Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

Lakini vipi hakuna hata mmoja alienusurikaa labda kuwaambia nini kilitokea wenzake kupoteza maisha esp ile situation uwa tunaambiwa wanafunzi wa Rugambwa walikufa wameshikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes tulirudia mitihani kwa sababu ya awali ilizama katika meli. Katika darasa la watu 58 tulibaki 26. Tulirudi shule kabla hawajafungua likizo ya June. Kufanya mitihani ukiwa kwenye tension ya kupoteza wenzio na kwamba huna materials za kujisomea na wakati huo mko wachache sana shuleni ilikua changamoto lakini lilipita na maisha yanaendelea.
Samahani kukukumbusha yaliyopitaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini vipi hakuna hata mmoja alienusurikaa labda kuwaambia nini kilitokea wenzake kupoteza maisha esp ile situation uwa tunaambiwa wanafunzi wa Rugambwa walikufa wameshikana

Sent using Jamii Forums mobile app
Alinusurika mmoja aliepanda meli ile lakini alikua mbali na wenzetu kwaiyo si rahisi kujua kama ni kweli walishikana au la. Na katika wanafunzi wote watatu ndio walipatikana, mmoja alizikwa kwao na wawili walizikwa Igoma.
 
Kumbe uenda hii story uwa sio kwel au pengn ao watatu ndo walishkana wengn hapana, lakin katika simulizi za huyu mmoja alisema kilitokea nn mpk ajali kitokeaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe uenda hii story uwa sio kwel au pengn ao watatu ndo walishkana wengn hapana, lakin katika simulizi za huyu mmoja alisema kilitokea nn mpk ajali kitokeaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Meli ilikua imejaa sana abiria pamoja na mizigo. Walipokaribia gatini ikawa haibalance hivyo wafanyakazi wa melini wakawa wanajitahidi kubalance uzito wa watu on both sides ikawa ngumu ndio ilipoanza kuyumba hatimae ikapinduka
 
B
49084f27b80275392537b418022a96b5.jpg
f4604464002f7be1e1669c1df1b6359f.jpg
MV Bukoba ilikuwa moja ya meli kubwa katika ziwa Victoria. Ilikuwa ina uwezo wa kusafirisha watu zaidi ya 400 na tani zaidi ya 100.

Meli hii ilikuwa ikiondoka Bukoba siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Meli hii sio kongwe kama ilivyokuwa MV Victoria iliyojengwa mwaka 1961; hii ilijengwa mwaka 1979 lakini ilikuwa chini viwango na mbovu kuliko MV Victoria.

Meli iliua watu zaidi ya 800 siku ya Jumanne ya tarehe 21 ya mwezi wa tano mwaka 1996 eneo la Bwiru KM 30 kutoka bandari ya Mwanza.

Basi nawakaribisheni mwenye kujua chochote kuhusu meli hii au alishasafiri na meli hii au aliponea chupuchupu ajali atupe experience.

Karibuni
Bwiru to mwanza centre Ni kilometa 7 vp ziwe km 30? Au umetumia newtical mile? Basi coz umbali was majini wanatumia newtical mile convert to km mkuu
 
Yes tulirudia mitihani kwa sababu ya awali ilizama katika meli. Katika darasa la watu 58 tulibaki 26. Tulirudi shule kabla hawajafungua likizo ya June. Kufanya mitihani ukiwa kwenye tension ya kupoteza wenzio na kwamba huna materials za kujisomea na wakati huo mko wachache sana shuleni ilikua changamoto lakini lilipita na maisha yanaendelea.
Poleni sana kwa kushuhudia tukio la hatari.
 
Mv bukoba kuna kipindi miaka ya tisini mwanzoni ilikuwa inaenda musoma pia,tukiwa wadogo tuliipanda,nakumbuka kwenye meli walikuwa wanakataa watoto wachanga kulia eti itazama,sifa nyingine ilikuwa inasafiri kiupande upande kama imeelemea upande mmoja!

