanamke bila kualalisha taratibu zote.
 
Ndikwega walio nje ya ndoa wana raha kwani ukiwa nje ya ndoa haina maana huna partner kwa hivyo utapata vyote tena zaidi ya aliye ndani ya ndoa
Wengi wanaingia kwenye kufurahisha jamii bila kuelewa ni ushirika kama Chama cha ushirika
You Give n Take sio You Take tuuuu

Ndoa ni kujifunga kitanzi fulani hivi sio wote lakini wengi wanajutia ndoa zao
 
We huna akili hkn maisha bila ya dini acha ukafir wako! Kwahy unataka uwaambie watu kuzin ni bora kuliko kuoa!
Kwahiyo Wewe ndiyo Una akili kwa Kunidhihaki mimi au siyo? Ahsante kwa Kushiriki!
 
Mkuu kwa upande wangu naona ndoa ni furaha sana. Mke wangu nimempa uhuru sana na mimi amenipa uhuru sana kwakua tumepeana neno uaminifu japo uwezi jua kilichopo moyoni.

Pesa tunasaka wote mmoja akikosa mwengine anamgawia ; mmoja akikosa muda mwingine anamsaidia..mmoja akichoka kukaa ndani mwengine anasindikiza out; mmoja akiumwa mwengine anamuuguza; mmoja akikadirishwa kazini mwengine anampa faraja ;mmoja akiwa na amu mwengine anamtolea amu. na Mengine mengi
Furaha ninayopata ndani ya ndoa kubwa sana sikuyapata nikiwa bachelor.
Asante umesema yote siongezi neno
 
Ndikwega walio nje ya ndoa wana raha kwani ukiwa nje ya ndoa haina maana huna partner kwa hivyo utapata vyote tena zaidi ya aliye ndani ya ndoa
Wengi wanaingia kwenye kufurahisha jamii bila kuelewa ni ushirika kama Chama cha ushirika
You Give n Take sio You Take tuuuu

Ndoa ni kujifunga kitanzi fulani hivi sio wote lakini wengi wanajutia ndoa zao
Mmh, haya Mambo ni Magumu. Ngoja tukusanye Michango ya wengine Mkuu!
 
Ndikwega walio nje ya ndoa wana raha kwani ukiwa nje ya ndoa haina maana huna partner kwa hivyo utapata vyote tena zaidi ya aliye ndani ya ndoa
Wengi wanaingia kwenye kufurahisha jamii bila kuelewa ni ushirika kama Chama cha ushirika
You Give n Take sio You Take tuuuu

Ndoa ni kujifunga kitanzi fulani hivi sio wote lakini wengi wanajutia ndoa zao
Bado hujui unachokisemea ingia uone
 
Back
Top Bottom