Tujihadhari na watu wanafiki, wanaohubiri amani lakini ni vinara wa Kuua Amani

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Amani haipotei kwa siku tendo la siku moja bali ni malimbikizo ya mambo mengi kwa muda mrefu.

Siku zote, wananchi wa kawaida huwa siyo wasababishi wa kupotea kwa amani. Kila mahali ambapo amani ilipotea, wasababishi wakubwa huwa ni watawala au watawala waliofarakana. Ni vigumu sana mwananchi ambaye hana chochote, hana bunduki, hana bomu, hana mzinga wala kifaru kusababisha amani ya nchi kutoweka. Wananchi huwa ni responders wa amani iliyoharibiwa na wenye nguvu.

Jiulize katika hali ya kawaida kabisa:

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, akiwa na wenzake watatu, wapo kwenye gari, wanaelekea mahakamani, wanahatarisha nini, na kwa nani? Halafu unawakamata, unawapiga, unawaumiza na kuwatupa porini! Hapa anayeharibu amani ya nchi ni nani? Yanapofanyika haya, kuna yeyote anaweza kusimama kwa ujasiri na kunena kuwa Tanzania kuna amani?

Fikiria mwandishi wa habari anataka kuingia kwenye ukumbi wa mahakama, ili apate habari na auhabarishe umma kwa usahihi, anazuiwa kuingia, anapigwa na kusukumizwa kwenye gari la polisi kupelekwa kusikojulikana. Hivi huyu mwandishi wa habari kuingia kwake mahakamani kulikuwa kunahatarisha nini? Kwa mazingira hayo utasema polisi wapo kwaajili ya kutunza na kulinda amani ya nchi au wapo kwaajili ya kuharibu amani ya nchi? Bado kwa mazingira hayo, utaendelea kusema Tanzania kuna amani?

Tunapewa taarifa, baadhi ya viongozi wa CHADEMA waliokuwa wanaelekea mahakamani kusikiliza kesi ya kiongozi wao, wamepigwa, wamevunjwa miguu na mikono, na mmoja inasemekana ameuawa. Hawa watu kwenda kusikiliza kesi ya kiongozi wao, wametenda kosa gani? Tujiulize, hivi ikitokea Samia, mwenyekiti wa CCM akashitakiwa kwenye mahakama ya The Hague, viongozi wa CCM hawataenda kusikiliza kesi dhidi ya mwenyekiti wao? Na kama wakienda, watachukuliwa kuwa ni wahalifu ambao adhabu yao ni kuvunjwa miguu na mikono au hata kuuawa?

RAI
Tamaa ya madaraka isitufanye kukosa akili, utu, na hekima, kiasi cha kuona kuwa ukiwa na madaraka, basi watu wengine wote siyo binadamu, na wewe mwenye mamlaka unaweza kuwafanya chochote, ikiwa ni pamoja na kuamua nani aishi, nani afe, nani awe kilema na nani afurahie mema ya nchi.

Ubinadamu wetu ni jambo muhimu kuliko chochote. Uwe Rais, uwe polisi, uwe IGP au Waziri au RC, wewe bado ni mwanadamu. Kama hutaki kuamini kuwa wewe bado ni mwanadamu, Mungu atakuonesha, atakudhihirishia kuwa wewe ni mwanadamu, uliyezaliwa kama mwingine yeyote, utakayeugua kama mwingine yeyote, na utakayekufa kama mwingine yeyote.

Watawala waombe hekima ya Mungu, la sivyo wanajitafutia laana.
 
Mungu ikikupendeza fanya tena haukutuacha kipindi kile naamini hautatuacha kipindi hiki kwakua unalipenda Taifa hili tunakukabidhi hawa watu ushighulike nao namna inayofaa
 
Amina.
Hakika Mungu wetu tunaujua ukuu wako. Siku zote ulinzi wa anayeonewa upo mikononi Mwako.

Kila mtu leo aombe ukuu wa Mungu uwafikie watawala wanaodhulumu binadamu wenzao, kwa namna ile ambayo YEYE anaona yafaa.

