pascal, hawa nao huwakumbuki? Dastan Tido Mhando, Chama omari Matata, Godfrey Mngodo, Teckla Gumbo, (Salim?- Mume wa Zamzam Maalim),Ahmed Kipozi, Julius Nyaisanga, Sango Kipozi, Abdul Omar Masudi, Mshindo Mkeyenge etc
Ahmed Kipozi na Sango Kipozi are they couples?
Esha Mihidimi Nilimsikia Wakati Tbc Inaanza Nikajua Ni Mtangazaji Wa Juz Juzi, Akatangaza Siku Kadhaa, Nilipenda Saaaaana.............. Si Akaondoka Ghafla, Yaani Hata Sijui Yuko Wapi?
Hiki ni kikosi cha first 11 ya Radio One.
Waliokaa kutoka Kushoto ni Charles Hilary kwa sasa yuko BBC-London
Mikidadi Mahamod (Brother) sasa ni Mkurugenzi wa Radio Uhuru, Mzungu Mike Ross, na Uncle J. Nyaisangah.
Waliosimama toka kushoto, Deo Mshigeni yuko US, Monica Mfumia yuko UK, Florah Nducha ni Mkuu wa UN Radio New York, Vicky Msina, ni PRO wa BOT, Aboubakar Liongo yuko DW-Radio ya Ujerumani, Lilian Mbaga sasa ni Mkurugenzi wa TGNP, Sunday Shomari yuko VOA na Taji Liundi sasa ni Meneja wa PRT ya TBC.
Jamani yuko wapi mtangazaji huyu Sekione Kitojo
Ni media manager wa Mlimani Media na mkufunzi wa utangazaji wa IJMC.Kuna wakati alikuwa Tume ya Uchaguzi ya Kiravu, sasa hasikiki tena , labda amekua freelance ? Pengine Pasco aje kutusaidia
Ni TSJ na sio DSJ!. Ndicho tulichosoma sisi, kilikuwa Ilala Shariff Shamba ndani ya campus ya BASATA, kilipohamishiwa UDSM, eneo liule ndipo kikaanzishwa DSJ.Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Shule ya Mawasiliano ya Umma, zamani ikiitwa DSJ
Mkuu Bramo hajapotosha.
Marehemu Ally Saleh ni cousin wangu.
Alifariki wakitoka kazini na gari ya TBC kwa kugongwa na treni kwenye crossing ya Ilala Shaurimoyo.
Walikuwa watatu:-
Ally Saleh, Kwege Munthali na mwingine jina limenitoka.
Matembele, asante kunikumbusha hiki kisa na majina na majina ya watangazaji hawa, by the time tunajoin RTD, kiliishatokea zamani kikihusishwa na ushirikina!.Mkuu Bramo hajapotosha.
Marehemu Ally Saleh ni cousin wangu.
Alifariki wakitoka kazini na gari ya TBC kwa kugongwa na treni kwenye crossing ya Ilala Shaurimoyo.
Walikuwa watatu:-Ally Saleh, Kwege Munthali na mwingine jina limenitoka.
Matembele, asante kunikumbusha hiki kisa na majina na majina ya watangazaji hawa, by the time tunajoin RTD, kiliishatokea zamani kikihusishwa na ushirikina!.
Details haziko very clear ni walikuwa wanatoka shift au wanaingia shift ila gari ni landrover 110, ilikuwa na watu 8, watangazaji 4, fundi mitambo 3 na dereva, walipofika rail crossing gari ikazimika katikati ya reli, treni inakuja huku ikipiga honi, dereva na mtu wa mbele walifungua milangoi wakashuka, na wale watu watatu wawili nyuma pia wakashuka, walibaki watangazaji wanne waliokuwa wamekaa siti ya kati!, wote wanne walifia papo hapo!. Majina mawili ndio hayo, bado wawili wengine. Naomba yeyote mwenye details kuhusu ajali hii, atakumbushe vizuri, ila majina nimeta update kule mwanzao!.
Pascal.
Ni sekioni yupo DW ujerumani, kila uchao hutangaza
kama sikosei yule mama alikuwa anaitwa deborah mwenda,yaani acha bwana zile ndio zilikuwa enzi za utangazaji,kwa tuliokuwa watoto kipindi kile kukosa kipindi cha mama na mwana ilikuwa kosa kubwa!Duh mmenikumbusha mbali sana.nilikuwa nakipenda sana tena sana kipindi cha mama na mwana.sikumbuki jina la mtangazaji ebu nikumbusheni wajf.nilikuwa sikosi kipindi .yaani nakosa raha nisipokisikiliza .hivi yupo yule mtanganzaji?? Pia kile kipindi cha zilipendwa kila jumapili nilikipenda sana