Tujadili: Wapi wana amani ama wanafurahia maisha kati ya wanandoa na walio nje ya ndoa?

Walio nje ya ndoa wana furaha zaidi. Si tu ndani ya ndoa hawana furaha,hata kuwa kwenye mahusiano permanent kunakunyima furaha,ksbb kuna mambo uyapendayo unaweza ukazuiliwa kuyafanya. Nakushauri kama hujaingia kwenye ndoa achana nayo kabisa hilo jjnamizi (Najua upande wa kuachana nalo hapa watu watakuja speed na mawe). Lakini huo ndio ukweli. Dunia inaendelea mbele,kwa hiyo wanaopingana nami ktk hili wataelewa miaka kadhaa mbele MUNGU akiwajalia uzima
 
Mkuu Inakuaje mtu unajutia? Si ni bora kubwaga manyanga kuliko kuchomana mkaa
 
Ndoa

1. Chama (mume/mke). Umoja ni nguvu

2. Msaada ( majanga, kuugua, nk)

3. Ushauri

4. Uwekezaji
- watoto
- vitegauchumi

5. Heshima ( kuwa na mke/mume)

Nk

Changamoto hazikosekani ndio maisha

Single
1. Ukiuguwa ......

2. Ukipata mkasa .....

3. Heshima...... nimhuni siku zote

4. Watoto kulelewa na mzazi mmoja ....?!

5. Huna hofu wala mshauri wa ndani.... unajiamlia tu utakavyo Siku zinasonga...... fainali uzeeni.

Faida kubwa kuwa single
1. Upo huru kufanya chochote ikiwemo Kulala popote bila kuulizwa.
 
Una hoja Mkuu. Kuna muda haya mambo kama yote yako sawa ama hayako sawa.
 
Ndoa ni nzuri kama tu ulihiari mwenyewe kuingia kwenye ndoa na upo na mtu sahihi kwako. Na ni chungu km uliingia kwa kulazimishwa au kutaka sifa.
Ukiingia kwenye ndoa inabidi uachane na ubinafsi ili muishi vyema na mwenzi wako, la sivyo watu wanaona ndoa ni chungu kwa sababu wanataka wafanye mambo ambayo ni kinyume na viapo vya ndoa zao.
Furaha ni dhana ngumu kuielewa, kwa upande wangu naona ukiwa kwenye ndoa ya hiari ni bora kuliko kuwa katika maisha ya useja.
 
Kwangu ndoa ina umuhimu kwanza uzao wangu kwa baba mmoja naona kuzaa kila mtoto na mwanaume tofauti kwa upande wangu sio kitu kizuri.

Pili malezi kwa Hawa watoto unawalea pamoja na baba yao inapendeza zaidi.

Tatu swala la Mambo ya chumban unakuwa na mtu mmoja ambaye mnakutana kuliko Leo unakutana na huyu kesho na huyu, ukiwa single unakuwa nje ya sheria hakuna wa kukuwekea mipaka.

Changamoto kubwa ya ndoa Kuna kauhuru flani kanakosekana ukiwa single Kuna baadhi ya Mambo unayatatua mwenyewe bila kumshirikisha mtu kwenye ndoa hakutaki ubinafsi. Ukiwa mbinafsi au muhuni Kuna uwezekano mkubwa ndoa kwako haliwezi kuwa Jambo la heri.
 
Usifananishe kuwa nje ya ndoa na vitu vya kijinga. Acha kabisa!
 
Ulimwengu huu hakuna jambo ambalo utalikuta halina side B, Challenge na hii ni kwa sababu kuna Mungu na Kuna shetani pia, kwa kifupi maisha yetu yote yapo na Ups pia yapo na down ingawa kila jambo lina namna ya ku-mitigate ugumu wake. hata hivyo suala la mahusiano linaonekana kuwa la kuumiza zaidi hasa kwa sababu ni suala linalohusisha emotion na vitu kama hizo

kM ilivyo kwa wasio na ndoa, katika ndoa upo wakati wanandoa wanakuwa na furaha lakini pia kuna wakati kuna machungu. Namna pekee ya kuishi vema ni kujua kuwa hizi changamoto zipo katika mambo yote ya kimaisha na wa kukabiliana nazo ni wewe mwenyewe si mtu mwingine.
 
Upo sawa Mkuu, ndiyo maana tunarudi pale pale Binadamu hatuwazi sawa. Shida lililo zuri kwa upande mmoja pengine wa pili ni shida. Karibu saana kwenye mjadala.
 
Kujadili ndoa wakati hujawahi hata kuwa na mke huo tunaitaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…