Tujikumbushe Wachezaji ambao ni ndugu Katika Soka!

Tujikumbushe Wachezaji ambao ni ndugu Katika Soka!

Ni kweli Mkuu! Walikuwa wanasafiri kwa Treni afu behewa lao limeandikwa KIBOKO YA VIGOGO! Pale JAMHURI Morogoro, Mnyama alipigwa 4-2! Hao akina MASENGA tayari washamtoa MASENGA mwengine anachezea MTIBWA na alicheza ile Fainali ya U20 v Azam FC ambayo MTIBWA akaibuka bingwa!
Umenikumbusha mtu huyu hamad said masenga waqt huo reli kweli ilikuwa kiboko ya vigogo bila kumsahau Ali malilo loketo au kidudumtu.
 
Mathew & Sean longstaff
IMG_20191006_225448.jpeg
 
Mm nliwajua wa4! wengine ni BONIFACE NJOHOLE (Reli, Morogoro) RIP na mwingine RENATUS NJOHOLE (Yupo Uswizi) kwa sasa! Huyo Boniface Njohole alichezea Reli ikiwa na akina David Mihambo, Kilambo, Duncan Mwamba, Peter Mjata, Madundo Mtambo (Prof. SUA), MWANAMTWA, Magosso na wengineo
Nico na Deo Njoole walikuwa kama watatu hivi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana. Shomari Kapombe ni mtoto wa mchezaji wa zamani kutoka Morogoro, SALUM KAPOMBE
Lila Shomari na Alan Shomari, mmoja alikuwa Simba mmoja Yanga.

Ila sijui kama huyu Shomari Kapombe naye ni uzao wa hawa?
 
Hapana. Shomari Kapombe ni mtoto wa mchezaji wa zamani kutoka Morogoro, SALUM KAPOMBE
Ahsante kwa taarifa, na vipi kina Lila Shomari na Alan Shomari kama una taarifa yoyote?
 
Wengi mnooo mkuu, sijui huyu rui costa na victor costa nyumba nao ni ndugu!!!
Diego milito, gabriel milito
Kolo toure, yaya toure
Kasper, peter schemeichel
Brian na michael laudrup
Jordi na johan Cruyff
Kina pogba
Justin na patrick kluivert
Simeone na paul inzaghi
Adur na edu gudjohsen
Frankie na ronald de boer
Zidane na enzo zidane
Paul na cesare maldini
Etc.
Sent using Jamii Forums mobile app
huyo Simeon na Philiph inzaghi ni MTU mmoja hakuna wawili
 
Soka ni mchezo wa aina yake, unafatiliwa na mamilioni ya watu ulimwenguni. Kuna baadhi ya wachezaji wametoka katika familia za soka. Unakutana baba na wanawe au mtu na kaka, mjomba, binamu yake wote wamecheza soka kwa kiwango cha juu. Mfano kwa Tanzania kuna akina Salum Swedi na Said Swedi. Hawa ni mtu na kaka yake.

Karibuni wadau tujikumbe wachezaji wa soka ambao wana undugu, iwe bongo au ulaya!
Sunday Manara na Kitwana Manara na Kassim Manara, Peter Tino, Emma Peter , Gebo Peter, Abassi Dilunga, Maulid Dilunga, Haidary Abeid na Khalid Abeid, Issa Athumani Na Kassongo Athuman , Madaraka Selemani na Iddi Selemani nk
 
Back
Top Bottom