Tujifunze softwares za music/audio production

Tujifunze softwares za music/audio production

Nitaamini kwa ushahidi, kwa ninavyoelewa android haina huu uwezo.
Labda sijaelewa, kama nu kuhusu kumpigia mtu simu na kumsikilizisha nyimbo zilizopo katika hiyo simu bila kukata simu... Basi kwa simu ninayokwambia inawezekana.. ukiweza nipe No. Nikupigie niweke na wimbo niuplay bila kukata hiyo simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi una faida sana, mimi napenda hiphop ngumu na ya tempo ya chini. Nimekuwa nikitengeneza beats kadhaa na nina mpango wa kuwa na home studio. Naomba wazoefu mnijuze ni vipi ninatakiwa nivizingatie katika kutengeneza beats za hiphop ngumu nyeusi.
 
Baada ya kuufuatilia huu uzi kwa muda mrefu kidogo japo si kwa kitambo sana, nami nilipata ushawishi wa kujaribu kutumia DAW ya Fl Studio, nilianza kutumia Fl Studio 12, baada ya hapo nikawa nabadili versions kila nilipopata taarifa kwamba zilitoka-versions mpya.

Safari ya Fl Studio haikuwa rahisi, hapo awali sikuelewa chochote. Yaani kujua kwamba hii ni channel Rack na vitu vingine vingi. Nakumbuka siku moja nilijaribu kutengeneza beat langu, niliweka snares zile zinazotoa sauti ya bati chache na kutumia drum Loops za drums za humo humo ndani ya Fl Studio, baada ya muda nili-export hiyo "beat" 😂😂😂 na kumpelekea jamaa mmoja ambaye alikuwa mwimbaji wa Bongofleva darasani kwetu, aliishia kuniambia "kazi nzuri ila haina ubunifu" 🤣🤣🤣🤣
 
Thanks kwa info, eti VST plugin ipi nzuri kwa kufanya final mastering yenye kutoa quality nzuri kama sina sound card?
Mastering mkuu haihitaji specific plugin, ni sikio na kujua weakness ya sound Yako then utaweza fanya levelling
 
Kumekuwa na ushindani mkubwa kwa miaka ya sasa hivi katika utengenezaji wa softwares ambazo hutumika katika music production. Ilikuwa kazi sana katika miaka kadhaa ya nyuma kwa mtu aliyetaka kuwa music producer kutokana na alitakiwa kujifunza na kumiliki vifaa vingi ambavyo gharama yake ni kubwa kidogo so wengi wao waliishia kutamani tu pasipo kujifunza.

Lakini kutokana na mabadiliko ya teknolojia siku hadi siku watu wanagundua njia rahisi ambayo inaweza kumsaidia mtu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja japokuwa anaweza kutokuwa na baadhi ya vifaa.

Softwares nyingi sana siku hizi ambazo watu huzitumia katika audio production kulingana na matakwa na uwezo wa mtu binafsi. Leo nitazungumzia baadhi ya softwares faida na hasara zake ambazo wewe kama ungependa kujifunza audio production waweza kuchagua ikufaayo.

Tunaanza na Fruity Loops (FL Studio). Faida zake ni kupatikana kwa urahisi na hukupa life time updates, rahisi kutumia, unaweza kutumia bila ya midi instruments, waweza load instruments nyingi uwezavyo,haihitaji system specifications kubwa mfano ram hata 512mb inatosha. Zipo faida nyingi ila hizo ni baadhi.

Tuje kwenye hasara haina auto saving project ambapo itakupa tabu wakati ikitokea imekorofisha kwa muda ile project yako huwezi kuikuta, inahitaji umakini wa hali ya juu wakati wa mixing na mastering wa nyimbo yako, haina time stretching nzuri kama softwares nyingine nk.

Software nyingine ni Cubase. Faida zake ni inakuwezesha kurecord multi tracks kwa muda mmoja, ina time stretching nzur ambayo inakupa option ya kuchagua jinsi utakavyo, inafanya mixing and mastering kwa ubora zaid nk. Hasara zake ni original setup yake mfano cubase 5.1 ni kubwa sana 6 GB, inahitaji system specifications kubwa, ni ngumu kutumia kwa mtumiaji wa mara kwanza, inahitaj midi instruments, pia sound card kwa ajili ya high quality sound nk.

Software nyingine ni Reason, Ableton live. Faida zake na hasara ni zile zile kama za cubase hazina tofauti sana.

Logic Pro X hii ni special kwa ajili ya Mac OS haipo kwenye Windows na hii ni moja ya hasara zake. Faida zake ni ina load instruments haraka zaidi kutokana na uwezo mkubwa wa computer aina ya Mac, mixing na mastering zinakuwa na ubora mzuri kutokana na built in plugins zake zenye ubora.

Hizo ni baadhi ya softwares za audio production ambazo unaweza kuchagua ikufaayo na kuanza kujifunza leo.

Nakaribisha michango yenu
Mkuu FL ina autosave na hii feature ipo kitambo sana, nimeitumia sana kurecord, mix na kumaster,
Na ukija kwenye uwezo hebu nikuulize, utarun kontakt 5+ kwenye PC ya 512MB au unafanya masiala.

FL ni very powerful software japo wengine hutumia kupiga instrument lakini hata sound recording, mixing and mastering ipo vizuri sana, na na recommend Kwa yeyote.

Ukija kwenye business
Hizi DAW unatakiwa kuzielewa karibia zote na uzuri wake zinatofautiana muonekano lakini vitu ni vile vile, ni rahisi kushift mfano kutoka FL kwenda Pro Tools kuliko kutoka Maya kwenda Zbrush Kwa watu wa modelling.

Kwenye biashara ukizielewa zote inakupa uwanja mpana sana mana unaweza Kuta studio hawatumii FL na wewe umeizoea FL so utashindwa kupewa session.

Kwahiyo FL, Logic, ProTools, Studio One, Ableton na Cubase unatakiwa kuzielewa zote kwenye industry.
 
Mkuu FL ina autosave na hii feature ipo kitambo sana, nimeitumia sana kurecord, mix na kumaster,
Na ukija kwenye uwezo hebu nikuulize, utarun kontakt 5+ kwenye PC ya 512MB au unafanya masiala.

FL ni very powerful software japo wengine hutumia kupiga instrument lakini hata sound recording, mixing and mastering ipo vizuri sana, na na recommend Kwa yeyote.

Ukija kwenye business
Hizi DAW unatakiwa kuzielewa karibia zote na uzuri wake zinatofautiana muonekano lakini vitu ni vile vile, ni rahisi kushift mfano kutoka FL kwenda Pro Tools kuliko kutoka Maya kwenda Zbrush Kwa watu wa modelling.

Kwenye biashara ukizielewa zote inakupa uwanja mpana sana mana unaweza Kuta studio hawatumii FL na wewe umeizoea FL so utashindwa kupewa session.

Kwahiyo FL, Logic, ProTools, Studio One, Ableton na Cubase unatakiwa kuzielewa zote kwenye industry.
Nimejaribu kuikimbilia Ableton V9, nimetokwa damu aisee.
 
Back
Top Bottom