Tujadiliane Kuhusu Hili Soko lenye paa mbili za bati, soko la Mbuyuni Lililojengwa Moshi Manispaa kwa Dhamani ya Bilioni 2!

Nyie si mliondoa madiwani wa upinzani na kuwanyang'anya manispaa kwa nguvu. Subirini iwaingie
 
Msidhani haya yanatokea kwa bahati mbaya? Kwa makusudi Samia anaachia watu waibe ili wawe tayari kumsaidia kuiba kura wakati wa uchaguzi. Yaani anataka viongozi wote wawe ndiyo watetezi wa kura zake kwa kuogopa mabadiliko yakitokea hawatakuwa tena na sehemu ya kuiba.
Nikweli kabisa
 
Kama Kuna uwezekano,hiyo BOQ ya hilo soko,ipelekwe TAKUKURU makao makuu
Kuna madudu ya ajabu!
Mkandarasi alitokea mwanga, na ana mahusiano makubwa na Mwajuma,tangu akiwa DED mwanga
 
Soko Lile lile la Mbuyuni,huko Moshi Manispaa, limepanda gharama kutoka 2 billions hadi 5.9 billions.

Tulishangaa gharama za awali ,sasa tunashangaa picha ya Samia yenye 5.9 billions.
Tuakukuru,Takukuru,Takukuru
 
Attachments

  • IMG-20250313-WA0006.jpg
    IMG-20250313-WA0006.jpg
    52.9 KB · Views: 1
  • IMG-20250313-WA0018.jpg
    IMG-20250313-WA0018.jpg
    92.4 KB · Views: 1
Kwa dhamani ya bilioni 2, wengi wanajiuliza ni wapi fedha hizo zimeelekezwa, hasa kwa kuzingatia hali ya soko lenyewe. Kila mmoja ana mtazamo wake, lakini kuna maswali mengi yanayohitaji majibu.
Piga kelele hata ufanyeje, maadam ni ccm "wamekula" hakuna tatizo.
CCM ni bora sasa mkaacha kuleana hadi ktk wizi!
 
Attachments

  • Snapinsta.app_483423170_1071770781641908_3545649834984004154_n_1080.jpg
    Snapinsta.app_483423170_1071770781641908_3545649834984004154_n_1080.jpg
    126.7 KB · Views: 1
Utangulizi
Soko la Mbuyuni, lililojengwa katika Manispaa ya Moshi, limekuwa kivutio cha mjadala mzito miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

Kwa dhamani ya bilioni 2, wengi wanajiuliza ni wapi fedha hizo zimeelekezwa, hasa kwa kuzingatia hali ya soko lenyewe. Kila mmoja ana mtazamo wake, lakini kuna maswali mengi yanayohitaji majibu.

Kwanza, ni muhimu kuchunguza muundo wa soko hili. Picha ya soko inaonesha paa la chuma, mabati, na sakafu ambayo haionekani kuwa na viwango vya juu vya ubora. Hii inashangaza kwa sababu fedha nyingi zilipaswa kuleta mabadiliko chanya katika muonekano na huduma za soko.

Je, ni kiasi gani cha fedha kilitumika katika ujenzi wa miundombinu hii, na je, fedha zilizotumika zinakidhi viwango vilivyokusudiwa?

Pili, kuna haja ya kuangazia mchakato wa ujenzi wa soko hili. Ni wazi kwamba kuna watu wengi waliohusika katika hatua hizi, lakini je, kulikuwa na uwazi katika utendaji wa kazi?

Takwimu za matumizi ya fedha na taarifa za wakandarasi wanahitajika ili kubaini kama kuna upotevu wa fedha au ufisadi. Serikali inapaswa kutoa taarifa ya wazi kuhusu mchakato mzima wa ujenzi na matumizi ya fedha hizi.

Pia, kuna wasiwasi kuhusu usimamizi wa soko hili. Je, kuna mfumo mzuri wa kusimamia shughuli za soko ili kuhakikisha kuwa wanunuzi na wauzaji wanapata huduma bora? Watu wanahitaji kujua ni vipi soko hili litakavyowafaidi kiuchumi. Mambo kama usalama, usafi, na huduma za msingi zinapaswa kuwa kipaumbele.

Wakati huu, ni muhimu pia kuangalia jukumu la taasisi za serikali kama Takukuru. Kila mmoja anatarajia kuwa watachukua hatua za haraka katika kutafuta ukweli kuhusu matumizi ya fedha hizi.

Hali hii inahitaji uchunguzi wa kina ili kubaini kama kuna wizi au ufisadi uliofanyika. Kutokuwepo kwa hatua zozote hadi sasa kunaweza kuashiria kuwa kuna matatizo makubwa katika usimamizi wa fedha za umma.

Kwa upande mwingine, ni muhimu kwa jamii kujihusisha na masuala haya. Wananchi wanapaswa kutoa maoni yao na kushiriki katika mijadala kama hii ili kuweza kushawishi mabadiliko.

Ni lazima wawe na sauti katika masuala yanayohusiana na maendeleo yao na matumizi ya rasilimali za umma.

Katika hitimisho, soko la Mbuyuni linaweza kuwa fursa kubwa kwa jamii ya Moshi, lakini lazima kuwe na uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha. Ni jukumu letu sote, wananchi na viongozi, kuhakikisha kuwa soko hili linakuwa kielelezo cha maendeleo na si kashfa ya ufisadi. Wakati umefika kwa kila mmoja wetu kuchukua hatua na kutaka majibu.
Dhamani ndiyo nini ewe punguani!?
 
