Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Na idhaa ya biashara ilikuwa inaanza kwenye kumi na robo hivi,pia nakumbuka matangazo ya radio yakikata gafla kabla hayajarudi tena kulikuwa na kaspecial alarm kanagonga kama dk moja hivi halafu matangazo yanarudi kwa mtangazaji kuomba radhi kwa kukatika matangazo
 
jumapili sa nane mchana nakumbuka ilikuwa NIPE HABARI,kikitangazwa na mkurugenzi DAVID WAKATI...ndio kipindi pekee ambacho Wakati alikuwa anatangaza,ukimsikia sauti yake mara nyingi itakuwa kuna jambo zito la kitaifa.

Kwa kweli ilikuwa ni zamani, lakini sidhani kama Jumapili kulikuwa na kipindi cha aina hiyo hiyo mida, najua kulikuwa na kipindi cha kanisa asubuhi kulikuwa na makengele yanalia, kisha kulikuwa na kipindi cha watoto mashuleni, zilipendwA, salamu za wagonjwa kisha habari,
Kwa jioni nadhani kuliwa na cheichei, kipindi cha dini, nadhani na club rahaleo show

Inawezekana kaka ni muda umepita kwa kweli
 
kweli mkuu ni kitambo kirefu inawezekana nami nimechanganya
 
Acha kabisa kwa kweli hizo zilikuwa enzi, hao watangazaji walikuwa na uwezo wa kutengeneza sauti na kizifanya ziwe pich kabisa, hadithi kama ya UA JEKUNDU, yule mama alikuwa anasimulia kama senema vile

Kwa kweli ulikuwa sahihi kutengeneza picha za hao watangazji kwa kutumia sauti na hiyo ilikuwa kwa kila mtoto
 
Ni kweli Ben kiko aliripoti kwa namna ya kutukatisha tamaa watanzania kutoka mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya Nduli Idd Amin Dadaa.
Fundi mitambo wa kutumainiwa na kutegemewa RTD walikuwa, crispin Lugongo, Noel Namaloe, Ally Said Tunku......
Watangazaji wa mpira wenye utani wa jadi na kuwa kivutio kikubwa kwa wasikilizaji walikuwa Ahmed Jongo na mwenzake wa simba.

Kipindi cha misakato kikiandaliwa kwa ustadi mkubwa. Vipindi kama malenga wetu, kijaluba, mkoa kwa mkoa, vijana leo n.k vilikuwa na mvuto wa pekee.

Mama na mwana, chei chei shangazi,pwagu na pwazi (p & p co. Ltd) mzee jangala, kidole, kiatu, mzee mundu (kwa udhamini wa kibuku) havitapata mpinzani japo havipo hewani.

Majira, mikingamo, salamu za wagonjwa, taarifa za habari, kila mtu alipenda kuvisikiliza

Tangazo la mabati ya galco nalikumbuka sana. Revola, philips ndio yenyewe......., National, n.k

Watangazaji walikuwa mahiri sana, kina Juma Ngondae, Julius Nyaisanga, Salim Mbonde, S. S. Nkamba, Abdul Ngarawa, Eda Sanga, Mikidadi Mahmud, Jackob Tesha.............

Mazungumzo baada ya habari yamewajia kutoka redio tanzania dar es salaam.
 
Nina Uncle wangu anaitwa Chupaki,alikuwa anapenda sana kubandika magazeti ya katuni chumbani kwake.Huenda ndicho chanzo cha jina lake
Umenichekesha madam,ila na mimi nilikuwa na likitabu kubwa ambamo nilikuwa nazikata hizo katuni na kuzibandika pia na picha za mpira,lakini mimi namshukuru mungu nimenusurika kuitwa chupaki.
 
Aksante mkuu
 
Aksante
 
Umenichekesha madam,ila na mimi nilikuwa na likitabu kubwa ambamo nilikuwa nazikata hizo katuni na kuzibandika pia na picha za mpira,lakini mimi namshukuru mungu nimenusurika kuitwa chupaki.
Nami pia na mdogo wangu tulikuwa tunabandika za Chakubanga. Sasa kuna mjomba wetu alikuwa nje ya nchi alipokuja alifurahia saana na kuzisoma zote. Natamani ningekitunza mpaka leo. lakini baadae walianzisha kama kitabu hivi cha Chakubanga. jamani old is gold!
 
Umenichekesha madam,ila na mimi nilikuwa na likitabu kubwa ambamo nilikuwa nazikata hizo katuni na kuzibandika pia na picha za mpira,lakini mimi namshukuru mungu nimenusurika kuitwa chupaki.
Basi mimi ntakuita kimoyo moyo kaka yangu
 
Ratiba ya ndege kipindi cha ATC hewanii saa nne na robo usiku,duh eti leo tuna ndege moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…