Tujikumbushe Mashairi tuliyoyapenda shule ya msingi

Nyumbani kwako kuzuri, japokuwa ni pangoni
Nyumba yako ni johari, ya mwenzako sitamani,
Hata pawe pa tajiri, hapafai maisha
Nyumbani kwako johari, kwingine usitamani.


Uipende nyumba yako, utaona raha yake, Kisha penda ndugu yako, kwako apaone kwake
Dunia mahangaiko, usipende pekepeke, Nyumbani kwako johari, kwingine usitamani.
 
Japo siku bahatika kulisoma lakini liko poa
 
Mm nayakumbuk ya olevel CHEKA CHEKA
 
Mimi panya ni mwepesi, hadi mnanidharau.
Vipi leo iwe kesi, mimi kuzamisha dau.
Dau kazamisha ng'ombe, ndipo likafanya pindu.
Kichwani ana mapembe, mgongoni ana nundu.

Kitambo sana
Mimi panya ni mwepesi, hadi mnanidharau.
Vipi leo iwe kesi, mimi kuzamisha dau.
Dau kazamisha ng'ombe, ndipo likafanya pindu.
Kichwani ana mapembe, mgongoni ana nundu.

Kitambo sana
Mkuu hili shairi kama unalikumbuka lote naomba ulimalizie aisee
 
aisee umenikumbusha mbali sana braza

nilipewa kipande hiki kukariri ili nije kuimba siku ya kufunga shule

tulikua std 5 mwaka 2000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…