Soko Lile lile la Mbuyuni,huko Moshi Manispaa, limepanda gharama kutoka 2 billions hadi 5.9 billions.

Tulishangaa gharama za awali ,sasa tunashangaa picha ya Samia yenye 5.9 billions.
Tuakukuru,Takukuru,Takukuru
Sasa hizo lawama ni za nani; mkuu wa DED, Mkuu wilaya, DAS, Mkuu wa Mkoa, mkurugenzi TAMISEMI au waziri husika Mchengerwa.

Mpaka ujaeleweka shida ni nini; na lawama unampa nani.
 
Dhamani ndiyo nini ewe punguani!?
Wanashida hao, awamuwezi ‘Priscus Tarimo’ na wana hasira nae kwa sababu alikuwa upande wa ‘bi-tozo’ kutetea uwekezaji wenye tija bandarini wa DPW.

Wapambane na hali zao, sasa walitaka mmbunge apingane na serikali. Wanachukia wakiona Priscus anaunga mkono hoja za Samia; ndio msingi wa chuki zao kwake.
 
Huyu ndio alisema JPM ni mzima na anapiga kazi wakati Yuko alikua anapigania uhai wake
siwezi maisha kumuamini huyu.
 
Utangulizi
Soko la Mbuyuni, lililojengwa katika Manispaa ya Moshi, limekuwa kivutio cha mjadala mzito miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

Kwa dhamani ya bilioni 2, wengi wanajiuliza ni wapi fedha hizo zimeelekezwa, hasa kwa kuzingatia hali ya soko lenyewe. Kila mmoja ana mtazamo wake, lakini kuna maswali mengi yanayohitaji majibu.

Kwanza, ni muhimu kuchunguza muundo wa soko hili. Picha ya soko inaonesha paa la chuma, mabati, na sakafu ambayo haionekani kuwa na viwango vya juu vya ubora. Hii inashangaza kwa sababu fedha nyingi zilipaswa kuleta mabadiliko chanya katika muonekano na huduma za soko.

Je, ni kiasi gani cha fedha kilitumika katika ujenzi wa miundombinu hii, na je, fedha zilizotumika zinakidhi viwango vilivyokusudiwa?

Pili, kuna haja ya kuangazia mchakato wa ujenzi wa soko hili. Ni wazi kwamba kuna watu wengi waliohusika katika hatua hizi, lakini je, kulikuwa na uwazi katika utendaji wa kazi?

Takwimu za matumizi ya fedha na taarifa za wakandarasi wanahitajika ili kubaini kama kuna upotevu wa fedha au ufisadi. Serikali inapaswa kutoa taarifa ya wazi kuhusu mchakato mzima wa ujenzi na matumizi ya fedha hizi.

Pia, kuna wasiwasi kuhusu usimamizi wa soko hili. Je, kuna mfumo mzuri wa kusimamia shughuli za soko ili kuhakikisha kuwa wanunuzi na wauzaji wanapata huduma bora? Watu wanahitaji kujua ni vipi soko hili litakavyowafaidi kiuchumi. Mambo kama usalama, usafi, na huduma za msingi zinapaswa kuwa kipaumbele.

Wakati huu, ni muhimu pia kuangalia jukumu la taasisi za serikali kama Takukuru. Kila mmoja anatarajia kuwa watachukua hatua za haraka katika kutafuta ukweli kuhusu matumizi ya fedha hizi.

Hali hii inahitaji uchunguzi wa kina ili kubaini kama kuna wizi au ufisadi uliofanyika. Kutokuwepo kwa hatua zozote hadi sasa kunaweza kuashiria kuwa kuna matatizo makubwa katika usimamizi wa fedha za umma.

Kwa upande mwingine, ni muhimu kwa jamii kujihusisha na masuala haya. Wananchi wanapaswa kutoa maoni yao na kushiriki katika mijadala kama hii ili kuweza kushawishi mabadiliko.

Ni lazima wawe na sauti katika masuala yanayohusiana na maendeleo yao na matumizi ya rasilimali za umma.

Katika hitimisho, soko la Mbuyuni linaweza kuwa fursa kubwa kwa jamii ya Moshi, lakini lazima kuwe na uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha. Ni jukumu letu sote, wananchi na viongozi, kuhakikisha kuwa soko hili linakuwa kielelezo cha maendeleo na si kashfa ya ufisadi. Wakati umefika kwa kila mmoja wetu kuchukua hatua na kutaka majibu.
ccm imetamalaki
 
Kwanini wachaga hamuwezi kuzema THAMANI, mnasema DHAMANI, how comes ?... Turud kwenye mada hapo tumepigwa
 
Hili soko,hata choo,hakukujengwa,bali wananchi wanatumia choo Cha zamani.
2. Hakuna eneo lililotengwa kwa ajili ya walemavu kufanyia biashara
3. Hakuna vipaza sauti vya kutoa matangazo sokoni
4. Hakuna vifaa vya kuzimia moto,na awali soko hilo liliungua
5. Hakuna eneo lililotengwa la parking za magari,boda Wala bajaji.
 
Tangu CCM washinde ubunge wa Manispaa ya Moshi 2020, mji umekuwa mchafu sana na wizi umerudi kwa kasi ya kutisha. Ni mambo ya aibu sana yanafanyika manispaa ya Moshi
 
Back
Top Bottom