Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV


Asanteni kwa taarifa, nime update list, sasa idadi ya Watangazaji wa iliyokuwa Radio Tanzania, Dar es Salaam (RTD) wamefika 31!, kwa taasisi moja, waliofanya kazi ndani ya jengo moja (BH) pale Pugu Rd, vifo vya watu 31, ni vingi mno!.

Pascal.
 

Kuna vitu viwili hapa, eidha umri wangu haujaenda sana kama ninavyodhani au hawa ni wakongwe wa zamani sana. Yaani angalau kwa mbaaaaali nimewahi sikia jina la Omar Jongo pia Halima mchuka. Namkumbuka Sued Mwinyi na Nkamia mpirani. Ila nina uhakika hao kwenye list walikuwa balaaa.
 
[h=3]Mkuu Watu8, Asante kwa taarifa, nime update list, sasa idadi ya Watangazaji wa iliyokuwa Radio Tanzania, Dar es Salaam (RTD) wamefika 31!, kwa taasisi moja, waliofanya kazi ndani ya jengo moja (BH) pale Pugu Rd, vifo vya watu 31, ni vingi mno!.[/h]
Pasca
 
Barafu, utakuwa dogo, enzi hizo redio ilikuwa moja tuu, RTD, na kulikuwa hakuna TV, hivyo wale wa zamani, haya ni majina ya kawaida sana!, na huo uliowataja, wa zamani ni Jongo, wengine ni wa juzi kati!.

Pascal.
 
Wadau hivi Jacob Tesha yuko wapi siku hizi?
 

Dada Yetu Restuta Bukoli sijaona jina lake.
 
Kharid Ponela nae ametutoka lini jamani, RIP watangazaji wote wa RTD, sitokuja kumsahau Siwatu Luanda, yule dada alivyokufaga nilitoaga machozi
Mkuu Ram, Ponera alitutoka siku nyingi!, ila Siwatu alitangulia sana!, alikuwa na mguu hatari!.

RIP Ponera, RIP Siwatu.

Pascal.
 
Wadau hivi Jacob Tesha yuko wapi siku hizi?
Jakob Tesha yupo, ni mstaafu, mara mwisho alikuwa wizara ya Habari na Vijana na Utamaduni. Sasa hivi yeye na Edda Sanga wana kampuni ya ushauri wa habari, wanaishauri Mlimani Radio na TV.

Pascal.
 
Dada Yetu Restuta Bukoli sijaona jina lake.
Mkuu Masuke, naomba tukumbushane details, alikuwa ni mtangazaji wa lini, vipindi vyake, na alitangulia lini mbele ya haki, ila sio lazima kutaja kilichomtanguliza!.

Pascal.
 
Mimi nakumbuka kipindi cha mama na mwana japo sifahamu kama mama yetu yu hai alitusimulia hadith ya adili na nduguze, kidogo nakipindi cha kombola tulikua kambi ya umishumta bahi sokoni muda huo mwalimu ndyo aliutumia kutuamsha kuanza mazoezi,daa kweli sasa tumezeeka.
 
Mkuu Masuke, naomba tukumbushane details, alikuwa ni mtangazaji wa lini, vipindi vyake, na alitangulia lini mbele ya haki, ila sio lazima kutaja kilichomtanguliza!.

Pascal.

Nakumbuka alikuwa anaripoti kutoka Shinyanga hasa kipindi cha majira asubuhi na usiku, na wakati TBC1 (TVT wakati huo) ilivyoanza akawa anaripoti kwenye taarifa za habari za TV kutokea Shinyanga huko huko.

Sikumbuki hasa ni miaka ipi alianza kutangaza, hata mwaka aliofariki exactly sikumbuki ninachokumbuka ni kwamba alifariki kipindi cha Kikwete inaweza kuwa kati ya 2006 na 2007 kwa sababu Kikwete alihudhuria ule msiba na mazishi yalifanyika mkoani mwanza sehemu moja inaitwa Kisesa.
 
Masuke, asante kwa taarifa, kumbe huyu ni Mtangazaji wa RTD ya juzi ilipokuwa TBC!, hawa karibu wote ni watangazaji wa zamani iliyokuwa RTD kabla haijawa TBC.

Hata hivyo nimemuongeza kwenye list.

Thanks.

Pascal
 
Udaa, Kipindi cha Mama na Mwana ni cha Deborah Mwenda, sasa hivi amestaafu, ila anaendelea na kipindi TBC-1
 
Masuke, asante kwa taarifa, kumbe huyu ni Mtangazaji wa RTD ya juzi ilipokuwa TBC!, hawa karibu wote ni watangazaji wa zamani iliyokuwa RTD kabla haijawa TBC.

Hata hivyo nimemuongeza kwenye list.

Thanks.

Pascal

Ameanza kutangaza wakati huo ikiitwa RTD.
 
michael katembo kipindi cha mkoa kwa mkoa duh mara ya kwanza nausikia wimbo wa kila munu ave na kwao. zamaniiii
 

Huo wimbo naupenda sana.
By the way Salama Mfamao alikuwa sister wako sana au "sister wako sana"?
 

Malima Ndelema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…