....natumia akili mingi sana kuvuta kumbukumbu ya Solid Ground Family kwenye jukwaa moja la Yo!Rap Bonanza na Da Young Mobb,
..ila haiji mzazi!
....Da Young Mobb ni kabla/sambamba na Sugu ujue mzazi
Ukisema Dar Young Mob ni kabla, sambamba na Sugu unajionesha huijui Dar Young Mob wala Sugu.
Too Proud (siyo Sugu wala Mr II enzi hizo) alikuwa member wa Dar Young Mob, hapo katoka Mbeya. Dar Young Mob ilianzishwa na washkaji wawili, Too Proud akakaribishwa alivyokuja Dar kutoka Mbeya.
Baadaye ndiyo akaenda solo na kujiita Mr. II na badaye Sugu.
Mr. II mimi nisharekodi naye Don Bosco, ila sitaenda kwenye details for reasons of anonimity.
Yo! Rap Bonanza haikufanyika mwaka mmoja, imefanyika tangu Too Proud yupo Dar Young Mob mpaka alivyoenda solo.
Na kila mwaka mtiririko wake ulikuwa kama ligi ya mtoano, inaweza kwenda awamu tatu au nne. Mpaka wakina No Name walishiriki, ilikuwa unajiandikisha tu, kama ma judge wanaona huna uwezo wanakutoa mapema tu, kwa hiyo kusema fulani hajashiriki kwa maana ya kwamba hilo ni jukwaa kubwa sana nakuona huelewi Yo! Rap Bonanza ilivyokuwa inaenda.
Mi najua kwa sababu nishashiriki, kuna wiki tulianza, halafu kuna wiki iliyofuatia nilikuwa na mitikasi sikuweza kwenda nikafikiri tutatolewa machizi wakapetesha jahazi.
Tushazunguka sana na marehemu Kim Mgomelo kwao pale Billicanas kwa nyuma, kuandaa instrumentals etc kwa ajili ya Yo! Rap Bonanza. Kim was super nice, yani jamaa alikuwa na savoir faire fulani hivi watoto wa Dar walikuwa wanaita "zungu la roho".
Yani Kim unaweza kumuambia unataka mabadiliko fulani madogo tu kwenye show, kama ikiwezekana, isipowezekana poa tu, lakini yeye atahangaika kichizi kufanikisha, ukimwambia Kim kama ni kazi kubwa potezea tu, anakataa katakata, anakwambia we must get this done right. Nilijifunza sana kutafuta kuifanya kazi vizuri kupitia kwake.
Naandika vitu nilivyoishi, enzi za Live With Purpose, Fun With Sense, Unique Sisters, Weusi Wagumu Asilia, all the way back into Raiders Posse na Kwanza Unit.
Si vitu nimesoma kwenye magazeti na kuhadithiwa au kwenda kwenye concert kuangalia, hawa watu nimeishi nao, tumekutana sana studios za Don Bosco kwa Marlon, Temeke kwa Enrico, Masaki kwa P Funk, Oysterbay kwa Master J.