Tujenge Kariakoo nyingine maeneo muhimu

Hatuna viongozi wenye akili hizo ndugu.
ndio maana mimi nimejitolea kuwapa ushauri wa bure kabisa.
RC wa Mkoa wa Dar, waziri wa TAMISEMI wanaweza kuchukua mawazo hayo au wanaweza kuacha.
Ushauri nilio utoa utatatua changamoto ya miaka zaidi ya 20 ijayo endapo tu Soko kubwa la Kisasa lita Jengwa Maeneo ya Mbezi Mwisho ambalo limekuwa eneo
 
Eneo la Mbezi mwisho ni strategic area kwa sababu kubwa moja
1. kituo cha Mabasi yaendayo mikoa yote pamoja na nchi Jirani watu wato wanashukia hapo.
 
Wazo zuri
 
kujenga Soko K.Koo maeneo ya Kituo Cha Mabasi cha Magufuli ni suluhisho kwa changamoto kwa machanga kwa miaka 30 ijayo.
kwa nini tunasema lijengwe maeneo hayo?
hakuna ubishi kuwa kwa sasa eneo la Mbezi Mwisho na viunga vyake ndilo eneo pekee linalo kusanya umati wa watu kila siku, hivyo ni eneo la kimkakati endapo tu watendaji wetu watakuwa na maarifa ya kuona mbali zaidi.
pili ktk maeneo hayo bado kuna fursa ya space ukilinganisha na sehemu zingine.
kazi kwenu watendaji wa Jiji la Dsm na TAMISEMI
 
unaongelea upande mmoja tu, unajua umati unaokusanyika Mbagala kila siku na magari ya kusini yanavyomwaga watu??
 
Unataka kila kitu kipelekwe kwenu Mbezi waje Gongo la Mboto au Temeke bado kuna maeneo
 
Umeandika vizuri mkuu!!
 
Tuwe wabunifu, tuache kusababisha msongamano katikati ya Jiji, ni muhimu sasa tuanze kuwekeza pembezoni ili kutanua Jiji na kupunguza msongamano usio wa lazima.
Tuwe wabunifu na pia tuweke mipango ya miaka 50 ijayo tusiangalie mipango ya mika 10.
 
Wazi zuri ila viongozi wetu sijui walisema wapi? Ubuntu ZERO wengi wao
 
Hata halmashauri ya Ubongo ambao stand ipo kwao wanaweza tenga eneo hapo karibu wakajenga soko kubwa la kimataifa. Watu wakitoka mikoani au nje ya nchi wanafika hapo, wananunua bidhaa na kusepa zao.

Mbona Mawasiliano ndani wamejenga hiko kitu.
 
Nani kakwambia kariakoo imejaa

Saa hizi ghorofa zinatobolewa ni mwendo wa Underground za kutosha


Kuijengea kariakoo mpya ni zoezi la miaka 30 kuendelea

Mipango ya nchi ipo hivyo?
 
Mfano tegeta ilitakiwa iwepo
Kko ya kimtindo
Kimara mwisho ilitakiwa iwepo
Kko ya kimtindo
Na mbagala

Ova

Kimara mwisho hata soko la nyanya hamna

Pale barabarani wametangaziwa kuondoka

Eneo la wazi mtu amehodhi amefanya parking[emoji706][emoji706]
 
Waachie wataalamu wa mipango miji naona ushauri wako haufai. Kaa pembeni au rudi kajifunze kuusu miji, mipango miji na ukuaji wa miji
 
Uwepo wa soko eneo la kariakoo kumechagizwa kulingana na jiografia ya eneo husika,maana Ni jirani na bandari,jirani na ofisi na taasisi mbali mbali,lakini pia ilikuwa jirani na stendi kuu ya mabasi ya zamani(kisutu),jirani na hospital kuu ya taifa, jirani na stesheni ya treni

Ukiona mpangilio wa vitu vyoye hv utagundua vilikuwa vinachagiza uhitaji wa soko mahala pale kuliamisha soko inawezekana ila italeta athari kubwa kiuchumi kwa namna moja au nyingine.

Kwa ninavyoona nadhani jopo la wataalamu wa land development, civil & building engineer bila kuwasahau wataalamu wa land management wangekaa pamoja na kubuni mchoro mpya wa kuweza kuwajumuisha wafanyabiashara wengi na kupunguza msongamano...

