SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Mainjinia waliochora na kuujenga uwanja wa Ben Mkapa walijenga uwanja huo kwa uwezo wa kuchukua uwezo siyo tu wa idadi ya mashabiki wanaotajwa wa 60,000 lakini pia makadirio ya uzito fulani.
Ni kawaida kwenye mechi kubwa, mfano kama shughuli ya jana ya Simba Day kwa watu kuingizwa kuzidi idadi hii iliyowekwa kwa uwanja huu. Inasemekana uwanja ulijaa hadi wenye tiketi wengine hawakuruhusiwa kuingia. Kwenye siti, watu wanakaa wawili wawili, bado wale wengine wanaojaa kwenye ngazi. Nimejaribu kupiga mahesabu ya haraka, tuchukulie wazidi watu 2,000 tu (na idadi hii huwa ni kubwa kuzidi hii), wastani wa uzito wa mtu mmoja ni 60 kg, kwa watu hao 2,000 tunaongelea zimezidisha tani 120. Mimi sina utaalamu sana kwenye masuala ya civil engineering au building engineering ila nadhani hili lina madhara kwenye structure nzima ya yale majengo.
Nchi hii imepitia majanga mengi hasa ya meli, maarufu ni MV Bukoba ambayo vyanzo vyake mara nyingi vimesemekana ni kujaza watu na mizigo kuzidi uwezo. Maafa haya yanapotokea, tunafunika kombe maisha yanaendelea, hatujifunzi tunarudia makosa yale yale.
Sijajua lifespan ya huu uwanja ila kuna miaka inabidi ipunguzwe katika lifespan yake kutokana na matumizi mabaya kama haya.