Tujikumbushe Big Dogg Pose (BDP Kamili)

Mwanzoni penzi letu lilipamba moto,
Kupeana ulimi, kama na mama wake mtoto,
Mabusu kede wa kede kila mahali, ulkuwa upande wangu wa kushoto, na kwenye mahaba nilikubali kweli we' moto.
Hukusita, kunishika, kuashiria...

Enzi hizo "rudi mpenzi" na "kitambo kidogo" nilizihifadhi kichwani zote...

Mwenye nazo atuwekee hapa wanakwetu. Hasa "kitambo kidogo" ni kama "kamanda" ya daz nundaz...
 
"wanagwaya gwaya wamekanyaga miwaya"

nakumbuka mashairi kama hayo ya BDP ila sikumbuki wimbo uliitwaje
huo unaitwa YAMENIKUTA sio wa BDP ni wimbo wa wale jamaa wa tmk ya zamani wakina KR,KULWA,juma nature kipindi iko hajulikani...wale walioimba kamua.
 
ha ha ha we kweli wa zaman afu daz nundaz walitohoa kamanda toka kitambo kidogo
 
Hawa jamaa walikuwa hatari
 
Hao ni GWM kina KR wimbo unaitwa Yamenikuta wakimshirikisha II Proud aka Sugu kwa sasa na si BDP.
Yamenikuta mzee mwenzangu
Sina changu
Wanga wengi anga zangu
Kiama chao ama changu
Ukiishi kwa upanga
Utakufa kwa upanga
Walimwengu wana mambo
Watakusemasema kwa kila jambo
Hawakai kukupakazia
Flan ana HIV
Wanapakaza hivi hivi
Ukirudi kwenye mitaa
Ndio balaa
Polisi wanakughasi
Wanatamani watumalize kwa risasi
Kucheka nataka
Kulia nataka
 
Walishirikishwa ngoma moja Kali sana ya Mr. II Sugu na lady JayDee "Mud a Mrefu". Mwenye huo wimbo naomba aniwekee.

Jinsi ya ku-upload ndio utata ila ingia kwa jamaa wanaitwa 'Zilipendwa zaidi' utapata joints nyingi sana za kizazi chetu,mimi muziki libraly yangu ina hizo ngoma kibao za zamani.
 
Jinsi ya ku-upload ndio utata ila ingia kwa jamaa wanaitwa 'Zilipendwa zaidi' utapata joints nyingi sana za kizazi chetu,mimi muziki libraly yangu ina hizo ngoma kibao za zamani.
Ngoja niutembelee
 
Hii hapana! Hawa GWM kama sijakosea!
Hii verse aliimba Sugu baada ya kushirikishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…