Mimi nilikua na wazo masoko makubwa yawe matatu maeneo tofauti labda chanika lijengwe soko kubwa la vifaa vya ujenzi na huko kuwe pia na vifaa vyote vya umeme, vitu kama simu, halafu lijengwe soko lingine mbezi kubwa hapo sasa ndio wawekwe wauzaji wa nguo zote, viatu vyote yaani mavazi kwa ujumla kuwe huko halafu soko la kariakoo labda libakie la kuuza spareparts za magari, pikipiki, bajaji na huko ndio ziuzwe pikipiki, bajaji, toyo za mizigo na kubakie bidhaa nyingine kama vipodozi na zile bidhaa za majumbani yaani pipi, jojo, sabuni za kufulia na kuogea, vyombo vya ndani vibakie huko halafu ujenzi huo uende sambamba na upanuzi mahususi wa barabara yaani anzia mbezi, ubungo, bunguruni Gongo la mboto, chanika barabara ziwe njia nane yaani zinazoingia na kutoka ziwe njia nane na ziambatane na madaraja ya watembea kwa miguu hapo unakua umebalance jiji na hutoona msongamano kama wa sasa kariakoo