Na Haji Manara Na Mpira wake wa Mdomoni
Watu wa Kigoma wamejaaliwa Vipaji Kila eneo walilopo
Kwenye Mpira, kwenye dini, kwenye ushirikina, kwenye ubishi, kwenye Biashara n.k
Hawa Jamaa Mkoloni angewapiga Shule Kama alivyofanya Kwa Wachagga Na Wahaya Pengine ingekuwa ishakitenga Kama Eritrea kutoka Ethiopia
Heshima kwako Mkuu,
Naunga mkono maelezo yako kwa asilimia nyingi sana,
Kwa kweli Kigoma vipaji vipo vingi sana japo hupotea kutokana na baadhi ya changamoto kama mazingira yasiyo rafiki kuviendeleza vipaji na hali tete katika masuala ya uchumi katika mkoa wa kigoma,mzunguko wa pesa ni mdogo sana lakini Chakula na ardhi ipo ya kutosha na inahimili mazao mengi,
Katika soka watu walio wengi wanaweza kucheza mpira vizuri sana,
Mimi nimepata kusoma Shule ya msingi kigoma, Mama yangu Muha na Baba yangu mnyamwezi hivyo waweza kuniita Muha/mnyamwezi pia nimeweza kushiriki moja ya copacocala kuwakilisha Kigoma...
Kunajamaa yangu mmoja nilikuwa namtania kipindi cha nyuma kwamba Kigoma ikipata viwanja bora na vifaa bora vyamazoezi vijana wakijifua vilivyo Taifa star's hawawezi nusu atapua watachalazwa vibaya mno nanilimwambia hivyo kwa kuwa nilipata kutembelea mikoa mingi,arusha,tanga,kagera,dodoma,singida,Moro,Shinyanga,iringa n.k na nikawa najitahidi kwenda kutazama mazoezi ya mpira jioni.
Sasa tuwatazama watu wakigoma kwa uchache kidogo.Watu wa kigoma Ubinafsi (umimi) wengi huwa hawashikani mikono kuinuana ili wakwende pamoja kama baadhi ya watu wa mikoa mingine wafanyavyo,Ubahili,Ubishi,kuendekeza imani za kishirikina lakini jambo zuri huwa ni wachapakazi sana,hawakati tamaa,hawachagui kazi,hawapendi kumbuluzwa.
Kigoma vipaji vipo vingi,Tanzania ikiweka mfumo mzuri wa soka mawakala wa soka muitembelee kigoma mkaone maajabu ya soka.
Naamini pia kigoma siku miundombinu ikiwa ya uhakika na bora na Umeme wa uhakika bila kusahau kujengwa kwa vyuo na shule nyingi kigoma itashangaza wengi katika nyanja nyingi.