Tujifunze ya ndege: Hiki ndicho Kisanduku cheusi (black box) cha mawasiliano kila ndege ipatapo hitilafu au kuanguka huwa kinakitafuta

Tujifunze ya ndege: Hiki ndicho Kisanduku cheusi (black box) cha mawasiliano kila ndege ipatapo hitilafu au kuanguka huwa kinakitafuta

Aisee we jamaaa huwa sikosi kusoma post zako leo umenipa chakula ya ubongo na yule gentacimnie sijui aje aone GT kama ww
 
Voyage Data Recorder au Black Box kwa kiswahili kinafahamika kama kisanduku cha kuhifadhi taarifa za safari katika meli.

Hiki hukusanya taarifa zote kuanzia mazungumzo ya sehemu ya kuongozea na sehemu ya injini, chati za kuonyesha njia, tarehe,sehemu,kina cha maji,uelekeo wa meli,mzunguko wa injini na spidi ya meli.

UFANYAJI KAZI WAKE
Ufanyaji wake kazi inakusanya hizo taarifa mbalimbali na kuzitunza kwa masaa 12 mpaka 48 kabla ya ajali kutokea na zinaweza zikachezwa kama audio ili mamlaka au mmiliki kufanya uchunguzi wa ajali.

Pia baada ya kurekodiwa taarifa za siku 30 huifadhiwa kwenye memory card iliyopo katika VDR.

Namna kinavyofanya kazi endapo ajali imetokea, hiki kifaa kinatunzwa ndani ya kasha la plastic. Endapo meli imezama hiki kifaa kikutana na presha ya maji kitajifungua chenyewe na Kubaki sehemu ya ndani ambayo itaelea na kusambaza taarifa kwa meli na ndege zilizo karibu na eneo la tukio.

UBORA NA UIMARA
Black Box ya meli imekuwa bora kuzidi ya kwenye ndege kwa sababu inakusanya taarifa nyingi zaidi na inaweza kuplay taarifa za masaa zaidi ya 12 kabla ya ajali.

Uimara wake hiki kifaa hakiwezi kuungua kwenye moto, kuharibika na maji au kugongwa na kitu kizito.

MELI ZINAZOTAKIWA KUWEKEWA VDR
Mamlaka inayosimamia usafiri wa bahari ulimwenguni (IMO) kupitia sheria ya usalama wa watu na mali baharini (Safety of life at Sea Convection-SOLAS) kila meli iliyojengwa kuanzia mwezi wa 1,mwaka 2002.

UMUHIMU
Kifaa hiki kinasaidia kupatikana kwa taarifa muhimu za meli kipindi cha uchunguzi wa ajali. Mamlaka za usimamizi na wachunguzi huandaa ripoti za ajali na kuweka mipango ya kuzuia ajali kama iliyotokea.

AMI_Float_Free_Capsule.png
 
Kwa muda mrefu nimesikia na kuamini kwamba kuna kijisanduku kidogo ambacho hakiharibiki na hutunza kumbukumbu zote za kilichoendelea ndani ya ndege kabla ya kupata ajali.

Hivi idea ya kutengeneza haka kajisanduku ambako ni imara na hakawezi bomoka kwa nini isitumike kutengenezea ndege ambayo hata ikianguka haiwezi kubomoka watu wakatoka salama
 
Mkuu sio kwamba hilo box haliharibiki ila huwekwa sehemu salama zaidi ambapo ni vigumu kupata uharibifu mkubwa. Huwa linawekwa nyuma kabisa ya ndege.

Pia huwa sio jeusi siku hizi ni la orange ili kurahisisha upatikanaje wake pale ndege inapoanguka
 
Kwanza haitapaa,maana itakuwa nzito kupita kiasi. Pili itatumia nyenzo ngumu ambazo ni ghali pia(vyuma).
 
MKUU SIO KWAMBA HILO BOX HALIHARIBIKI ILA HUWEKWA SEHEMU SALAMA ZAIDI AMBAPO NI VIGUMU KUPATA UHARIBIFU MKUBWA. HUWA LINAWEKWA NYUMA KABISA YA NDEGE.
PIA HUWA SIO JEUSI SIKU HIZI NI LA ORANGE ILI KURAHISISHA UPATIKANAJE WAKE PALE NDEGE INAPOANGUKA

Asante kwa kunijuza
 
Hakika, hivi vifungwe na kwenye usafiri wa umma. Kwani bado bei yake ni 130 Millioni? Haijashuka?

Okay hata kama hatutaweka vya kiwangi hicho basi hata kamera na video tu vitatosha
 
Vipindi vya aircraft investigation huonyesha. Azam na DStv.azam jioni saa Moja kifurushi Cha 35k.jarabu unanishukuru
 
Back
Top Bottom