Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

...Dominick Chilambo...
Hatupo nae sasa.... Nakumbuka nilisikia sauti yake ya mwisho..live... Tukuyu Stars ilikua uanjan...

RTD ...ilirusha...
RIP.
 
Mie nlikuwa napenda kile kitangazo "Wewe acha kula mali ya uma, wewe acha kujitafunatafuna kama punguani, wewe!" Teh! Teh!
 
....hii je...?

"shambani shambani
"twende tukalime mazao bora shambaniii"
 
saa moja jioni kipindi cha kahawa....lol.....na kale kanyimbo chake..."kahawa ni zao lenye faida kubwa"".....cjui nini nini......!!!! au wakati wa adhuhuri hapo kitu cha dongo kipo jikoni kitu ndani ya chungu hadi kina abuu wanapata harufu yake....lol
 
kipindi cha majira saa tatu na ule wimbo wa kuashiria kipindi kinaanza na lile tangazo la sabuni ya komoa"nipeni maji nifueee komoa sabuni ya komoa komoa"ilikua burudani tosha
 
..hihi je: boomuu boomuu bomuuu eeehhh....watu wote wanazaaa....bwana bomuuu kazidiiishaa weee....!!!
afu kulikuwa na kipindi flani hivi majira ya saa moja usiku kilikuwa kinahusu igizo la kuhamasisha mambo ya maji...kuna mzee mmoja hivi alikuwa mbishi vibayaaa....sijui kilikuwa kinaitwaje kile kipindi!!
 
Deborah mwenda (mama na mwana) ua jekundu,mazungumzo baada ya habari. karibun watotoo woote,tufurahi watotoo wotee.
 
Sikiliza bwana umemeeee cjui ilikuwa ni kila juma ngap ah kitambo sana
 
Alafu kuna kialarm fulan kilikuwa kinapga kama ikitokea mitambo kukorofisha au umeme ukikatka rtd.Nduuuu nduuuu ndu ndu ndu nduuuu.Kinadumu kama dk 2 au 3 then afta hapo kumradhi za kumwaga zinafata.Ha ha ha ha ha
 
Bustani ya malenga unaikumbuka? Enz hzo saa 6 mchana njaa inauma sana dizain bi mkubwa au mfanyakaz yupo jikon anapka ugali na mboga fulan huipendiiii.Bas na yale mashairi ndo yanazd kuongeza unenge na hasira fulan.Ha ha ha mbaya zaidi jiran unaskia harufu ya mikarangizo ya kufa mtu kwenda huwez mana bi mkubwa anakukomalia usile kwa watu.Ha ha ha very funny
 
Mwaka ilipovunjika jumuia ya Afrika Mashariki yale mazungumzo baada ya habari kuhusu NYAN'GAU.Klabu raha leo shoo ambapo bendi zilitoa nyimbo zao mpya walizorekodi rtd.Mikingamo kilijaa unafiki kwa kuwatoa kafara vidagaa na kuyaacha mapapa na nyangumi.Pwagu na Pwaguzi.Kijaruba na Abdala Mlawa.External service Ras T (sasa Baba T wa EA radio) alikuwa na kipindi cha muziki wa reggae siku ya ijumaa au jmosi.Na msituko waliopata wasikilizaji wa kipindi cha michezo mtangazaji maarufu wa kipindi marehemu Abdul Masudi Jawewa alipoacha kazi rtd na kwenda ajiliwa kwa Virani.Matangazo ya moja kwa moja(live) siku kiongozi wa chama cha wapigania uhuru wa msumbiji FRELIMO marehemu Samora Machel alipokuwa akiwasuta hadharani wasaliti wa harakati hizo kutokea nachingwea.Matangazo ya moja kwa moja ya mazishi ya marehemu Edward Sokoine na Cardinal Rugambwa.NITARUDI BAADAE.
 

Namkumbuka Tesha.
Nakumbuka siku anatangaza kustaafishwa u RPC bwana Maji.
Namnukuu:
"Habari kamili, Dar es Salaam.
Serikali imemstaafisha kwa manufaa ya umma, kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dar es Salaam, Bwana Tryphone Maji."
 
Juma Ngondae, Salim Mbonde na Abdul Ngarawa walikuwa wataalam wa "Mazungumzo baada ya habari",
yakiratibiwa kwa karibu na Paul Sozigwa.
 

Ni Jumamosi aisee, si J2. Marudio J3, saa 11.02 jioni.
 

I like this!
 

Hapo ulipoandika "wananchi" kulikuwa na neno "wazalendo"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…