Tujifunze kutafakari: Aliyekimbia toka Kigoma alitumiaje siku 22 umbali wa 1400KM?

Anastahili pongezi
 
Shortcut ???? hahahahah
 
2. Mchana aliutumia kukimbia na kutembea kwa masaa zaidi ya 15 kwa siku

HAKIKA HESABU ZAKO HAZINA WALAKINI 😀
Hujaelewa nini hapo? Maana yake ni kwamba mchana wote alitembea na kukimbia meaning 12 hrs na mengine 3 yale ya alfajiri na jioni
 
Unafahamu njia alizopita au njia zote ni hizo km zako 1400?
 
Njia yako yakupata jibu la hiyo hesabu ni ndefu na complex sana. Nyie ndio mlitufanya tukimbie hesabu😬😬😬🏃‍♂️

Yaani nimeambulia tu 5km/hr
 
Dar-Kigoma Ni Km 1253.... 1253/22=57km kwa siku... Hi Inawezekana Kabisa kwa Pace ya 6.3km/hr..!!! Maana yake akikimbia masaa Tisa kwa Siku inatosha Sana...Pia Inawezekana kwa Mtu mzoefu
 
Mimi nilikua natumia dk 40 kwenda shule umbali wa km 6 kurudi km 6 ni mpando kidogo natumia lisaa 1 tena tunatembea tupo relaxed hakuna jasho mwilini.

Nachoweza kusema jamaa aongeze mazoezi ametuangusha wanariadha kwa siku anaoaswa kwenda km 100 au zaidi.

Kipindi kijacho nategemea atatumia siku 15 tu ama pungufu zaidi.
 
Yah.
Mi huwa nafanya jogging nikiwa peke yangu kwa sababu sipendagi saikolojia ya kukimbia kwenye makundi maana nahisi yananinyima fuursa ya kukimbia kwa speed ninayoitaka. Mi ni mtu wa high speed.

Huwa nakimbia 23km kwa saa kila jioni siku za kawaida na asubuhi weekend.

So huyo muha yawezekana ni mkweli
 
 
Yaani ukimbie kileta 5 kwa saa moja?
Sasa hii sayansi yako ni ya aina gani? Hata mtu asiye mwanariadha anaweza kukimbia mpaka kilometa 30 kwa saa.
Sasa sembuse mwanariadha?
 
1400/22=63

Haiwezekani kwa siku binadamu atembee kilomita 63.Never!
Una maoni gani kuhusu yule Muhindi ambae alikimbia zaidi ya 9900km ndani ya siku 100 huku lengo lake likiwa kukimbia 10,000km?
 
Hiyo speed ya 5 km per hr ni speed ya kutemba sio kukimbia
Na inakufanya uwe na nguvu na pia pumzi isikupotee. Ukikimbia, utafanya 20kph kwa labda saa 1 zima halafu utashindwa kuendelea kukimbia sababu ya uchovu. Wakati hiyo ya kutembea angeweza kufanya hata masaa 8 kwa siku akakava 40kph..

Yaani ruti ndefu ukikimbia utaenda umbali mfupi kuliko anayetembea
 
Huwa unakimbia umbali gani?
 
Mtoto wa mama kula kulala unaweza kuona ni maajabu au anatumia uchawi, hebu fikiri marathon km 42 yule mkenya alipiga chini ya saa moja, na huyu jamaa anafanya hayo mazoezi kama anavyosema aliwahi kwenda tabora na kurudi kigoma akikimbia, na hizo km 1400 huyo sio treni kwamba lazima afuate njia anaweza kupita shortcut na akapunguza km nyingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…