Tujifunze kushukuru! Zitto hatafuti umaarufu, alishakuwa maarufu tangia zamani

Tujifunze kushukuru! Zitto hatafuti umaarufu, alishakuwa maarufu tangia zamani

Mtondoli

Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
70
Reaction score
174
Niwakumbushe nyinyi mlioingia kwenye siasa juzi, mjue kwamba Zitto kwa kumuomba rais amwachilie mbowe hatafuti umaarufu, alishakuwa maarufu wakati ambao hawa wanaopiga kelele wote hawapo.

Zitto kabla ya Lissu alikuwepo na alikuwa maarufu, kabla ya mnyika, Kigaila Heche, Msigwa, Sugu na wengine wote unaowafahamu wewe.

Zitto alikuwepo na alikuwa maarufu, mbunge mmojawapo wa kwanza kwanza wa upinzani ukiwataja watano, Zitto alikuwepo. Hajaanza kuipigania Chadema Leo alianza kabla nyinyi wote hampo.

Kumwondoa Chadema zilikuwa njama za kumuua kisiasa kwa kumpa tuhuma za hovyo kabisa yeye na Mbowe hawajakutana barabarani mwachieni amzungumzie mnampa majina ya hovyo hamjui yy na Mbowe walikotoka.

Lissu alikuwa Kenya na badae ubelgiji mpinzani pekee aliyeenda kumuona kote huko no zitto mwachieni kinana wetu afanye siasa zenye tija sio makelele
 
Chadema wanalaani Mbowe kukamatwa
Lakini Zitto akisema Mbowe aachiwe..wanamponda Zitto..
As if Zitto ndo adui wao mkubwa

Zitto anamuombea Mbowe msamaha kwa kosa gani?
 
Mbna sasa unatufokea.....

Wakati mama kasema hii nchi ni ya demokrasia
 
Mbona Mabalozi wakiwasemea Chadema. Hamsemi mnajimudu?Zitto ndo adui wenu mkuu?

Mabalozi sio wanafiki wala hawataki political milleage. Simply hakuna aliyehitaji msaada wa Zito na kwa namna alivyoiweka. Hadaa wapelekewe wasiojitambua.
 
Ni mwenyekiti wa TCD, na Chadema walifikisha malalamiko yao TCD rasmi

Ni kweli kabisa, ila yeye anamuombea Mbowe msamaha katika hali ya upotoshaji. Mbowe sio mkosaji msamaha wa nini? Yaani ufanyiziwe kisha ndio uombe kusamehewa? Hiyo political milleage haikubaliki.
 
Waache waendelee kumtusi zitto huku yeye akiendelea kuwasemea mazuri watanzaia tunaendelea kuiona rangi ya chadema
 
Mbowe ataachiwa tu na huyu mama. Atake asitake. Aombwe ama asiombwe, atamwachia Mbowe.

Acha ajifarague tu
 
Kiukweli hawa chadema ni watu wenye fitina tu hasa Zaidi tundu lisu huwezi kuonyesha chuki kwa mtu anayekusemea mazuri
 
Chadema wanalaani Mbowe kukamatwa
Lakini Zitto akisema Mbowe aachiwe..wanamponda Zitto..
As if Zitto ndo adui wao mkubwa


Chadema wameshikwa na hasira ya; kwanini Zitto awe mtetezi katika ngazi za juu wa kuachiwa kwa Mbowe ilhali wao wapo tu huku wameshindwa kufanya jambo hilo.--- hofu yao ni hii kwamba Mbowe akiachiwa/akifutiwa mashitaka Zitto atapanda chat ya kisiasa na Chama chake kitapata hadhi kubwa, huu ni ubinafsi wa kisiasa wa Viongozi na wafuasi radicals wa Chadema.

Hao hawana huruma na kiongozi wao anayetaabika mahabusu, misukumo na hisia zao za mapambano ya kisiasa zimepofua sense ya ubinadamu katika nyoyo zao, watu wa aina hii ni wabaya kama watakabidhiwa nchi kuiongoza.
 
Niwakumbushe nyinyi mlioingia kwenye siasa juzi, mjue kwamba zitto kwa kumuomba rais amwachilie mbowe hatafuti umaarufu ,alishakuwa maalufu wakati ambao Hawa wanaopiga kelele wote hawapo,,zitto kabla ya lissu alikuwepo na alikuwa maarufu, kabla ya mnyika ,kigaila ,heche,msigwa,sugu na wengine wote unaowafahamu wewe zitto alikuwepo na alikuwa maarufu,,mbunge mmojawapo wa kwanza kwanza wa upinzani ukiwataja watano zitto alikuwepo,hajaanza kuipigania chadema Leo alianza kabla nyinyi wote hampo ,kumwondoa chadema zilikuwa njama za kumuua kisiasa kwa kumpa tuhuma za hovyo kabisa yeye na mbowe hawajakutana barabarani mwachieni amzungumzie mnampa majina ya hovyo hamjui yy na mbowe walikotoka,lissu alikuwa Kenya na badae ubelgiji mpinzani pekee aliyeenda kumuona kote huko no zitto mwachieni kinana wetu afanye siasa zenye tija sio makelele
Humjuwi Zitto? Waulize wanao mjuwa wakupe japo data uje kurekebisha hili andiko... Wewe njoo tuungane uku tule na kunya tuwaache majasusi wapambane ...
 
Ni kweli kabisa, ila yeye anamuombea Mbowe msamaha katika hali ya upotoshaji. Mbowe sio mkosaji msamaha wa nini? Yaani ufanyiziwe kisha ndio uombe kusamehewa? Hiyo political milleage haikubaliki.


Huo ni uongo unaousema, katika hotuba yake Zitto hakumuombea Mbowe "MSAMAHA" --- hakuna neno Msamaha, nenda kamsikilize vyema Zitto alivyosema.
 
Back
Top Bottom