Tujifunze kitu kwa misiba ya vigogo hawa na idadi ya watoto

Tujifunze kitu kwa misiba ya vigogo hawa na idadi ya watoto

Hao wana kipato na resources za kuhakikisha malezi na future za watoto wao hata ikitokea emergency wametoweka duniani .
Wewe na kazi yako hiyo ya ukuli kwa wahindi ,ulivyo zoba umezaa watoto kumi
Elewa mada wewe zwazwa
Nashukuru kwa kunisaidia wananipa kazi kubwa Sana kuwaelewesha hawa watu, hawaelewi kabisa
 
Na kuna uwezekano kuwa , Ndugulilie na Mafulu wasinge zaliwa endapo wazazi wao wangezaa watoto wa 2 tu...
Mkuu,

Unafikiri Ndugulile na Mafuru wasingezaliwa asingekuwepo mtu mwingine kama wao kufanya mambo waliyofanya au hata zaidi?
 
Watoto wakavu utasema wamefiwa na jirani.
Tunajidanganya eti tunawalea watoto kisasa. Mtoto tangu chekechea yupo boarding. Alirudi anakaa ndani "dada". Baadae anapelekwa kusoma na kuishi ughaibuni. Wazazi anaongea nao kwa video call tu. Mapenzi kwa mzazi ayatoe wapi?
 
Nipo nacheki hapa msiba WA Ndugulile, kuacha watoto wawili tuu, pamoja alikuwa ana uwezo wa kipesa na cheo lakini kaishia kwenye watoto wawili, watoto wawili hawa naona kawakuza na kuwasomesha kwenye shule za gharama inawezekana nje ya nchi maana hata Kiswahili chao ni broken sana wanakuwa kama sio watanzania.

Lawrence Mafuru nae nadhani aliacha watoto wawili tuu.

Swali kwa makapuku wenzangu, hivi Sisi maskini tunazaa watoto wengi ili iweje? na utakuta pengne hata uwezo wa kuwahudumia tuu kikamilifu kwenye elimu na gharama za kila siku hatuwezi, nini maana ya hii?

Nahis NI vizuri kuzaa watoto kulingana na kipato chako, ambao utawamudu vizuri, utakaowapa elimu ya uhakika sio hii ya kuunga unga.

Sisi maskini tunawaza eti tukizaa watoto wengi ndio hao badae watatusaidia, wewe mzazi somesha mtoto, hudumia kwa kadiri ya uwezo wako maana ni jukumu lako, badae akipata maisha mazuri NI yeye sasa atajua atakusaidiaje, ndio ile utakuta wazazi wananunia wakwe zao wanaona kama wao ndio wanafanya wasipewe pesa na mtoto wao.

Tuzae Kwa mahesabu, utakuta mtu ana watoto wanne, halafu kapanga chumba na sebule, sasa jiulize hapo ndani wanaishije, tuwekeze nguvu kwenye kujenga uchumi Kwanza na kuzaa kwa akili.

View attachment 3167382
Ni ulemavu wa kufikiria mtu unamiliki gari moja alafu watoto wawili badala ya kuwa na watoto sita.
 
Hivi kafarik kwa ugonjwa gani mbona cjaona popote ilipotajwa ugonjwa.. Hata salamu za familia hazikugusia kilichomuua

Wakati mwenzie Mafuru walitaja ugonjwa.
Kwa kiongozi wa umma inabidi waseme na Asię kiongozi kwa jamii ya waelewa huwa wanasema.
 
Safi sana,mim nilitaman niwe na mtoto mmoja tu,sahv ninao watatu

Wanawake sio watu wazur kabisa
 
Mkuu kama mtu hujawahi mlisha au kumsadia kwa hali na mali puguza ushauri kwa yasiyo kuhusu.
Kuzaa watoto wengi ama wachache hakuna formula! hivi kuna mtu ana mtazamo wa kuja kufa masikini kweli?

Sawa leo ni maskini je unaijua kesho yake? Sioni sababu ya kuzaa kwa kuangalia uchumi nilio nao maana nina malengo ya kuja kuwa tajiri mkubwa hapo kesho ....

hiyo mifano uliyotoa mkuu watu kama waalimu,police{samahani} basi hawapaswi kabisa kuwa hata na mfano wa watoto tu. hata mimi mwenye sipaswi kabisa kuwa hata theruthi ya mtoto maana hao mabosi ubosi wao hata siwezi linganishwa kwa no yoyote ile.
 
Nimewahi kuwa na mtazamo wa kijinga namna hii yaani eti niwe na watoto wawili, sasa nimefungulia watoto wanne mama tafauti na naendelea kuzaa aisee sababu utazijua ukija kuwa na akili timamu, ila nikukumbushe tu hakuna mtu amewahi kujutia kwa kuwa n watoto wengi
 
Donald trump anawatoto watano wakati Bill Clinton ana mtoto mmoja na Obama ana watoto wawili.

Kwanini tusimuige mwamba Trump.

JK wa msoga na marehemu Julius Kambarage Nyerere watoto zaidi ya watatu wakati Mzee wa Lupaso amekufa na wangapi sijui.
 
Unaposema fulani ana watoto wawli uwe unaongeza neno. KWA MKE WAKE WA NDOA AU ANAYETAMBULIKA.

UTANISHUKURU SIKU NYINGINE.
 
Back
Top Bottom