Mf kuanzia makutano ya taa za msimbazi na mnazi mmoja ushuke Hadi mnazi mmoja,then barabara ya inayopita makao ya ccm,mpk Morogoro road,ukunje mpk faya,ukifika kwenye mataa urudi kuelekea msimbazi Tena...
Hilo eneo lingekuwa mall yenye amajengo makubwa ndani yake kuwe na maduka soko, migahawa , warehouse ,jengo la parking kubwa kwenda juu...

Hii ingesaidia kuchukua watu wengi kwenye mpangilio maalum na kwa eneo dogo sema limekwenda juu

Lakini ingekuwa rahisi kwenye usimamizi na ukusanyaji wa mapato
Pia ingekuwa rahisi kwa wageni kupata mahitaji kwa Urahisi bila kupotea
Lakini itapunguza mizunguko miingi maana utaweza kwenda moja kwa moja kwenye duka la bidhaa husika
Kwakuwa majengo yamejengwa kimpangilio wa kisasa ingerahisisha uchukuzi na upakiaji wa mizigo inayoingia na kutoka kwa muda mfupi bila kubugudhi shughuli zingine

Itapunguza majanga au athari Zinazotokana na majanga yenyewe km Moto uliotokea hv karibuni..

Nimalizie tu kusema soko la kariakoo Ni mashuhuri mno,wafanyabiashara kutoka Malawi, Zambia,msumbiji,comoro, wanakuja kufunga mzigo hapo Ni wakati wa serikali kuona vipaumbele na kuviboresha
 
Sawa ni Jambo zuri na Jema kwa hatua ya Serikali kuamua kujenga Kituo cha Kibashara ktk maeneo ya Ubungo kilipojuwa kituo cha Mabasi ya Mikoani lkn kwa mtizamo wangu bado naona sehemu hiyo haikustahili kujengwa kituo cha kibiashara, kwa sababu zilezile tunazo zizungumzia mara zote nayo ni Msongamano.
watendaji wetu wanapaswa kufikiria mambo miaka 50 ijayo sio miaka 5 au 10!! tunachezea fedha bureee!!!
Jengeni vitu kama hivyo ktk maeneo makubwa na ya kimkakati kama nilivyo sema hapo juu, miradi hii inapaswa iishi zaidi ya miaka 50 bila kero wala usumbufu.
Tuwe na mikakati ya kulitanua Jiji sio kulibananisha.
tujifunze hata kwa majirani zetu, sio kusongamanisha kila kitu katikati ya Jiji.
tutumie maeneo ya pembezoni.
bado narudia tena Mbezi mwisho na viunga vyake ni "strategic area" kwa sababu ndio lango kuu lkn pili Magufuli bus terminal, vyote hivyo vinafanya eneo hilo kuwa la kimkakati kwa uchumi wa DSM na nchi kwa ujumla.
 
wazo zuri sana
 
Sawa ni Jambo zuri na Jema kwa hatua ya Serikali kuamua kujenga Kituo cha Kibashara ktk maeneo ya Ubungo kilipojuwa kituo cha Mabasi ya Mikoani lkn kwa mtizamo wangu bado naona sehemu hiyo haikustahili kujengwa kituo cha kibiashara, kwa sababu zilezile tunazo zizungumzia mara zote nayo ni Msongamano.
watendaji wetu wanapaswa kufikiria mambo miaka 50 ijayo sio miaka 5 au 10!! tunachezea fedha bureee!!!
Jengeni vitu kama hivyo ktk maeneo makubwa na ya kimkakati kama nilivyo sema hapo juu, miradi hii inapaswa iishi zaidi ya miaka 50 bila kero wala usumbufu.
Tuwe na mikakati ya kulitanua Jiji sio kulibananisha.
tujifunze hata kwa majirani zetu, sio kusongamanisha kila kitu katikati ya Jiji.
tutumie maeneo ya pembezoni.
bado narudia tena Mbezi mwisho na viunga vyake ni "strategic area" kwa sababu ndio lango kuu lkn pili Magufuli bus terminal, vyote hivyo vinafanya eneo hilo kuwa la kimkakati kwa uchumi wa DSM na nchi kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…