Siku inazama pale shule ya nyanza primary mapema tulipata taarifa,sie tuliokuwa tunakaa nera kando ya ziwa,kuna muda miili ilikuwa unaikuta ufukweni mwa ziwa ukienda kupiga mswaki "bichi"
Ilikuwa hatari sana tulimpoteza mwanafunzi mwenzetu wa nyanza ali mwarabu na familia yake wakitoka harusini,pia imam wa kwanza wa masjid al asais makongoro nae mauti yalimkuta humo!
Mkuu hiyo ya maiti kuelea ufukweni maeneo ya nera tena ukienda kupiga mswaki ni chai tena ile ya kuwaua virus wa corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kiliniuma sana wale wanafunzi wasichana wa Rugabwa waliokuwa wamemaliza kidato cha sita wote waliteketea; walivyoona sasa wanakufa walishikana wote kuagana kwa safari ya milele - too sad.

Hii ajali ilimtwaa Dada yangu akitoka kumaliza mitihani yake ya FVI hapo Rugambwa Secondary
 
Nakumbuka hii siku ilikuwa jumatano kama sikosei nikiwa darasa la Pili, nikiwa tayari nimeshajiandaa kwenda shule mida ya saa nne asubuhi ndipo niliposikia habari Mvunjiko kutoka Radio Free Africa, nikamuita dada angu aje asikilize.

Hakuweza kuvumilia, akapiga ukunga, watu wakaja kujua nini kimetokea, mmoja wa waliokuja alikuwa ni mke wa mwalimu wetu wa tuition alikuwa ni mhaya. Kumbe yule mama alikuwa anamsubiri mgeni wake kutoka Bukoba na alikuwa ndani ya ile meli. Yule mama alipagawa, wala hata hakufunga ofisi yake akakimbia kwenda Custom. Tuliokuwa Mwanza kipindi hiko tunajua namna mji ulivyozizima kwa Majonzi kipindi kile
 
Hahahaa inawezekana mie nimesoma nyanza from 1992-1997.na nilikuwa nakaa kona ya Nera opposite na hospital ya dr chogo,karibu na kiwanda cha pipi karanga ziwani kabisa pale!
We jamaa umesoma nyanza na umekaa nera?!!the same to me

96 ulikua darasa la ngapi kama la pili itakua we ni classmate wangu tena from the same neighborhood!!!

Nakumbuka tulikua tunakaa kwenye kile kimlima juu(nera)kinachoangalia ziwani kuangalia zoez la uokoaji coz shule ilifungwa due to huo msiba wa kitaifa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui watanzania tuna tatizo gani na kuoverweight hata kwenye gar imeandikwa tan moja gar inabeba tan na nusu siti za watu wa tano tunakaa 9
Siyo tatizo la wwatanzania tu ...ni kote duniani hasa kwa nchi zinazoenddelea
 
49084f27b80275392537b418022a96b5.jpg
f4604464002f7be1e1669c1df1b6359f.jpg
MV Bukoba ilikuwa moja ya meli kubwa katika ziwa Victoria. Ilikuwa ina uwezo wa kusafirisha watu zaidi ya 400 na tani zaidi ya 100.

Meli hii ilikuwa ikiondoka Bukoba siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Meli hii sio kongwe kama ilivyokuwa MV Victoria iliyojengwa mwaka 1961; hii ilijengwa mwaka 1979 lakini ilikuwa chini viwango na mbovu kuliko MV Victoria.

Meli iliua watu zaidi ya 800 siku ya Jumanne ya tarehe 21 ya mwezi wa tano mwaka 1996 eneo la Bwiru KM 30 kutoka bandari ya Mwanza.

Basi nawakaribisheni mwenye kujua chochote kuhusu meli hii au alishasafiri na meli hii au aliponea chupuchupu ajali atupe experience.

Karibuni
Umeleta mada ya maana Sana...hongera
 
Back
Top Bottom