Tujikumbushe Wasukuma waliowahi kucheza soka

Tujikumbushe Wasukuma waliowahi kucheza soka

Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    24.9 KB · Views: 46
Mmoja kati ya wachezaji bora kabisa kutokea dereva huyo wa garimoshi enzi hizo kukiwa na mashindano ya mikoa (sunlight )yakifanyikia uwanja wa ilala (karume )walitwaa kombe hilo miaka mitatu mfululizo akiwa na juma mrisho nae alikuwa mwamba waqt mmoja wamekwenda uganda kucheza kombe la Gossage (challenge cup )mkewe a kajifungua huko basi alipotumiwa ujumbe atoe jina akatoa jina la mashindano (Gossage )kijana akakuwa na jina hilo la Gossage mrisho.
 
Japo mimi sio mshabiki wa michezo lakini nachangia kidogo.
Wiki iliyopita nilitoka Moshi - Mwanza. Nikapanda gari ya Kampuni ya Mohamed Trans iliyokuwa imetoka Tanga - Shinyanga. Nilisikitika moyoni jinsi kondakta wa gari hiyo anaitwa Paul John Masanja alivyokuwa natoa ushuhuda kuwa alikuwa mchezaji tena alichezea timu ya Taifa, akawa anataja nchi mbalimbali walizokwenda kucheza.
Mwishoe akahitimisha kuwa, "namshukuru Mungu sijaadhirika kama waliokuwa wachezaji wenzangu japo nimepata kazi ya ukonda wanangu wanakula. Ila kama nikuchezea hela nilichezea hela. Hapa nina watoto wa nje 11....."
Paulo John Masanja ni muongeaji/mcheshi sana. Ukikaa naye hutachoka kumsikiliza. Ni msimuliaji mzuri na ana stori nyingi...hasa za wanawake na vituko vya wachezaji na michezo; mambo ya ulozi kwenye soka, vibweka vya wachezaji, ushamba wa wachezaji, na kadhalika. Kifupi ni mtu mzuri, anayecheka na kila mtu na anayependa utani.
Alicheza Young African (Yanga) na timu ya taifa kwa mafanikio kiasi chake. Kama wachezaji wengine wa zama za giza la soka Tanzania hana mafanikio kihiivyo. Ni Msukuma na anaishi Shinyanga. Kwasasa ni kondata katika mabasi ya Mohamed Trans.
 
Back
Top Bottom