Tujifunze softwares za music/audio production

Nitaamini kwa ushahidi, kwa ninavyoelewa android haina huu uwezo.
Labda sijaelewa, kama nu kuhusu kumpigia mtu simu na kumsikilizisha nyimbo zilizopo katika hiyo simu bila kukata simu... Basi kwa simu ninayokwambia inawezekana.. ukiweza nipe No. Nikupigie niweke na wimbo niuplay bila kukata hiyo simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi una faida sana, mimi napenda hiphop ngumu na ya tempo ya chini. Nimekuwa nikitengeneza beats kadhaa na nina mpango wa kuwa na home studio. Naomba wazoefu mnijuze ni vipi ninatakiwa nivizingatie katika kutengeneza beats za hiphop ngumu nyeusi.
 
Baada ya kuufuatilia huu uzi kwa muda mrefu kidogo japo si kwa kitambo sana, nami nilipata ushawishi wa kujaribu kutumia DAW ya Fl Studio, nilianza kutumia Fl Studio 12, baada ya hapo nikawa nabadili versions kila nilipopata taarifa kwamba zilitoka-versions mpya.

Safari ya Fl Studio haikuwa rahisi, hapo awali sikuelewa chochote. Yaani kujua kwamba hii ni channel Rack na vitu vingine vingi. Nakumbuka siku moja nilijaribu kutengeneza beat langu, niliweka snares zile zinazotoa sauti ya bati chache na kutumia drum Loops za drums za humo humo ndani ya Fl Studio, baada ya muda nili-export hiyo "beat" πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ na kumpelekea jamaa mmoja ambaye alikuwa mwimbaji wa Bongofleva darasani kwetu, aliishia kuniambia "kazi nzuri ila haina ubunifu" 🀣🀣🀣🀣
 
Thanks kwa info, eti VST plugin ipi nzuri kwa kufanya final mastering yenye kutoa quality nzuri kama sina sound card?
Mastering mkuu haihitaji specific plugin, ni sikio na kujua weakness ya sound Yako then utaweza fanya levelling
 
Mkuu FL ina autosave na hii feature ipo kitambo sana, nimeitumia sana kurecord, mix na kumaster,
Na ukija kwenye uwezo hebu nikuulize, utarun kontakt 5+ kwenye PC ya 512MB au unafanya masiala.

FL ni very powerful software japo wengine hutumia kupiga instrument lakini hata sound recording, mixing and mastering ipo vizuri sana, na na recommend Kwa yeyote.

Ukija kwenye business
Hizi DAW unatakiwa kuzielewa karibia zote na uzuri wake zinatofautiana muonekano lakini vitu ni vile vile, ni rahisi kushift mfano kutoka FL kwenda Pro Tools kuliko kutoka Maya kwenda Zbrush Kwa watu wa modelling.

Kwenye biashara ukizielewa zote inakupa uwanja mpana sana mana unaweza Kuta studio hawatumii FL na wewe umeizoea FL so utashindwa kupewa session.

Kwahiyo FL, Logic, ProTools, Studio One, Ableton na Cubase unatakiwa kuzielewa zote kwenye industry.
 
Nimejaribu kuikimbilia Ableton V9, nimetokwa damu aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…