Tujifunze: Niliuza simu na kuanzisha biashara

Small bring big that is the principle of business ,what u need to make more effort for what u have started don't see embrace to any one don't hesitate do it, we are many in town, waiting for employment
Fact
 
Japo mleta mada anaweza kuwa si mhusika mkuu, ila ni mawazo mazuri pia ushauri kwa vijana ambao unakuta simu ya laki 3 wakati soli ya viatu vyake imeisha kwa kutembeza bahasha ya kaki kuomba ajira wakati hiyo pesa ni mtaji tosha..
Umeandika kifasihi umeuvaa uhusika, hongera lakini kwa ubunifu umeleta wazo zurii Jukwaani
 
Good idea! Ila sasa hivi unatumia simu gani kuingia humu JF
Nmejieleza mkuu, natumia ya wife kuingia mtandaon mara moja kuchek habar na kubadilishana mawaz km hv na zaid kuona km kuna email ya kuitwa huko tulikojarb au laa
 
Umeandika kifasihi umeuvaa uhusika, hongera lakini kwa ubunifu umeleta wazo zurii Jukwaani
Ni mim mwenyew na sio km hvo uzaniavo mkuu, con faida ya kudanganya hvo mkuu
 
Mkuu mtaji wa chips kwa laki mbili. Ebu fafanua kidogo mkuu. Kumbuka huyu mtu hana majiko wala vyombo
 
Kabla sija comment ningetamani kujua hizo yebo ni product za hapa hapa nchini kwetu ama?

Maana huu uchuuzi wa kuongezea ajira Wachina unaniumiza sana kichwa.
Acha kukatisha tamaa watu aisee.Toa ushauri sio kuanza kuhoji hoji mambo ambayo hayamjengi mtoa maada
 
Acha kukatisha tamaa watu aisee.Toa ushauri sio kuanza kuhoji hoji mambo ambayo hayamjengi mtoa maada
Mtoa mada alishaelewa concern yangu na alishatoa jibu.....sasa hilo la kukatisha tamaa ni hisia zako tu.

Sipingani na kufanya biashara yoyote ile na wala mimi sijamlenga mtoa mada moja kwa moja...so just be humble and sit down.
 
A very big brain, big up
 
Sio kweli, japokua inawezekana....umetengeneza story.. Ila kama ulikua unasita kuchukua hatua, nakutia moyo, anza kufanya hivyo..
 
Ukweli ni mchungu ila inabidi usemwe tu maana waweza kuwa na msaada.
Katika zama hizi kukosa simu ni kupunguza wigo wa mawasiliano yenye tija kwa zaidi ya asilimia 80.simu ni nyenzo kwa maana kule ulipoomba kazi umeacha namba ya simu na e-mail kwa hyo unaweza kupigiwa simu ukawa hupatkan ikala kwako na pia wanaweza kuku-email ukaja ukaona ujumbe kwa muda uliochelewa hvyo utakuwa umepoteza. Pia waswahili wanasema ongea na watu upate viatu, hii ina maana kwamba kile kitendo cha kuwasiliana na wenzako uliomaliza nao chuo na mkapeana update ya kile kinachoendelea mtaani na kujulishana michongo ingesaidia ww kuwa na mawazo mapya kila uchao. Na kwa ujumla simu ni nyenzo kubwa sana kwa mtu ambaye anatafuta.cha kukushauri ungenunua hata simu ya button ya elf 15 ukawa unaunga sms za elf 2 za mwezi hyo hela iliyobaki ungeanza biashara zako.mwisho naomba uchukue hii "uwekezaji wowote ni mzuri unapofanyiwa uchunguzi na unapoandaliwa mazingira yakuleta tija kinyume na hapo utakuja kujuta kwann uliuza simu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…