Tujikumbushe: Series hii ya udogoni "journey to the west"

Tujikumbushe: Series hii ya udogoni "journey to the west"

Hivi ITV imekuwaje jamni siku hizi kutwa mikutano ya chama
itv ilikuwa zamani siku hizi utopolo mtupu....

kipindi hicho acapulco, the bold and the beautiful, mzee ojwangi, tausi, mambo hayo, shivo, star wars ya katuni na baadaye wakaleta zile series.... kipindi hicho katuni zao hazikuwa nzuri wanaweka akina Mario siku wakifurahi ndo wanakuwekeeni Batman hahaaaaa
yaani tulikuwa na ratiba zote za vipindi vya Televisions....kunazia CTN majuto na Chekibud.....DTV mzee Small....baadaye ikaja TVT wao movie saa 4 usiku jumapili.....nakumbuka ITV kila tarehe 31 Dec lazima waweke movie kali wazee ilikuwa kupiga mabati kidogo movie ndo saan usiku huo watu wote wapo nje hahaaaaaaaaaaaaaa

Baadaye zikaja kupoteza mvuto zote ikaibuka EATV....movie kali jumapili....siku hizi DSTV na Azam mambo kuchele but old is gold hahaaaaa
 
Hahaha eti kima
nilikuwa natizama tuuu ili mradi...halafu watoto wengi tulikuwa hatuilewi kiviiiile ingawa ilikuwa na subtitle km sikosei sema tulipenda zile pigana pigana mara wanabadilika badilika....anaweza akawa boga hahaaaa mi niliona uzushi nikaona bora Rino Lenzi ( Mapikipiki na SunSet Beach huku naombea saa nne usiku ifike haraka niangalie Days of lives hahaaaaaa.......
 
Halafu jumamosi usiku wakawa wanaonesha mieleka aseeh
 
nilikuwa natizama tuuu ili mradi...halafu watoto wengi tulikuwa hatuilewi kiviiiile ingawa ilikuwa na subtitle km sikosei sema tulipenda zile pigana pigana mara wanabadilika badilika....anaweza akawa boga hahaaaa mi niliona uzushi nikaona bora Rino Lenzi ( Mapikipiki na SunSet Beach huku naombea saa nne usiku ifike haraka niangalie Days of lives hahaaaaaa.......
Yeah kweli ila kwa sasa tukijikumbusha ndo unapata utamu halisi kabisa.
Ila season ya 3 na ya 4 wameharibu sana japo ndo final hizo
 
Yah kipindi hicho usimpomjua Hulk Hogan huna cha kuhadithia jumatatu shule hivyo lazima utazame mieleka ili upate wa kukusikiliza
Hahaha nilikuwa primary that time japo sio mkongwe sana lakini nami nami nimefaidi mema ya zamani
 
Mkuu
Kwa wale wa kishua tuwaite kipindi hicho ITV walikuwa wanaicheki hii series journey to the west ..

Ilikuwa maarufu hii ilikuwa ni story ya kichina inayomuhusu master mmoja jina lake aliitwa Chen..ama sisi tulimuita "shivo"..
Mtu huyu alikuwa ni mtoto ambaye alitelekezwa kwa kuwekwa kwenye kitenga majini .na hatimaye mwalimu mmoja wa kibudha na mmiliki wa temple akamuokota na kumlea kwa misingi ya dini yao hiyo ya budha .

Mtoto akakua na akawa lecture ama tu muhubiri wa scripture hizo za kibudha

Hatimaye avalokitesvala " god of mercy" anashuka chini duniani kutafuta mtu mmoja msafi wa roho na mfuatiaji mzuri wa scripture za Buddha ili amtume safari ya mbali kwenda huko west kufata scripture ili baadae aje kuisambaza hiyo scripture (mahubiri) dunia nzima ijae watu wema

Lakini master huyu mdogo hana uwezo wa kupambana na monsters walioko huko njiani ni wengi na safari ni ndefu ilichukua takribani miaka 25 njiani.

Hatimaye anapatiwa walinzi watakaomlinda wakati wa safari ,kumtafutia chakula.

Mlinzi wa kwanza alikuwa ni monkey king jina lake halisi ni "wu Kong".

Huyu alizaliwa kwenye jiwe Na akafundishwa na master mmoja wa ki taoist ambapo akapewa transformation 72 za kujibadilisha .

Aliwahi kupewa kazi huko mawinguni ya kutunza farasi na akaacha na kuona ni dharau .
Kisha akala matunda ya bustane ya mfalme (immortal) ukila matunda hayo utaishi milele .tunda moja miaka 500 mengine miaka 1000

Alivuruga sana palace ya mfalme ( jade emperor)

Na wanajeshi wote angani walimshindwa ndipo tatagatha Buddha mkuu mwenyewe alipomdhibiti na kumfunga kwenye mawe chini na akasubiri kwa miaka 500 ndipo master yule apite hapo kuelekea safari yake ya kuelekea west .kuja hapo kusoma karatasi juu na kumtoa ..safari inaanza.

Mlinzi wa pili huyu ni Marshal tiang ama Piggie kama tunavyomuita.

Ana transformation 32 tofauti.

Alitupwa duniani baada ya kulewa kulipokuwa na sherehe huko mawinguni na yeye kama official akamtamani mke wa mfalme na kutupwa duniani akatokea ndani ya tumbo la nguruwe.

Udhaifu wake ni ulafi sana anaweza kula hata Mara 60 kwa siku.

Anapenda warembo.

Wa mwisho ni sha wuneng huyu alikuwa monster wa mto mmoja na akawa nae ni moja ya walinzi wa tsuang tsang ama master. Shivo

Inaaminika nyama ya huyu shivo ni atayeila atakuwa immortal ,ataishi milele..

Hii inafnya changamoto iwe kubwa njiani kwani kila monster anataka kuila.

Master huyu pia ana sifa ya ubishi japo ni kipanga kweli kweli ana uwezo wa kusoma vitabu 60 na kuvikariri vyote hapo hapo...!
Mkuu hongera sana unajua kusimulia mpka nn maana umenikumbusha sun wukong na bajjie safi sana mkuuu.
 
Back
Top Bottom