Tujikumbushe: Lissu ni Mshindi

Naona uzi huu umejaa sifa kedekede kwa Lissu, lakini kwa maoni ya watanzania wazalendo Lissu ni msaliti mkubwa kwa nchi yake.

Lissu ni mwanasiasa aliyekuwa tayari nchi itengwe kimataifa na kunyimwa misaada ya aina yoyote ili kulipiza kisasi kwa mtu mmoja tu Magufuli. Lissu alitamani nchi hii iwe Kama Zimbabwe kipindi cha Mugabe ili roho yake ifurahi kuwa kamkomesha Magufuli. Anasahau watanzania wengi ni maskini na namna gani wangepitia mateso makubwa ya kiuchumi Kama yangetokea hayo aliyotamani yawe.

Katika harakati za Magufuli kupambana na mabeberu kuhusu mikataba ya madini, Lissu alionyesha dhahiri ni namna gani asivyokuwa mzalendo na nchi yake kwa kuwa mtetezi wa kampuni ya ACCACIA na kutishia kuwa serikali ingeshitakiwa MIGA kama ingeedelea kufuatilia mikataba iliyopo.

Lissu asivyokuwa mzalendo alishirikiana na wafanyabiashara mbali mbali waliokuwa na mgogoro na serikali ili ndege za Air Tanzania zikamatwe, matokeo yake mojawapo ya ndege yetu ilizuiliwa Afrika kusini hadi zilipofanyika jitihada za wanasheria wazalendo kupeleka utetezi ktk mahakama ya Afrika kusini ndo ndege yetu ikaachiliwa.

Kitendo cha Lissu kupigwa risasi kibinadamu siyo kitendo kizuri, na Lissu amejaribu kutumia turufu hiyo Kama ajenda ya kiasiasa ingawa haikumsaidia katika uchaguzi wa 2020, kwani hata alipoitisha maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi hakuna Mtanzania aliyejitokeza kwenye maandamano hayo.

Kwa kukimbia aibu hii Lissu akaamua kukimbilia Ubelgiji kwa kisingizio cha kutishiwa usalama wake licha ya kwamba alifanya kampeni za uchaguzi kwa zaidi ya miezi 2 bila hofu yoyote ya usalama.

Kwa ujumla Lissu hana mvuto wowote kwa siasa za Tanzania, Chadema wasirudie kumuweka tena huyu kama mgombea wao, nina Imani hata Lowasa wa leo ana mvuto kwa Watanzania kuliko alivyo Tundu Lissu.
 
Umeandika upumbavu mtupu!
 
Mkuu na wewe ni Expert Member!! Point zako haziendani na hoja za MADA, hapo ndipo penye ukakasi na uexpert.
 

Nchi ikifanya upumbavu ni Bora itengwe.
 
Huu uzi umeurudia kwa nini?

Nakumbuku uliuweka kipindi cha kampeni za uchaguzi 2020.

Ni kweli jamaa ni mshindi,naunga mkono hoja.
 
Lissu alipopona tu nikajua Magufuli hachomoi, lazima karma itamlamba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…