Tujikumbushe: Series hii ya udogoni "journey to the west"

Hivi ITV imekuwaje jamni siku hizi kutwa mikutano ya chama
itv ilikuwa zamani siku hizi utopolo mtupu....

kipindi hicho acapulco, the bold and the beautiful, mzee ojwangi, tausi, mambo hayo, shivo, star wars ya katuni na baadaye wakaleta zile series.... kipindi hicho katuni zao hazikuwa nzuri wanaweka akina Mario siku wakifurahi ndo wanakuwekeeni Batman hahaaaaa
yaani tulikuwa na ratiba zote za vipindi vya Televisions....kunazia CTN majuto na Chekibud.....DTV mzee Small....baadaye ikaja TVT wao movie saa 4 usiku jumapili.....nakumbuka ITV kila tarehe 31 Dec lazima waweke movie kali wazee ilikuwa kupiga mabati kidogo movie ndo saan usiku huo watu wote wapo nje hahaaaaaaaaaaaaaa

Baadaye zikaja kupoteza mvuto zote ikaibuka EATV....movie kali jumapili....siku hizi DSTV na Azam mambo kuchele but old is gold hahaaaaa
 
Hahaha eti kima
nilikuwa natizama tuuu ili mradi...halafu watoto wengi tulikuwa hatuilewi kiviiiile ingawa ilikuwa na subtitle km sikosei sema tulipenda zile pigana pigana mara wanabadilika badilika....anaweza akawa boga hahaaaa mi niliona uzushi nikaona bora Rino Lenzi ( Mapikipiki na SunSet Beach huku naombea saa nne usiku ifike haraka niangalie Days of lives hahaaaaaa.......
 
Halafu jumamosi usiku wakawa wanaonesha mieleka aseeh
 
Yeah kweli ila kwa sasa tukijikumbusha ndo unapata utamu halisi kabisa.
Ila season ya 3 na ya 4 wameharibu sana japo ndo final hizo
 
Yah kipindi hicho usimpomjua Hulk Hogan huna cha kuhadithia jumatatu shule hivyo lazima utazame mieleka ili upate wa kukusikiliza
Hahaha nilikuwa primary that time japo sio mkongwe sana lakini nami nami nimefaidi mema ya zamani
 
Mkuu Mkuu hongera sana unajua kusimulia mpka nn maana umenikumbusha sun wukong na bajjie safi sana mkuuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…