Kwa msio jua meli ilipinduka ndio ikazama, yaani kichwa chini mi guu juu!!
Hii meli ilikuwa imejaza kupita kiasi na ilikuja upande upande toka bukoba!!
Na ijulikane meli ya victoria na iyo mv bukoba zina sehemu ya kukaa abiria chini kabisa wanaziitaga third class sasa ilipo binuka watu walikua wanagonga kitako cha meli wakiwa ndani ya meli kuomba msaada, ndipo wakaja na wazo watoboe kwenye kitako ili wawatoe kumbe ndio wanaizamisha!!
Izo third class ambazo ndio wengi ujazana huko zinatisha aisee, yaani meli ikiwa inaenda mnakuwa tayari mshazama kama ikotoboka chini, maji yanaanzia kwenu!! Kunakuwa na ngazi mnaingia huko chini kabisa aisee yaani hata kama meli ina kwangua chini mnaisikia!! Wameweka siti.