Tujifunze kutafakari: Aliyekimbia toka Kigoma alitumiaje siku 22 umbali wa 1400KM?

Tujifunze kutafakari: Aliyekimbia toka Kigoma alitumiaje siku 22 umbali wa 1400KM?

Umbali wa kutoka kigoma kwenda Dar ni almost 1400KM

Ili ufanikiwe kutoka kigoma kwa kukimbia inabidi at most ukimbie kwa Speed ya 5km/hr ili kumaintain stability na pumzi!
Kwa maana hiyo, ili kupata mda sahihi ukichukua umbali 1400 gawa kwa mwendo 5 utapata majibu ya 280 ambayo ni idadi ya masaa kwa umbali huo mfululizo NON STOP ( Yaani hakuna kukojoa wala kula)

Masaa 280 ukichukulia alikimbia mchana NON STOP 12 Hours maana yake (280/12) ni sawa na siku 23 na masaa mawili (23.3) NON STOP

Hivyo basi, speed ya 5Km/hr kwa masaa 12 mfululizo bila kupumzika, bila kukojoa,Bila kula na kunywa, bila kuchimba dawa yaani kila sekunde na hatua, tunatarajia mtu angetumia siku 23.3 (JAMBO AMBALO HALIWEZEKANI BINADAM Kukimbia 12hrs bila kusimama)

Kama kwa gari tu ni ngumu kukimbia 12hrs pasipo kuchimba sawa, iweje kwa mkimbia kwa mguu?

Huyu jamaa kawezaje kukimbia kwa siku 22 kutoka Kigoma hadi Dar wakati kiuhalisia 12hrs NON STOP ni siku 23?

Ina maana huyo jamaa alikatiza misitu ya hatari huko nyakanazi, na kupandisha mirima pasipo KUSIMAMA 12 hours Kila siku Hadi atangazwe katumia siku 22?

Tunaambiwa alianza safari tarehe 15 April mchana, na kufika Dar tarehe 7 may ! Amewezaje kutumia mda huo ambao ni mchache zaidi ya uhalisia?

JE, hakusimama kula, kuchimba dawa, kukojoa wala n.k
Mbona sayansi inagoma?
AU NDO TUAMINI ULE MSEMO kuwa alikimbia mijini, inje ya mji alidandia maroli?
Au hii hesabu ikoje?View attachment 1782115View attachment 1782116View attachment 1782117
Tulishafanywa vichwa wa wendawazimu ata mimi jana niliangalia habari nikawasikiliza nikawazoom nikawachekiii nikasema hiiiiiiiii yaaaaniii.
 
1400/22=63

Haiwezekani kwa siku binadamu atembee kilomita 63.Never!
Jamaa ameshakuambia hukimbia km43 kwa chini ya masaa3, maanayake akiamua kukimbia kwa masaa sita 86 km zitahusika! Hivyo 63km ni chai kwake!
Ila ukikaa utafakari inafikirisha sana i see🤔!
 
Ila yale mapori i see yanatisha sana! Huyu alikuwa ameamua kukomiti suisaide! Anatakiwa achukuliwe sheria kali ili liwe funzo kwa wengine wenye mawazo kama yake😡!
 
Jamaa ameshakuambia hukimbia km43 kwa chini ya masaa3, maanayake akiamua kukimbia kwa masaa sita 86 km zitahusika! Hivyo 63km ni chai kwake!
Ila ukikaa utafakari inafikirisha sana i see🤔!
Mambo ya kupumzika,afya ya binadamu,kuchoka,distabances za hapa na pale na kadhalika umeviangalia?
 
chukua km1400 gawanya kwa siku 22 ndio unapata alikuwa anakimbia km64 kila siku, ukigawa kwa masaa12 ya siku moja mchana tu, unapata kwa saa moja alikuwa anakwenda km5, ambayo ni kawaida kwa wakimbiaji, navojua alikimbia sana asubuhi na jioni wakati mchana alikuwa anatembea.
 
Mimi hutumia dakika 45 kutembea kwa mguu urefu wa kilometa 5.

Km 5 per hour hyo sio sahihi kwa binadamu
 
Si tulishakubaliana kuwa huyu jamaa alikua anapanda malori usiku
 
Watu wa Yanga kwa ujanja ujana tunawajua wala huwezi pata nao shida kiuhalisia it is imposible na Uongozi wa Utopolo walivyokuwa hawana akili eti wakamwita na kuamini kweli alitembea toka kigoma hadi Dar hilo jambo halikuwa kweli ilikuwa kiki tu kwa yanga na vile Yanga hawapati attention kubwa katika midia kama vile Simba na wao huwa wanatafuta attentiion ili wazungumzwe kama Simba hali kama hii inapelekea kufanya mambo ya ajabu kama haya yaana katika vitu navyochukia kupenda sifa katika jamii kwa jambo lisilowezekana
 
Jamaa ameshakuambia hukimbia km43 kwa chini ya masaa3, maanayake akiamua kukimbia kwa masaa sita 86 km zitahusika! Hivyo 63km ni chai kwake!
Ila ukikaa utafakari inafikirisha sana i see🤔!
Siyo rahisi kukimbia marathon mbili kwa chini ya masaa 6.
 
Amejenga mwili
Juzi me nlitembea km 15 kwa 1h 45min
 
Hili jambo linawekana tu kwa mpangilio mzuri- muda wa kukimbia kila siku,muda na mahali pa kupumzika,chakula na maji ,usalama wa mkimbiaji(wanyama wa pori,magari barabarani,majambazi) na la muhimu zaidi mazoezi ya kutosha kuhimili kupiga masafa marefu kila siku kwa siku 20+ mfululizo.
 
Oya mambo mengine mbona ni yakujiongeza tu wewe mwenyewe tumepigwa pale.
 
Back
Top Bottom