Mama Bikra Mkingiwa dhambi ya asili, ambaye Taifa liliwekwa kwenye ulinzi wa maombezi yako, tunaomba uyafikishe maombi yetu kwa mwanao, aliye Bwana wetu, yeye ambaye alituachia amani, lakini watawala wameiondoa amani katika mioyo ya watu wanaowatawala.
 
Nikuibie siri tanzania hakuna mwananchi mpumbavu wa kwenda kupambana na dola kwa matumbo ya wengine watu waliumizwa mwisho wa siku waliunga juhudi na mafisadi wakawa wagombea uraisi wa upinzani rejea lowassa na membe...
 
Amani haipotei kwa siku tendo la siku moja bali ni malimbikizo ya mambo mengi kwa muda mrefu.

Siku zote, wananchi wa kawaida huwa siyo wasababishi wa kupotea kwa amani. Kila mahali ambapo amani ilipotea, wasababishi wakubwa huwa ni watawala au watawala waliofarakana. Ni vigumu sana mwananchi ambaye hana chochote, hana bunduki, hana bomu, hana mzinga wala kifaru kusababisha amani ya nchi kutoweka. Wananchi huwa ni responders wa amani iliyoharibiwa na wenye nguvu.

Jiulize katika hali ya kawaida kabisa:

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, akiwa na wenzake watatu, wapo kwenye gari, wanaelekea mahakamani, wanahatarisha nini, na kwa nani? Halafu unawakamata, unawapiga, unawaumiza na kuwatupa porini! Hapa anayeharibu amani ya nchi ni nani? Yanapofanyika haya, kuna yeyote anaweza kusimama kwa ujasiri na kunena kuwa Tanzania kuna amani?

Fikiria mwandishi wa habari anataka kuingia kwenye ukumbi wa mahakama, ili apate habari na auhabarishe umma kwa usahihi, anazuiwa kuingia, anapigwa na kusukumizwa kwenye gari la polisi kupelekwa kusikojulikana. Hivi huyu mwandishi wa habari kuingia kwake mahakamani kulikuwa kunahatarisha nini? Kwa mazingira hayo utasema polisi wapo kwaajili ya kutunza na kulinda amani ya nchi au wapo kwaajili ya kuharibu amani ya nchi? Bado kwa mazingira hayo, utaendelea kusema Tanzania kuna amani?

Tunapewa taarifa, baadhi ya viongozi wa CHADEMA waliokuwa wanaelekea mahakamani kusikiliza kesi ya kiongozi wao, wamepigwa, wamevunjwa miguu na mikono, na mmoja inasemekana ameuawa. Hawa watu kwenda kusikiliza kesi ya kiongozi wao, wametenda kosa gani? Tujiulize, hivi ikitokea Samia, mwenyekiti wa CCM akashitakiwa kwenye mahakama ya The Hague, viongozi wa CCM hawataenda kusikiliza kesi dhidi ya mwenyekiti wao? Na kama wakienda, watachukuliwa kuwa ni wahalifu ambao adhabu yao ni kuvunjwa miguu na mikono au hata kuuawa?

RAI
Tamaa ya madaraka isitufanye kukosa akili, utu, na hekima, kiasi cha kuona kuwa ukiwa na madaraka, basi watu wengine wote siyo binadamu, na wewe mwenye mamlaka unaweza kuwafanya chochote, ikiwa ni pamoja na kuamua nani aishi, nani afe, nani awe kilema na nani afurahie mema ya nchi.

Ubinadamu wetu ni jambo muhimu kuliko chochote. Uwe Rais, uwe polisi, uwe IGP au Waziri au RC, wewe bado ni mwanadamu. Kama hutaki kuamini kuwa wewe bado ni mwanadamu, Mungu atakuonesha, atakudhihirishia kuwa wewe ni mwanadamu, uliyezaliwa kama mwingine yeyote, utakayeugua kama mwingine yeyote, na utakayekufa kama mwingine yeyote.

Watawala waombe hekima ya Mungu, la sivyo wanajitafutia laana.
Ajabu, halafu wanasifiana na kujifanya wanabeba maono wakati wanabeba maovu na ukumbaff
 
Back
Top Bottom