Mbasembase1970
JF-Expert Member
- Jun 11, 2015
- 6,056
- 4,608
Nikiwa si muumini wa hivi vitu viitwavyo dini itaniwia vigumu kuelezea nini maana ya Sunday School ama Madrasa. Hii nawaachia wafia dini zilizoletwa na washenzi waliotulazimisha kufuata mila na desturi zao na kuambia za kwetu ni za kishenzi. Wakatuletea Novel zao wakatuambia vinaitwa vitabu vitakatifu ambavyo kuna mistari inahalalisha utumwa na kushusha thamani ya wanawake.
Baada ya kuuamini ushenzi wao tukawaamini watusaidie kuwafundisha watoto wetu njia rahisi ya kumfikia Mola bila kujua tulikabidhi mbuzi kwa Simba aliyejifanya Beberu. Mengine ni historia.
Najua baadhi watakuja na comment kali hata za kunikashifu ama kuwakashifu watakao iunga mkono hoja. Bali ukweli utabaki palepale baada ya kutusaidia kwa kutuunganisha dini zimekuja kuwa vyanzo vya upotevu wa amani kwa jamii nyingi. Dini zimesababisha vita vikubwa duniani kuna baadhi ya maeneo vita vinaendelea mpaka leo.
Ifike wakati tukubali hizi dini tulizoletewa hazikuja kutusaidia bali kutuangusha tusifike huko mbinguni. Chini kuna clip ya kudhihirisha nini nilichokisema hapo juu. Huko nyuma tuliona mapadre wakilawiti watoto lakini sababu watu wa dini tunawaweka katika makundi ya watu wa Mungu tulinyamazia na hivyo kuwafanya vijana waendelee kunyanyaswa na washetwani.
Niweke neno la kuwaomba msamaha kwa watakaokwazika na huu uzi lakini ndiyo ukweli wenyewe lazima usemwe waziwazi badala ya kuendelea kulumbana dini ya nani bora zaidi hakuna dini iliyo bora zote ni za kishenzi.