Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 51,453
- 41,274
My friends, ladies and gentlemen,
Sote ni mashuhuda kwamba, hivi sasa amani na utulivu wa nchi yetu kisiasa, kijamii na kiuchumi tangu tumalize uchaguzi mkuu wa kihistoria Oct.29.2025, unaendelea kuimarika na kushamiri vyema sana, na hiyo inatoa nafasi na fursa kwetu sisi sote kama familia ya mama Tanzania, kujiandaa vema na kukaa mguu sawa kuelekea maridhiano ya kihistoria ya kitaifa, ambayo hatimae yatatujengea msingi muafaka sana, kuelekea mchakato muhimu sana wa kupata katiba mpya, huku kila moja wetu akiwa tayari ana moyo mweupe na wa shukrani kwa taifa na kwa Mungu, kwa mema yote aliotutendea tangu tupate uhuru wa taifa letu.
Ni raia yangu kwa waTanzania wote, kote ulimwenguni, kutumia vizuri fursa hiyo adhimu ya maridhiano kusameheana, kusahihishana kwa hekima na kurekebishana kwa upendo, hasa kwenye yale maeneo ambayo, kwa namna moja au nyingine yalijenga hali ya uhasama au uadui miongoni mwetu kama familia ya Tanzania na pengine kupelekea vurugu, uharibifu na maafa ambayo yalituathiri sote kama ndugu wa baba na mama moja Tanzania.
Maridhiano yaweke msingi madhubuti wa kuepuka kurejea changamoto hiyo tena, na pasiwepo kundi la watu, chama cha siasa, taasisi ya dini au asasi ya kiraia kuhodhi au kujimilikisha mchakato huu muhimu wa maridhiano, kuelekea katiba mpya.
Mchakato uwe mali ya waTanzania wote.
Kumbuka maridhiano ni tendo la hiyari na sio lazima uwe sehemu ya maridhiano hayo ya kitaifa, utawakilishwa na walio wengi.🐒
Mungu Ibariki Tanzania