Kisima kinahifadhi gallon 30,000 na simtanks mbili za lita 20,000 . Alivyojenga simtank zikijaa maji yanakwenda kisimani. Akiyahitaji anavuta kwa pump kwenda kwenye simtankNi njia nzuri ya jutunza mazingira pia, ametengeneza tanki la ukubwa gani? Kwakweli maji ya mvua ni mengi tu tukiweza kuyahifadhi hata kwa garden yanafaa.
Muulize Bashite mkuu wa hilo jiji lenye mtaa uitwao ufipa kwa nini mitaa mingine haina maji kwenye jiji kubwa la kibiashara?Huko ufipa huwa mnafanyaje?? Maana watu wanajisaidia nyumba za jirani, ofisi haina maji chooni
Kwani haya maji mengine kwenye mabwawa na visima hayatokani na maji ya mvua? maana kwa komenti za humu inaonekana maji ya mvua ni kitu tofauti sana
Wewe uliyesoma hayo tuambie, maana sisi wengine ni wataalam wa upasuaji wa ubongo na mfumo wa fahamuUmesoma kuhusu Hydrological cycle na Underground water?
Ungesoma usingeuliza ulichoandika!
Ukiweza kuhifadhi maji yanaweza kukuaaidia katika kilimo kidogo cha mboga mboga hasa wakati wa kiangazi.Pia idara ya Maji wanatiba mbalimbali za Maji kutokana na Maji husika siyo mbaya kuwaona
Nilifanikiwa kuwatembelea siku ya Nanenane wanaelekeza vizuri sana na Dawa zoa mbalimbali
Pia ni vema ukiwaona wakakupimia na Maji unayotumia ukapata na ushauri
Tatizo lako la maji ni mtaji wa mwanasiasa, usivune maji ya mvua utapunguza ahadi za Rais na Mbunge.Maji ya mvua yanapatikana bure na kama yanatumika vizuri tunaweza kupunguza matumizi ya reservoirs. Ukihifadhi maji haya kwa matumizi ya binadamu inabidi kuyaongezea baadhi ya kemikali.
Maji ya mvua yanaweza kutumika kwa sewage system ya nyumba nzima. Unachimba shimo na kulisakafia kama shimo la maji. Ukiongeza na Simtank unaweza kuhifadhi lita 50,000 kipindi cha masika. Haya yanaweza kutumika mwaka mzima.
Chlorine Sterilisation
- The initial dosage to be a minimum of 5 milligrams of chlorine per litre of rainwater to be treated.
- A concentration of 0.5 milligrams of chlorine for every 1 litre of rainwater must be maintained, 30 minutes after the initial dose.
View attachment 1267222
View attachment 1267223
View attachment 1267229
Ukiweza kuvuna vizuri maji ya mvua na kutumia umeme wa solar utaishi kwa gharama nafuu sana Tanzania. Tuna jua karibu kila siku linapotea tu.Wairan wanatushangaa sana wao wanavuna maji ya mvua kwa kilimo sisi tunayaacha halafu tunalalamika
sawa kabisa, japo wataalamu watahitajika maana ni suala nyeti kwa uhai wa mwanadamu.Ukichimba mashimo ya maji taka, tenga na shimo la maji safi ya mvua.