Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Ah ah ah aj ah we nomaaa kaka
 
Da kulikuwa na vipindi vizuri kama vile:

1. Duniani juma hili (jumapili mchana) hapo akina Sekione Kitojo, Mohamed Dahman, Nasoro Nsekeli, Abisai Stephen kabla hajapelekwa Songea.

Wakati mwingine marehemu David Wakati alishika usukani wa kipindi hicho, na bila kumsahau Abdalah Mbamba kutoka redio ya umoja wa mataifa.

2. Kipindi cha Harakati (saa kumi jioni) na Albert Misemembo akishirikiana na marehemu Saraha Dumba.

3. Mikingamo - hiki kilisimamiwa na Abisai Stephen kabla ya kwenda Songea.

4. Mchezo wa redio - kila ijumaa saa mbili na nusu usiku ambapo akina mzee Jongo, babu Kipara (Fundi Saidi), Zena Delep, Mariam Yusuf na Ajuae hawakukosa.

5. Kipindi cha Ugua Pole, na watoto wetu kila jumapili asubuhi.

6. Wakati wa kazi kila siku saa tano asubuhi.

7. Majira asubuhi saa 12:30na usiku saa 3:00- hapa wakongwe kama Salum Mbonde, Abisai Stephen, Tumbo Tamimu Risasi, Peter Makorongo, na Chisunga Stephen hawakukosa kukiendesha kipindi hiki.

Pia mikoani walikuwa na wawakilishi kama Saidi Mtaalam, Ben Kiko, Mshindo Mkeyenge na wengine wengi.

Pia mkuu kuna nyuzi kadhaa zinazohusu watangazaji wa zamani wa RTD kupitia jamaa yetu Pascal.

Tuwakumbuke Watangazaji Wa Zamani wa Iliyokuwa RTD Waliotangulia Mbele ya Haki!
 
Ukitaka kutoa wimbo kama umeandika neno mapenzi linakatwa inatakiwa mapendo
 
Zilipendwa, mikingamo, majira, mahoka, kipindi cha shule, kipindi cha wagonjwa kila jumapili, watangazaji enock ngombale, tido mhando, masudi, Charles Hillary, Edda sanga, na wengi
 
Umesahau haka sadiki mbona unajikuna ngwalala ngwalala tumia sabuni ya foma namimi nimekasahahu kidogo nikumbushe
 
Namkumbuka upande wa michezo, ezekel malongo pamoja na harima mchuka walikuwa wananipa raja sana hawa Watu wanapotangaza Mpira.
 
Mazungumzo baada ya habari, ngoma za Mzee moris kabla ya taarifa ya habari, mama na mwana, taarifa za safari za meli(sea star), kujiunga na sauti ya Tz Zanzibar, pia lile tangazo la rushwa~~Rushwa ni mdudu mbaya mwenye sumu Kali, akikung'ata!! Ukipona bahati yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…