Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vichupa ni ile rede ya Vichupa au?Kimama mama Kila siku walikuwa wananieka mtoto..nlikuwa sipendi mimi kutumwa dukani af wenzio wanaingia kwenye banda la kuku eti ndo chumbani.
Kuchezesha vichupa sijui unaikumbuka hii..
Ice cream za uchoyo teh..a.k.a nimeshatemea mate hakiombeki
Vichupa ni ile rede ya Vichupa au?
Teh kibaba baba na kimama mama sio kizuri kwa watoto. Kuna muda wanafanyaga kweli[emoji85] [emoji85]
Wee me hadi zamani nishawahi kuona, usicheze na akili za watoto. Sijui wanajulia wapi mambo hayo, watoto wa dot com wanacheza basi hawaHahaa..labda siku hizi ndio sio nzuri sababu ya utandawazi. Zamani wala haikuwa na madhara.
Nakumbuka enzi zangu za ufundi wa magari ya waya...alaf chini unafunga suspensions za makoa ya kufungia mbao za kenchi...kitu kinakuwa na mneso aka mnepo hadi nkilala usiku nlikuwa naota magari ya waya tu.....
Later tukahamia mwanza nkakuta kuna mafundi wa magari ya matete or mabingobingo....ambayo unaweza kuyageuza in any structure kutokana na mahitaji yako...mf tukitaka kucheza kivita vita bas mnayakata na kuyakunja kuwa bunduki...Shuleni pale butimba pr school kulikuwa na kilimo cha bustani za nyanya..ambazo asbui tunazilima na jion tunarudi kuziiba...
Pia msimu wa maembe kulikuwa na ufundi wa kutengeneza vitanda juu ya miti, tulikuwa tunapanda kwny miembe na chumvi tu....dah
Daah..Umenikumbusha Tina na Mjuba..Kipindi hicho Tausi iko hot mbaya...wakina Dama,Siti bin Kasri,Kalumanzira,Rhoda,Lindi, Balaza n.k ....Kitambo sana aisee
Tobo bao kakaHakuna mchezo wa mpira mtamu kama one touch
Yani kumbe zamani mnaizungumzia hii zamani ya Juzi wakati TV tayari zipo?? Ama kweli tumetofautiana.
Mzee mwenzangu Dark City njoo ushuhudie zamani za vijana wetu uburudike kidogo.
Mkuu kama serikali ya nchi ingekuwa na mfumo mzuri leo hii ungekuwa unafuma kbs magari.
Unafahamu doba ngumi?
Hahaa..labda siku hizi ndio sio nzuri sababu ya utandawazi. Zamani wala haikuwa na madhara.
zamani ipi unaizungumzia wewe,watu tulikua tunagongana kiukweli kweli mkuu?
kuna hili songi nimekumbuka
Mungu mkubwa, bwa bwabwa na samaki, ki king majuto, to tone la maji, ji jitu la kale, le lenye midevu, vu vumbua dhahabu........Nimesahau linaendeleaje