Tujifunze kutafakari: Aliyekimbia toka Kigoma alitumiaje siku 22 umbali wa 1400KM?

Tujifunze kutafakari: Aliyekimbia toka Kigoma alitumiaje siku 22 umbali wa 1400KM?

1400/22=63

Haiwezekani kwa siku binadamu atembee kilomita 63.Never!
Km 63 akikimbia kilomita 5 kwa saa anahitaji masaa 13 maximum wewe unasema haiwezekani ?
Full Marathon huwa ni km ngapi na watu kutumia masaa mangapi ?
 
Nadhani mtoa mada hana ufahamu na umbali kwa kilomita alizozitaja. Mtu kutembea kilomita 60 kwa siku ni jambo la kawaida sana. Kwa mfano huo mwendo wa km 5 kwa saa ni mwendo mdogo sana. Mimi huwa nikipenda natembea chini ya nusu saa kutoka ofisini hadi nyumbani umbali wa kama km 4 hivi.

Hivyo kwa mwanariadha kukimbia kutoka Kigoma hadi Dar kwa siku 22 inawezekana kabisa bila tatizo lolote.
Kilomita tano ni safari ya 45 minutes kwa kutembea
 
Jamaa anashangaza sana mtu akimbie 5km tu per hour ?
Kukimbia 5km/h ni sawa na 12m/km. Hii ni pace ndogo sana, hata anayetembea kwa haraka anaweza fanya hivyo. Shida ni kwamba ana nguvu za kufanya hivyo kwa siku 22 mfululizo kwa umbali mrefu?

Screenshot 2021-05-13 14.40.54.png
 
Ni jambo la kawaida tu hata kama alikuwa anasimama na kupiga story ni sawa na usikariri sidhani kama alipitia hiyo njia ya nyakanazi ni ndefu mno huyu alipasua tabora ila ni kawaida mimi tu nakimbia zaid ya km 15 ndani ya saa 1 na dakika 17
 
Umbali wa kutoka Kigoma kwenda Dar ni almost 1400KM

Ili ufanikiwe kutoka Kigoma kwa kukimbia inabidi at most ukimbie kwa Speed ya 5km/hr ili kumaintain stability na pumzi! Kwa maana hiyo, ili kupata mda sahihi ukichukua umbali 1400 gawa kwa mwendo 5 utapata majibu ya 280 ambayo ni idadi ya masaa kwa umbali huo mfululizo NON STOP ( Yaani hakuna kukojoa wala kula)

Masaa 280 ukichukulia alikimbia mchana NON STOP 12 Hours maana yake (280/12) ni sawa na siku 23 na masaa mawili (23.3) NON STOP

Hivyo basi, speed ya 5Km/hr kwa masaa 12 mfululizo bila kupumzika, bila kukojoa,Bila kula na kunywa, bila kuchimba dawa yaani kila sekunde na hatua, tunatarajia mtu angetumia siku 23.3 (JAMBO AMBALO HALIWEZEKANI BINADAM Kukimbia 12hrs bila kusimama)

Kama kwa gari tu ni ngumu kukimbia 12hrs pasipo kuchimba sawa, iweje kwa mkimbia kwa mguu?

Huyu jamaa kawezaje kukimbia kwa siku 22 kutoka Kigoma hadi Dar wakati kiuhalisia 12hrs NON STOP ni siku 23?

Ina maana huyo jamaa alikatiza misitu ya hatari huko Nyakanazi, na kupandisha milima pasipo KUSIMAMA 12 hours kila siku hadi atangazwe katumia siku 22?

Tunaambiwa alianza safari tarehe 15 April mchana, na kufika Dar tarehe 7 may! Amewezaje kutumia mda huo ambao ni mchache zaidi ya uhalisia?

JE, hakusimama kula, kuchimba dawa, kukojoa wala n.k Mbona sayansi inagoma?

AU NDO TUAMINI ULE MSEMO kuwa alikimbia mijini, inje ya mji alidandia maroli?
Au hii hesabu ikoje?

