Tujikumbushe vya zamani kidogo, vimepotelea wapi hivi?

Tujikumbushe vya zamani kidogo, vimepotelea wapi hivi?

kuna hili songi nimekumbuka

Mungu mkubwa, bwa bwabwa na samaki, ki king majuto, to tone la maji, ji jitu la kale, le lenye midevu, vu vumbua dhahabu........Nimesahau linaendeleaje

Hahaha mama wa kambo, mbo mbona wanitesa, sa sasa naondoka, ka kaa peke yako, ko koma kunipiga, ga gari la jeshi, shi shingo ya mtu, tu tundu la nyoka, ka karibu na wewe, we wembe wa kucha, cha chakula kitamu, mu Mungu mkubwa.....
 
Bu bubu wa semii....mi mimi mdogo.......go gogo la mti ti tina na mjuba..ba...

Nmekumbuka enzi zile kitu ya kombolelaaaa...

Banda umizaaa.....dj afro...
Pale moro, mafiga..real miss

Eeeh ulikaa mafiga kaka mtumishi, mwee usikute ushawahi kuniona dada ako enzi zangu za usichana kwenda shule na kidumu na ufagio teh
 
Mkuu ongeza na "makida makida" sana mabinti walipenda sn huu mchezo na ulivuma sn kitambo iko...walikuwa wakiruka kwa kutumia mpira mwembamba wa manati km sikoseiBila kusahau 'bilingeba yoyo bilingeba yo..tunamuomba talentboy atuoneshe maringo yke bingilibingili mpaka chini"...,...aisee!Ila mkuu hii si ilibidi uipelleke kule 'chit chat' hii.

Daah nimesmile peke angu. Umenikumbusha mbali mnooo
 
kuna ule wimbo wa mama kapika ugali na mfinyango wa nyama ya dede ya dede yaaaa! na ule katoka shamban na mkungu wa ndizi, kipindi hicho shule mnasoma kitabu cha hawafu mwenye nguvu, mkicheza football unavaa kiatu mguu m1 kingine unampa mwingine.
 
Eeeh ulikaa mafiga kaka mtumishi, mwee usikute ushawahi kuniona dada ako enzi zangu za usichana kwenda shule na kidumu na ufagio teh

Dada mtumishi pale kulikuwaga na ligi ya chadimu kati ya sobibo na timu gan sijui uwanja wa mafiga ps..kombe ni wale wadudu wanaitwa pimbi, pia wale wengine wanaitwa 'siri'

Tena tulicheza komborelaaaa.....
Nmekumbuka tuu jinsi ulivyokuwa unapenda kubadilishana nguo....
 
1.Kibaba baba na kimama mama hehhehehehhe
2. Mdako
3. Tulikuwa na yale madoli basi tunapishana tu kuyafanyia birthday party. Tunajipikilishaje
4. Ukuti Ukuti, wameme wameme

Afu kulikuwa na ice cream za vijiti a.k.a ice cream za uchoyo.
 
  • Thanks
Reactions: Art

Hahhahaha hatari kabisa.
 
Bu bubu wa semii....mi mimi mdogo.......go gogo la mti ti tina na mjuba..ba...

Nmekumbuka enzi zile kitu ya kombolelaaaa...

Banda umizaaa.....dj afro...
Pale moro, mafiga..real miss

Moro Mafiga, Mtaa gani mkuu?
 
Nakumbuka enzi zangu za ufundi wa magari ya waya...alaf chini unafunga suspensions za makoa ya kufungia mbao za kenchi...kitu kinakuwa na mneso aka mnepo hadi nkilala usiku nlikuwa naota magari ya waya tu.....

Later tukahamia mwanza nkakuta kuna mafundi wa magari ya matete or mabingobingo....ambayo unaweza kuyageuza in any structure kutokana na mahitaji yako...mf tukitaka kucheza kivita vita bas mnayakata na kuyakunja kuwa bunduki...Shuleni pale butimba pr school kulikuwa na kilimo cha bustani za nyanya..ambazo asbui tunazilima na jion tunarudi kuziiba...

Pia msimu wa maembe kulikuwa na ufundi wa kutengeneza vitanda juu ya miti, tulikuwa tunapanda kwny miembe na chumvi tu....dah
 
Hakuna mchezo wa mpira mtamu kama one touch

Dah nakmbk mnaanza gemu saa mbili asubuhi mnatoks saa saba kwa ajili ya msosi then mnalianzisha mpaka kumi na mbili.....mtu unatoka umechoka chepechepe afu ukilala usiku ukiamka asubuhi kitanda kama bwawa vile....
 
We ulikuwa unabadilishana na mkaka au mdada nguo?

Mitoto ya siku hizi iulize kuhusu series za kikorea tuuu,

Yeyote tu..sana sana wakaka. Si unajua mtaani pale kitoto toto Kila mtu anakuwa na crush wake,basi wakisema Leo ya kubadilishana nguo Kila mtu anamuwahi wake.
 
Kwetu kulikuwa na mchezo unaitwa msindi kuinama,ukijisahau uiname unakula teke la adabu huko nyuma..
 
Na kulikuwa na zile mambo za kuwawekea wadada vioo chini kuchungua bahasha zao shuleni, ila omba usikamatwe na mwalimu maana utazeeshwa kwa kipondo...

Kuna anaewajua fukufuku....unamwimbia..fukufuku toka, baba yakoo kaja,.......... Akitoka unaenda kumwekea msichana kwenye manyonyo....eti yatakuwa makubwa fasta...dah..it was funny
 
1.Kibaba baba na kimama mama hehhehehehhe
2. Mdako
3. Tulikuwa na yale madoli basi tunapishana tu kuyafanyia birthday party. Tunajipikilishaje
4. Ukuti Ukuti, wameme wameme

Afu kulikuwa na ice cream za vijiti a.k.a ice cream za uchoyo.

Kimama mama Kila siku walikuwa wananieka mtoto..nlikuwa sipendi mimi kutumwa dukani af wenzio wanaingia kwenye banda la kuku eti ndo chumbani.

Kuchezesha vichupa sijui unaikumbuka hii..

Ice cream za uchoyo teh..a.k.a nimeshatemea mate hakiombeki
 
Back
Top Bottom