Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari wakuu,
Kutokana na ugumu wa maisha na ajira ndo hatuelewi kama zitakuja lini nilipata wazo la kuuza simu yangu pendwa Tecno W3 kwa laki moja na kuamua kufanya hivi;
![]()
![]()
Kama muonavyo hapo juu, nilinunua Yebo aina na rangi mbalimbali, mifuko ya sulfate(kipindi cha mavuno hiki), chumvi, viberiti na sukari.
Nazunguka mitaa na meneo ya jirani napanga mizigo yangu kama muonavyo hapo juu nachopata kidogo Mungu anasaidia.
Nimeona nilete kwenu ili tuweze kupeana fursa zingine na mawazo mbadala, pia lazima tujue laki moja pia ni mtaji tosha tu tatizo ni uthubutu.
NB: Simu hii nimeazima na huwa naazima mara moja moja kwa wife kuangalia labda email imepotea njia huko.
Nawasilisha, matusi dharau ni mwiko
Umeandika kifasihi umeuvaa uhusika, hongera lakini kwa ubunifu umeleta wazo zurii JukwaaniJapo mleta mada anaweza kuwa si mhusika mkuu, ila ni mawazo mazuri pia ushauri kwa vijana ambao unakuta simu ya laki 3 wakati soli ya viatu vyake imeisha kwa kutembeza bahasha ya kaki kuomba ajira wakati hiyo pesa ni mtaji tosha..
Oh, hiyo ni afadhali.Made in Mkuranga
Chai hiiHongera sana mkuu!!! Ni ujasiri ulioje!!!
Yaani mie natamani niiuze simu hii ata leo ili niingize pesa kwenye biashara.... Sema simu yenyewe ya kuazimwa [emoji26][emoji26][emoji26] Nimependa kweli wazo lako
Mkuu mtaji wa chips kwa laki mbili. Ebu fafanua kidogo mkuu. Kumbuka huyu mtu hana majiko wala vyomboHapo uko vizuri ndugu Mimi nikushauli kama upo center au town au karibu na chuo fungua biashara ya chips itakulipa kuzidi hiyo unayo Fanya sababu kula lazima kila siku watu wanakula.
Ila izo yebo MTU akinunua Leo mpaka ziishe ndio aje kununua tena.
Mtaji Wa chips unaitaji laki mbili tu ivyo uza na cm ya mkeo ongezea utatoka tu ndugu.
Usiogope wala usiwe na haibu. Mimi mwenyewe baada ya kumaliza chuo nilikaa kwa shemeji ajira hakuna
Nikabahatisha kwenye Beting nikapata mkwanja nikaanza biashara ya chips ilinilipa mpaka nilipo pata ajira yakudumu kanda ya ziwa so najua unachofanya usikate tamaa mzazi.
Because I think you can make it, in fact, I'm sure and if you fall, stand tall and comeback for more.
Because ain't nothing worse than to stay at home wait for an employment man.
You Got me man
Do not stop man until you get enough.
Acha kukatisha tamaa watu aisee.Toa ushauri sio kuanza kuhoji hoji mambo ambayo hayamjengi mtoa maadaKabla sija comment ningetamani kujua hizo yebo ni product za hapa hapa nchini kwetu ama?
Maana huu uchuuzi wa kuongezea ajira Wachina unaniumiza sana kichwa.
Mtoa mada alishaelewa concern yangu na alishatoa jibu.....sasa hilo la kukatisha tamaa ni hisia zako tu.Acha kukatisha tamaa watu aisee.Toa ushauri sio kuanza kuhoji hoji mambo ambayo hayamjengi mtoa maada
A very big brain, big upHabari wakuu,