Tujenge utaratibu wa kuhifadhi maji ya mvua

Tujenge utaratibu wa kuhifadhi maji ya mvua

Ni njia nzuri ya jutunza mazingira pia, ametengeneza tanki la ukubwa gani? Kwakweli maji ya mvua ni mengi tu tukiweza kuyahifadhi hata kwa garden yanafaa.
Kisima kinahifadhi gallon 30,000 na simtanks mbili za lita 20,000 . Alivyojenga simtank zikijaa maji yanakwenda kisimani. Akiyahitaji anavuta kwa pump kwenda kwenye simtank
 
Kwani haya maji mengine kwenye mabwawa na visima hayatokani na maji ya mvua? maana kwa komenti za humu inaonekana maji ya mvua ni kitu tofauti sana
 
Imeeleweka mkuu, ifikie kipindi watu tuweze kujiongeza ,inapiga mvua msimu mzima then kiangazi watu wanalia shida ya maji.
 
Umesoma kuhusu Hydrological cycle na Underground water?
Ungesoma usingeuliza ulichoandika!
Kwani haya maji mengine kwenye mabwawa na visima hayatokani na maji ya mvua? maana kwa komenti za humu inaonekana maji ya mvua ni kitu tofauti sana
 
Sky umenigusa kuna msemo wa biblia watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Waisraeli kwao ni nusu jangwa lakini wameendelea kwa kilimo
Maji ya mvua muhimu sana aise nakuinbox
 
Pia idara ya Maji wanatiba mbalimbali za Maji kutokana na Maji husika siyo mbaya kuwaona

Nilifanikiwa kuwatembelea siku ya Nanenane wanaelekeza vizuri sana na Dawa zoa mbalimbali
Pia ni vema ukiwaona wakakupimia na Maji unayotumia ukapata na ushauri
 
Ukiweza kuhifadhi maji yanaweza kukuaaidia katika kilimo kidogo cha mboga mboga hasa wakati wa kiangazi.
 
Maji ya mvua yanapatikana bure na kama yanatumika vizuri tunaweza kupunguza matumizi ya reservoirs. Ukihifadhi maji haya kwa matumizi ya binadamu inabidi kuyaongezea baadhi ya kemikali.

Maji ya mvua yanaweza kutumika kwa sewage system ya nyumba nzima. Unachimba shimo na kulisakafia kama shimo la maji. Ukiongeza na Simtank unaweza kuhifadhi lita 50,000 kipindi cha masika. Haya yanaweza kutumika mwaka mzima.

Chlorine Sterilisation
  1. The initial dosage to be a minimum of 5 milligrams of chlorine per litre of rainwater to be treated.
  2. A concentration of 0.5 milligrams of chlorine for every 1 litre of rainwater must be maintained, 30 minutes after the initial dose.

View attachment 1267222

View attachment 1267223

View attachment 1267229
Tatizo lako la maji ni mtaji wa mwanasiasa, usivune maji ya mvua utapunguza ahadi za Rais na Mbunge.
 
Maji tuyatumiayo ni machafu sana. Twapaswa kuweka vijitambo vidogo vya kusafisha kabla hayajatufikia kwenye bibomba vyetu.
Matenki hayasafishwi. Mabomba hayasafishwi
 
Wazo hilo zuri lilipaswa kutekelezwa na mamlaka zetu za maji safi na maji taka. Naifahamu nchi moja ambayo raia wake wanavuna maji ipasavyo na kunufaika!. Serikali ya nchi hiyo imekuja na mkakati wa kukusanya kodi ya uvunaji wa maji ya mvua kwa kuzingatia mita za mraba za eneo lililoezekwa.... Upo hapo?... Natabiri Mipango ataiandika hiyo!!.😉
 
wazo zuri sana, ntakapo jenga kwangu nitazingatia huu mfumo katika hatua za awali za ujenzi
 
wazo zuri sana, ntakapo jenga kwangu nitazingatia huu mfumo katika hatua za awali za ujenzi
Ukichimba mashimo ya maji taka, tenga na shimo la maji safi ya mvua.
 
Back
Top Bottom