View attachment 1782115View attachment 1782116View attachment 1782117
Mambo mengine hua tuna yaacha kama yalivyo
 
Huyu Jamaa wa Kigoma ni Muongo sana Tena Kipindi hiki cha Ramadhani!
Mtu tuu akikimbia Full Marathon 42km kwa pace ya 3-4!
Yupo hoi kesho hawezi amsha tena,
Eti Jamaa ka maintained kwa Siku 22!
Hata Kama Alikuwa anakimbia Kwa Pace ya 5 Flat siku Nzima Masaa 12!Kesho hawezi Kuunganisha Eti Pace ya 5Tena flat kwa asiku 22!
Yaani Sijui kuna watu wanajua Kukimbia ukiwa barabarani Ukifumba macho unaenda tuu!
Ndio Maana Vyombo vya Riadha (RT) wamemchunia jamaa wanajua Ni uwongo na hawezi Kuthibitisha!Eti jamaa continue Kakimbia 22days Non stop na Speed ile ile...Nasema hivi wale ambao wanasikia Mbia
Waje Dar city Marathon tarehe 23/5/2021 Mnazi Mmoja wakimbie hata 5Km ndio watajua tunaposema Kukimbia Tunamaana Gani?
UMEONGEA POINT SANA BIG UP SANA
 
Wewe utakuwa mboga saba kukimbia kl 5 utumie saa nzima hapo utakuwa unatambaa wala syo hata kutembea
 
Ni kutembea pasipo masihara lakini kigoma isikie tu! Dreva yoyote anaijua ilivyo palefu halafu anatokea NGIDO MMOJA anasemaje amekimbia kwa mguu siku 22 tena anakwambia alipumzika morogoro siku 3 kwa homa ya tumbo
Sasa nyie wajuba mlikuwa mnatembea wastani wa 70km/h umbali wa 1400km ambapo mlitumia masaa 20, sasa mjuba katumia siku sio masaa, wazee mlifeli hesabu?
 
Mtoa mada unaweza kuwa na point ILA mambo ya kukimbia yamekupitia kushoto. Ngoja Mimi mkimbiaji wa kujifurahisha nikuwekee namba zangu.
Huwa nakimbia kitu wanaita PACE ya 6(hii ni yetu wazee vijana). Maanake ni kuwa kwa dakika 6 nakimbia km1 Kwa maana hii 1hr nakimbia 10km. Na huwa nashiriki half marathon 21km natumia masaa mawili na dakika 20 hivi.
Sasa ina maana kama sitasimama kwa masaa 10 nitakimbia km 100+
Tafuta taarifa kutoka kwa jamaa wa Goba runners wana watu wao wanakimbia Dar Moro. Wengine walikimbia kuzunguka Dar usiku saa sita Hadi 12 asubuhi I guess sikumbuki ni km ngapi. Wapo wengi wanakimbia kama huyu jamaa wa Kigoma mkoa to mkoa.
Binafsi naona kabisa inawezekana toka Kigoma mpaka Dar kwa hizo siku.

Umbali (Kigoma-Dar)/Muda (siku) alizotumia. = 1400/22 = 63.63km

Akikimbia masaa 10 kwa siku inamaana kwa kila saa anakimbia 6.4km. Akianza safari saa 10 alfajiri na akipumzika saa 12 jioni ukitoa masaa 2 ya breakfast na lunch yanabaki almost masaa 11. Yanatosha kukimbia hata km 70.

Kuna siku atakimbia nyingi zaidi na nyingine atakimbia chache. Kutokana na fatigue.

Ni jambo linawezekana kabisa.
 
Hivi nyie mnadhani watu wanajua hesabu kiviile?
Hesabu sio rahisi kama mnavyodhani.ndo maana wana simba mnapinga

Kama alitumia 22 days basi ni mzembe[emoji4]

Hizo 22 days ilibidi atumie mtu wa kawaida ambae hana mazoezi.

Mtu ambae hawezi kimbia hata mita 200 kitambi kule, kweli anaweza amini kuwa jamaa aliweza?

Nimesoma comments za wanamazoezi + wale ninaowajua personally.

Kabisa inawezekana acheni ubishi nawachapa viboko.
Comments nyingi hazina reasoning.

Mtu wa mazoezi anafika dar ndani ya siku 16 straight.

Km 63 kwa siku hata watoto wa shule wanazi-cover.
 
Binafsi naona kabisa inawezekana toka Kigoma mpaka Dar kwa hizo siku.

Umbali (Kigoma-Dar)/Muda (siku) alizotumia. = 1400/22 = 63.63km

Akikimbia masaa 10 kwa siku inamaana kwa kila saa anakimbia 6.4km. Akianza safari saa 10 alfajiri na akipumzika saa 12 jioni ukitoa masaa 2 ya breakfast na lunch yanabaki almost masaa 11. Yanatosha kukimbia hata km 70.

Kuna siku atakimbia nyingi zaidi na nyingine atakimbia chache. Kutokana na fatigue.

Ni jambo linawezekana kabisa.
Intelligent person
 
Back
Top Bottom